Mgogoro dayosisi ya Mpwapwa

Mgogoro dayosisi ya Mpwapwa

Baadhi ya dinari na pareshi zilivutiwa na sera zake hadi kupelekea wasiwasi kwa viongozi wa dayosisi na kanisa anglikana kwa ujumla.

Kamati ya uchaguzi iliondoa jina lake tena wakati uchaguzi ukiwa umeshafanyika kwa madai kuwa Kuta hana vigezo,jambo mojawapo lililosemwa ni kuwa bwana Kuta anajihusisha na masuala ya mapenzi ya jinsia moja.Ikumbukwe kuwa Kuta anatokea maeneo ya kanda ya Mlali ambapo ndipo hasa kwenye mgogoro mkubwa,baada ya kuondolewa kwake zaidi ya makanisa 80 yaliyopo kanda hiyo ya Mlali yaliamua kujitoa dayosisi ya Mpwapwa.
Ugomvi wote makanisani ni pesa, ifike mahali sasa makanisa yatoe huduma bure, na hao makasisi watafute kazi za halali za kuwaingizia vipato badala ya kugombania sadaka
 
Ushamba mkubwa uliowahi kutokea duniani ,watu wagombane wengine ila chuki zisambazwe kwa wengine.

Si dini ,nchi hata ngazi ya familia watu wanaweza kupishana kauli na kupelekea utengano ila ni sawa kwa vile ni binadamu na wote tuna dhambi.

Ujinga 👉Panapotokea ugomvi basi wale waliogombana ndio wanahusika ila wengine hapana ,utengano wa viongozi ndio chanzo cha kugawa watu na kupelekea upotofu ,hapa kama viongozi lazima watabeba dhima maana wameaminiwa ila wao wanaangalia maslahi yao binafsi.

Enyi viongozi! Kuweni waadilifu na wekeni maslahi yenu kando kuna watu wanawaamini sana.
 
Kanisa langu la Anglikana na KKKT kwa kweli MUNGU atusaidie.

Ukisikia chaguzi za viongozi wakubwa, tambua ni muda wa matatizo ndani ya kanisa umewadia.

Shetani ametamalaki kwa viongozi wetu wanaotanguliza maslahi binafsi ya tumbo kuliko wito wao wa kiutume wa kuchunga kondoo walioitiwa.
 
Ugomvi wote makanisani ni pesa, ifike mahali sasa makanisa yatoe huduma bure, na hao makasisi watafute kazi za halali za kuwaingizia vipato badala ya kugombania sadaka
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom