Binafsi nichukue nafasi hii kuwashukuru Halima Mdee na Jafari Chege kwa kuwasemea Wananchi wa maeneo haya kuhusu manyanyaso ya Serikali dhidi yao.
Nianza na Kata ya Nyatwali. Kata hii ina vijiji vitatu Tamau, Nyatwali na Serengeti. Vijiji vyote viko kisheria na vilianzishwa tangu mwaka 1972 na vina hati halali. Mwaka 2014 kulitokea hoja kuwa vijiji hivi vinapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na hivyo ni vema vikapisha ili kuwe na mapito ya wanyama mpaka ziwani kwa ajili ya maji na wanyama kuwa huru.
Hoja hii ilipopelekwa mbele ya Baraza la Mawaziri Awamu ya Tano Mwenyekiti akiwa Hayati Mhe. Magufuli alilikataa hoja hii na akasema Wananchi wasisumbuliwe na Wananchi wa Kata ya Nyatwali wakapewa mrejesho juu ya suala hili.
Awamu ya sita ilipoingia madarakani hoja hii ilifufuliwa upya na hatimaye wakaanza tathmini kuhusu mali za Wananchi. Hata hivyo malipo yaliyopendekezwa hayalingani na hali halisi na maisha ya sasa. Wananchi wanapendekeza kuwa ekari moja walipwe kiasi cha Tshs.10,000,000 kwa ekari lakini uthamini wao wanapendekeza Tshs.2,000,000 kwa ekari kitu ambacho hakiendani na hali ya sasa.
Pili, kuhusu Kijiji cha Utegi. Kijiji cha Utegi kimekuwapo tangu operesheni Vijiji na wananchi wameishi pale takriban miaka sitini sasa. Leo hii wanaambiwa wahame na kwa kejeli cha kuambiwa kuwa watalipwa kifuta machozi. Hili ni jambo la ajabu kabisa na wanakaa nje ya beacons za Shamba la Mifugo la Utegi.
Ninamwomba Mhe. Rais aliingilie kati migogoro hii vinginevyo uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025 wananchi Mkoa wa Mara waikataa CCM.