Mgogoro wa DRC: Viongozi wa Africa hawawezi kufanya maamuzi, waache unafiki

Mgogoro wa DRC: Viongozi wa Africa hawawezi kufanya maamuzi, waache unafiki

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Iko wazi kuwa kweli banyamulenge wana haki ya kuwa raia wa Congo na kupata haki zao zote za msingi kama raia wa nchi hiyo.

Lakini je, inapofikia raia hawana uzalendo tena na nchi ambayo kimsingi ni yao na wanaonesha mapenzi na utii kwa kiongozi wa Taifa hasimu tena mwenye asili yao hao bado ni raia au wahaini? Kuna cha kujadili hapo? Hao wakongo gani ambao miaka yao yote wako royal kwa utawala wa Rwanda ni raia wema kweli hawa?

Serikali ya Congo wa si jeshi...Congo na watu/wanacongo wawe serious na nchi yao vinginevyo ni aibu kubwa na mwishowe ni laana.

Pia soma: Mazungumzo kuhusu mgogoro wa DRC na M23 ni unafiki na uoga tu. Wawaambie Rwanda na Uganda ukweli

Kama kweli viongozi wa SADC na EA pamoja na vyombo vyote vya usalama nia yao ni kuleta amani kweli wameshindwa na M23 pamoja na jeshi la Rwanda?

Ni aibu kwa vizazi vijavyo kwa viongozi wa Africa kushindwa kushughulikia mgogoro wa ndani wakati akina Lumumba, Nyerere, Nkwame Nkuruma walikutana na mazingira magumu zaidi.

AU na jumuiya zote za Africa kweli zimeshindwa kuichukulia hatua Rwanda?

Ni kwa mantiki hiyo hiyo Africa tuko nyuma, viongozi wetu hawawezi kuchukua hatua, sababu kubwa pia wao si safi, kumbe mtu ambae hawezi kufanya maamuzi ya kujenga lau sehemu ya kujihifadhi akijisaidia/kuchimba choo...huyo ataweza kujenga barabara, reli, na miundo mbinu mingine kama ya elimu na afya bila kuamuliwa na wengine?

Mungu atuhurumie Africa, lakini atusamehe kwa sababu tunaifedhehesha race ya Africa ulimwenguni kote, kwa kusema au kumwambia Mungu alituumba dhaifu.

Nenda Africa Kusini, America, Brazil nk, asili ya mtu mweusi imekua kama laana.
 
Iko wazi kuwa kweli banyamulenge wana haki ya kuwa raia wa Congo na kupata haki zao zote za msingi kama raia wa nchi hiyo

Lakini Je inapofikia raia hawana uzalendo tena na nchi ambayo kimsingi ni yao na wanaonesha mapenzi na utii kwa kiongozi wa Taifa hasimu tena mwenye asili yao hao bado ni raia au wahaini?kuna cha kujadili hapo?Hao wakongo gani ambao miaka yao yote wako royal kwa utawala wa Rwanda ni raia wema kweli hawa?

Serikali ya Congo wa si jeshi...Congo na watu/wanacongo wawe serious na nchi yao vinginevyo ni aibu kubwa na mwishowe ni laana

Kama kweli viongozi wa SADC na EA pamoja na vyombo vyote vya usalama nia yao ni kuleta amani kweli wameshindwa na M23 pamoja na jeshi la Rwanda?

Ni aibu kwa vizazi vijavyo kwa viongozi wa Africa kushindwa kushughulikia mgogoro wa ndani wakati akina Lumumba ,Nyerere,Nkwame Nkuruma walikutana na mazingira magumu zaidi

AU na jumuiya zote za Africa kweli zimeshindwa kuichukulia hatua Rwanda?

Ni kwa mantiki hiyo hiyo Africa tuko nyuma ,viongozi wetu hawawezi kuchukua hatua,sababu kubwa pia wao si safi,kumbe mtu ambae hawezi kufanya maamuzi ya kujenga lau sehemu ya kujihifadhi akijisaidia/kuchimba choo...huyo ataweza kujenga barabara,reli,na miundo mbinu mingine kama ya elimu na afya bila kuamuliwa na wengine?

Mungu atuhurumie Africa,lakini atusamehe kwa sababu tunaifedhehesha race ya Africa ulimwenguni kote ,kwa kusema au kumwambia Mungu alituumba dhaifu

Nenda Africa Kusini,America,Brazil nk asili ya mtu mweusi imekua kama laana
Uzi una madini mengi sana huu.
 
Back
Top Bottom