Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Burma au Myanmar tatizo ni Military Junta kupindua serikali za kiraia na sio suala la majimbo.
Wewe ndie unajadili kinyume nyume.
Nani kasema tatizo la Mynamar ni majimbo?
 
Hatari sana kamarada.....

Tanzania Iendelee tu kuwa "shock absorber" na sehemu tulivu ya KUPUMULIA matatizo lukuki ya bara la afrika......

My take: Makao makuu ya "AU" yanastahili kuhamishiwa Tanzania

Siempre JMT
 
Hii ni Vita ya pili Ethiopia katika Modern times ile ya miaka ya 70 ilikuwa ni Wananchi dhidi ya Ukomunisti kama huu wa CCM.

Vita ya sasa ni ubabe wa Serikali dhidi ya Wananchi kwa kuwakatalia kufanya Uchaguzi kwa kisingizio cha Covid19.

Tanzania tunahitaji Majimbo ili iwe vigumu kwa CCM kutuburuza.
 
Hilo halimaanishi kuwa utawala wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo yatake kujitenga. Ni uvivu kifikiri hivyo.
 
Mleta mada hujui kwa usahihi unachosema na sitakosea kukuita muongo!! Ingefaa ukaa unachokisema:

a) jambo moja zuri au baya haliwezi kutumika
Kwa ujumla. Umeeleza ubaya wa serikali za majimbo kwa Ethiopia. Ungeenda mbali zaidi na kutuambia ubaya wa jambo hilo kwa nchi kama South Afrika, Marekani, Canada, UK na hata Kenya. Kwa hutujua jambo hili vizuri utabisha kuwa hata Kenya haina mfumo huu, ungependa niseme kaunti badala ja jimbo.
b) si kweli TPLF ni jeshi la jimbo. Ni kikundi cha waasi kikichoanzishwa na watu wa jimbo la Tigray. Sawa na Banyamulenge mashariki mwa DRC. Jeshi la nchi ya Ethiopia lipo na limeshindwa vita eneo la Tigray na kuwafanya waasi washikilie eno.

Ambacho unataka kusema lakini kwa kuficha ni ukandamizaji wa kidemokrasia unaoendelea hapa Tanzania kwa kijisababu cha umoja. Sisi tuna halmashauri zinazoongozwa na chama kilichoshinda viti vingi vya udiwani. Na kiongozi kati halmashauri ni meya. Tungetaka kujilinganisha na wengine, huyu ndio angekuwa juu ya wateule wa Rais kama Mkuu wa wilaya, RAS na mkurugenzi. Wenzetu wamefanya sisi tunachofanya katika ngazi ya halmashauri kuwa na eneo kubwa zaidi kuwa machache!! Na wakawa na mabunge sisi tunaita kikaa cha madiwani!

Unachokisifia kama utaratibu mzuri actually ni kupoka madaraka ya serikali za mitaa. Ushihidi ni mlichokisema sana 2016-2020 - “mnatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM”. Yaani chama kingine kitoe sera zake kwa eneo husika, washinde idadi kubwa, wapate meya au mkuu wa hiyo serikali ndogo lakini mwishoni waletewe mkurugenzi na viongozi wengine na Rais ili kusimamisha ilani walioshindia na kutekeleza ilani ya washindwa!!
 
Hilo halimaanishi kuwa utawala wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo yatake kujitenga. Ni uvivu kifikiri hivyo.
Yaani baada ya kukupa mifano yote hiyo bado unang'ang'ana tu ?!! 🤣🤣

Ok.....

Sababu zinazosababisha baadhi ya majimbo kutaka kujitenga zinashahabiana duniani kote....."mgawanyo wa resources" ukiwa unaongoza.......

✓Majimbo ambayo yana raslimali kubwa huona yanatumika kubeba majimbo mengine na kwa kuwa wanaona hawawahitaji wengine basi hutaka kujitenga(Tigray ,Katanga ).

Kuna la WINGI wa watu (population demographic) mathalani Jimbo la OROMIA na AMHARA nchini Ethiopia.......

Kwa hiyo ndani ya Sera za MAJIMBO inaweza kupita miaka mingi ya UTULIVU ila iko siku tu historia inaweza kubadililishwa kwa sababu hizo nilizoziorodhesha hapo juu......


SIEMPRE JMT
KATIBA ILIYOPO INATOSHA
 
Nchi ina wajinga wengi sana, mbaya zaidi wanashindana kutangaza ujinga wao mitandaoni.
 
Mkuu nakukumbusha tu kuwa TPLF kilianzishwa mwaka 1975......na sasa ni CHAMA CHA SIASA pia.....kimeshawahi kuiongoza ETHIOPIA chini ya mwamvuli wa vyama....

Mkuu yaani unafananisha Banyamulenge na TPLF?!! Duuh hauko serious 😳🤣🤣

Umemsahau waziri mkuu aliyetawala muda mrefu hayati Meles Zenawi ?!!!!!
 
Tatizo unaangalia mambo kijuujuu sana. Mfano mmoja, Kurdistan ya Iraq haikutaka kujitenga kwa sababu ni jimbo linalijitegemea bali ilipewa status ya jimbo linalojitegemea kwa sababu inataka kujitenga. Wewe unaliangalia suala lao kinyume.

Na hilo suala ulilolieleza huanza namna hii.

Nchi inakuwa ya kimkoa kama hii yetu lakini kunatokea upendeleo katika kugawana mali. Wanakusanya pesa nchi nzima na kisha viongozi wanaenda kujenga kwao au mikoa inayowapa kura. Wanakopa pesa na kujenga barabara na miundombinu mingine Dar, wakati wa kulipa wanauza kahawa za Mbinga na dhahabu ya Geita. Watu wanaanza kunung'unika na kuanza kutaka kijitenga. Serikali ili kuzuia kujitenga wanaanzisha mfumo wa majimbo. Hii inawapa watu haki kidogo kutokana na mali zao. Lakini wengine wanaweza kuona haitoshi. Wanaamua kuendeleza harakati za kujitenga.

Sasa kwa mtiririko huu utasema mfumo wa majimbo ndiyo umesababisha kujitenga au ulikuwa unazuia kujitenga?

Mfano rahisi ni Kenya hapo. Kulikuwa na harakati za mkoa wa Pwani kujitenga baada ya kuona wanatengwa. Katika kutatua mambo kama hayo serikali ikaja na devolution/ugatuzi ambayo ni kama tu majimbo(tofauti ndogo sana). Kelele za pwani kujitenga hazipo tena.

Mfumo wa majimbo hutumika kuzuia nchi isisambaratike na wala hausababishi nchi kusambaratika. Unaangalia hili suala kivivu na kinyumenyume.
 
Na watu wanatakiwa kufahamu kuwa Nyerere alikuwa ni muumini mkubwa wa mfumo wa majimbo. Alianzisha Tawala za mikoa na serikali za mitaa na kukazia kuwa hizo ni serikali kamili zenye mamlaka. Akaenda mbali na kusema. "Serikali kuu haiwezi kuziongezea wala kuzipunguzia mamlaka serikali hizo."
 
Nimekuwekea takwimu....

Kati ya nchi 48 za Asia ni 5 tu zenye Sera za MAJIMBO.....

Kwa maneno yako hizo nchi 43 zisizo na mfumo huo "uupendao" zinasambaratika ama zingeshasambaratika.......

Kati ya nchi huru 54 za Afrika ni nchi 5 tu zenye Sera za majimbo.....

Kwa maneno yako nchi 49 zisizo na mfumo wa majimbo zinasambaratika ama zingeshasambaratika......

Kati ya nchi 12 za Amerika ya kusini ni 4 tu zenye Sera ya majimbo(Brazil ,Venezuela,Mexico na Argentina)....kote huko Kuna vikundi vya silaha vinavyotaka kujitenga(Ven-Zulia) (Arg-Patagonia) Brazil- Sao Paulo....Mexico imebaki "ngada"🤣🤣🤣

Hiyo mifano ya ubora wa Sera ya majimbo mnaitoa ULAYA NA MAREKANI?!!!!!

Marekani na Ulaya hatufanani nao kwa mengi tu na sidhani ni rejea yenye mantiki....

Huko juu nimeandika kwa kirefu kumjibu compatriot wako......

✓Ethiopia hali ni tete....ni marudio tu......
✓DRC ndio kabisaaa.....nchi imejikita tu kule Kinshasa na majimbo ya karibu....huko Mashariki serikali ya shirikisho haina udhibiti makini.......Katanga ilitaka kujichomoa mapema kabisa......

✓Nigeria ni sugu.....majimbo ya kaskazini yanajulikana kwa kukosa utulivu.......
Kule BIAFRA toka enzi ni fukuto tu hadi leo hii....nia Yao iko palepale ya kuiondoka NIGERIA

Nimekupa mifano ya nchi 3 tu za barani Afrika zenye "nakama" ya majimbo halafu bado unashupaza shingo tu 🤣🤣

SIEMPRE JMT
 
Kwanza elewa kuwa si lazima mfumo wa mikoa ulete machafuko lakini ni mbovu sana

Unaangalia mambo kijuujuu tu. DRC haina serikali za majimbo. Siyo federation. Na ukiiangalia Nigeria utagundua kuwa majimbo ndiyo yameiunganisha. Wakati wanapata uhuru ilikuwa imegawanyika sana. Njia pekee ya kuifanya kuwa nchi moja ilikuwa ni federation. Hata Ethiopia, Imefika hapo sababu ya mfumo wa majimbo. Mfumo mtu yeyote angejaribu kutawala kila kitu kutoka serikali kuu angefeli.

Unafikiri kwanini China wameipa Xinjiang autonomy? Mfumo wa majimbo unatumika kuzuia kusambaratika na si kusababisha. Hata Uingereza wanafikiria kuwa federal sababu ya vuguvugu za wascott kujitenga.

Na kingine, hizo nchi nyingi ambazo hazina mfumo wa majimbo utakuta zimefanya devolution ya kutosha, kama iliyofanyika hapo Kenya. Nchi chache sana zunaendeshwa kwa mfumo wetu ambao maamuzi yanatoka serikali kuu.
 
nakubaliana na ww kuhusu matatizo ya ethiopia ni zaidi ya issue ya majimbo but sikubaliani kabisa na mtazamo wako kuhusu abby, shida ni wa tigray kwanza si mara ya kwanza kwa wa tigray kuanzisha vita kuja addis ababa walishafnya hivyo miaka ya mwanzon mwa tisini wakafumbiwa macho na wanajiita jumuiya ya kimataifa, na sasa tena wana wanapigana kuelekea addis ababa again jumuiya ya kimataifa inawapressure ethiopia tu wakati watigray wako busy kuelekea tena kuuchukua mji mkuu, kimsingi wa tigray watatulia tu as long wanadhibiti serikali but km serikali ipo chini ya makabila mengine wao kwao ni shida, na walipokua madarakan walitumia rasilimali za taifa kujenga vikosi vyao vya TPLF kufikia kuwa na nguvu kiasi kile, ukishakua na jamii ndani ya nchi inaojiona inastahili zaidi ya jamii zingine hakutakuwa na amani haijalishi ni mfumo gani wa kisiasa mnao
 
Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi duniani zilizowahi kuwa na civil wars ni zenye mfumo wa majimbo.
kati ya hizo ulizozitaja, nane zishawahi kuwa na civil wars.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi duniani zilizowahi kuwa na civil wars ni zenye mfumo wa majimbo.
kati ya hizo ulizozitaja, nane zishawahi kuwa na civil wars.
Nchi zinazoongozwa kwa mfumo wa majimbo.

 
Ungejifunza kwanza kwa nini wakoloni walishi dwa kuikalia Ethiopia
 
Kwa nini Jiwe alitawala kwa mkono wa chuma?
 
Hizo habari za Chadema achana nazo. Miaka karibu 60 ya uhuru ccm imefanya nini zaidi ya kuwamasikinisha wananchi. Si ajabu kila siku mnawaita wananchi wanyonge, huo unyonge kawapa nani!? Deal zote za upigaji zinafanywa na wakuu wa chama na mashoga zao wahindi na waarabu.
Endelea kufurahia maendeleo yaliyofanywa na wenye uchungu na nchi zao huko Denmark ulipo.
 
Huko Zanzibar ambako siku zote mnapindua matokeo nako wanataka serikali ya majimbo!?
 
Asante kwa kuwasilisha maoni ambayo yanafanana moja kwa moja na maoni yangu. Hadi nimeangalia id isije ikawa nimeandika mimi, nikajisahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…