Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umeandika sahihi, lakini umejikita kwenye sehemu moja ya aina ya mfumo wa uongozi wa nchi. Lakini changamoto za Ethiopia ni zaidi ya hizo. Kinacholeta ukosefu wa amani ni kwa sababu ya serikali ya Abby kuwa wabinafsi na madikteta. Unajua kwa Nini kabla ya Abby migogoro hii haikuwa na Nguvu au haikuwepo? Ni kwa sababu wenzao Watigray walibalance uongozi bila ubaguzii.
Kwa sisi waafrika aisee hili suala la majimbo ni gumu sana unajua hatuna nationalism, mfano, marekani inaongozwa kwa mfumo wa majimbo Ila wana nationalism (utaifa, uzalendo) yani pamoja mtu anatoka let's say Colorado ,Ila unakutaa hawako tayari kujiondoa kwenye USA.Habari wanajamvi,
Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.
basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.
Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura
Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa
Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya
Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.
Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Kwanini mnapenda kutolea mfano nchi zilizoshindwa!! Mbona hauongelei success ya mfumo wa decentralization say Afrika kusini au Kenya?Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake
😍Nasirimgambo uko sahihi kabisa. Katiba yetu ni bora na madhubuti kuliko barani Afrika. Ushahidi mwingine ni kile kilichotupata mwezi March cha kupotelewa ghafla kwa rais aliyekuwa madarakani. Jambo kama hili lingalitokea kwa majirani zetu ambao CDM huwa inawasifia kuwa na katiba mpya bora, sijui hali ya huko ingalikuwaje. Kwani huko rais wa nchi na makamu wake hawako chungu kimoja na hawatoki chama kimoja cha siasa.
Mpka huwa najiulza au yale mazindiko ya Lindi hayakutuacha salamaumeandika sahihi, lakini umejikita kwenye sehemu moja ya aina ya mfumo wa uongozi wa nchi. Lakini changamoto za Ethiopia ni zaidi ya hizo. Kinacholeta ukosefu wa amani ni kwa sababu ya serikali ya Abby kuwa wabinafsi na madikteta. Unajua kwa Nini kabla ya Abby migogoro hii haikuwa na Nguvu au haikuwepo? Ni kwa sababu wenzao Watigray walibalance uongozi bila ubaguzii.
Kitu kingine ni aina ya Wananchi. Watanzania wengi wao ni kama mazombie. Hata uwafanye Nini hawezi kuchukua hatua, Ndio maana unaona Kiongozi anafanya anavyotaka na haguswi, Yaani hawajibishwi na raia. Ndio maana kwenye tozo wakasema Watanzania watazoea tu. Na kweli mmezoea.
Sasaivi bei ya mbolea juu, hakuna anayeona, watu wanalia kimyakimya, Tanzania Ina mambo mengi ambayo yangeweza kuwafanya waende msituni au waandame ila kwa sababu ya uzombi Ndio maana kila ripoti ikija Tanzania nchi isiyo na furaha sawa na somalia, Libya, Burundi na Kongo kwenye vita.
In short kila mtanzania anaandamana na kupigana na serikali hii motoni mwake. Ndio maana watu wanazidi kuchakaa. Maandamano ya moyoni ni mabaya kuliko maandamano ya dhahiri. Hope nimeeleweka.
Mbona unapotosha;Nasirimgambo uko sahihi kabisa. Katiba yetu ni bora na madhubuti kuliko barani Afrika. Ushahidi mwingine ni kile kilichotupata mwezi March cha kupotelewa ghafla kwa rais aliyekuwa madarakani. Jambo kama hili lingalitokea kwa majirani zetu ambao CDM huwa inawasifia kuwa na katiba mpya bora, sijui hali ya huko ingalikuwaje. Kwani huko rais wa nchi na makamu wake hawako chungu kimoja na hawatoki chama kimoja cha siasa.
Vurugu za Kenya mbona zimeanza hata kabla ya majimbo? In fact sahivi zimepungua sababu kila "kabila" lina serikali yake so linajipangia vipaumbele kuliko zamani ambapo wanufaika walikua wakikuyu/kalenjin pekee.Mabeberu wanataka kurudi na kutawala upya kupitia migogoro yetu kama hiyo ya Ethiopia tayari Marekani wanampango wa kupeleka ASKARI Ethiopia. Next ni Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka kesho tutegemee the same problem. Hapa Tanzania tayari sera ya majimbo CHADEMA ndio wanaotaka
Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣Mbona unapotosha;
Ruto na JK ni chama kimoja kinaitwa jubilee, in fact hiko chama kipya cha UDA ni moja ya vyama vilivyopo kwenye muungano wa Jubilee.
Then Rais angefariki wanarudi kwenye uchaguzi simple and clear sio sisi akifariki Rais basi makamu wake licha ya track record wala mandate ya watu anapewa tu Urais!!
Yes katiba mpya ya kenya ni bora kuliko yetu hasa kwenye kulinda uhuru wa bunge na mahakama ndio maana kuna uwajibikaji kuliko hapa kwetu.
Mfumo wa majimbo kwa waafrica bado Sana...changamoto zake bado waafrika hawana uwezo wa kutatuaHabari wanajamvi,
Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.
basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.
Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura
Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa
Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya
Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.
Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Kenya ilianza na ukabila na ndio unaowatafuna mpaka muda huu....majimbo yamekuja kuongeza balaa zaidi.....Vurugu za Kenya mbona zimeanza hata kabla ya majimbo? In fact sahivi zimepungua sababu kila "kabila" lina serikali yake so linajipangia vipaumbele kuliko zamani ambapo wanufaika walikua wakikuyu/kalenjin pekee.
Tatizo waTZ tunapenda kufungamanisha vitu, mfano tatizo la Ethiopia ni kukosekana inclusive economy ila tunakimbilia kulaumu mfumo wa majimbo!!
Mfumo wa majimbo CHADEMA ni sawa tu na halmashauri zilizopo kuongezewa wigo wa mapato na maamuzi tofauti ni kwamba badala ya halmashauri ya Kalambo kusubiri maamuzi ya Dodoma, wao wanaregulate na serikali ya jimbo la Magharibi n.k. ila masuala kama ulinzi yanabaki kwa serikali kuu.
Tusipotoshe
Kwani vifo vitatu ni expected occurence? Unasahau 2016 tulifanya chaguzi ya marudio zenji? Kila kitu ni mipango na chaguzi zinaachana siku 90 tokea makamu ashike nadhani so within that time frame serikali inakua imejipanga.Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣
Na kwa kuwa vifo si expected occurrence ndio maana framers wa katiba yetu waliliona hilo kuwaepushia wananchi gharama za chaguzi za mara kwa mara....au bado unataka tuendelee kuchangiwa fedha za uchaguzi na wahisani wetu?!!!Kwani vifo vitatu ni expected occurence? Unasahau 2016 tulifanya chaguzi ya marudio zenji? Kila kitu ni mipango na chaguzi zinaachana siku 90 tokea makamu ashike nadhani so within that time frame serikali inakua imejipanga.
Tuige mazuri na yale mabaya tuyaache kuliko kupinga mfumo mzima kisa tu "Ethiopia mfumo umefeli"
Majimbo yamepunguza ukabila in fact ili ushinde Urais ni lazima upate kura kwenye kaunti sio chini ya 27 so imelazimisha vyama kuwa vya kitaifa na sio vya kikanda tena.Kenya ilianza na ukabila na ndio unaowatafuna mpaka muda huu....majimbo yamekuja kuongeza balaa zaidi.....
Sera yenu ya Chadema ndiyo hayo majimbo yenyewe kwa kutaka halmashauri ya "Kalambo" ijikusanyie Kodi na kujipangia matumizi yake......
Nchi kama Tanzania inajulikana baadhi ya Kanda zina raslimali nyingi zaidi ya nyingine.....itafikia kipindi hizo Kanda zitauona mzigo kuchangia pato kubwa ndani ya serikali kuu na kutokea waasi na kuwa mwanzo wa kutaka UHURU WAO.........
Si siri baadhi ya maeneo nchini hapa yalitaka KUJITENGA toka enzi za uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere......
sio expected occurence lakini ni risk kubwa makamu kupewa Urais bila mandate ya watu, na ndio maana kuna watu serikalini wanampinga Mama wazi wazi sababu wanajua hana mandate yao. Na kaingia kwa sheer luck.Na kwa kuwa vifo si expected occurrence ndio maana framers wa katiba yetu waliliona hilo kuwaepushia wananchi gharama za chaguzi za mara kwa mara....au bado unataka tuendelee kuchangiwa fedha za uchaguzi na wahisani wetu?!!!
Sasa hiyo sio amani, huo ni ujuha. Watu wanalalamika mioyoni. Sijajua wewe upo class gani, lakini sisi tunaotoka poor class tunajua namna nchi ilikotoka na inavyozama baharini. Waulize wafanyabiashara na wakulima namna mambo yalivyo magumu. Anyway labda kama tunaishi ilimradi tuneamka salama basi sawa. Lakini tukitaka maendeleo ya kweli, lazima tuwe na watu wanaohoji na sio kukaa. Na maumivu moyoni.Kama "uzombi" wa watanzania ndiyo unaofanya tuwe na amani hii tuliyonayo na stability hii tuliyonayo, basi si uzombi bali ni akili.
Kwani wewe unadhani hili usionekane zombi basi lazima ulalamikelalamike? Kitu gani ambacho serikali hii imefanya ambacho hakikupasi kama wewe mwanachi ukifanye? Kama hutaki kutozwa tozo basi usitoe tozo na hakuna aliyekulazimisha utoe tozo. Watanzania tunaishi kwa kanuni ya "contentment", tunahitaji amani, tunahitaji stability, vinginevyo vitafuata kwa juhudi binafsi na maarifa. Basi.
Kwako wewe sababu siyo majimbo. Ila, kwa wengine sababu ni majimbo.Hakuna
Civil wars hazijengwi na MAJIMBO
Vita ya Burundi sababu sio majimbo
Vita DRC sababu sio majimbo
Vita Angola sababu sio majimbo
etc
Nipe nchi sababu ni "majimbo"!
Na nchi zenye vita unazodai zipo ngapi?
Wapumbavu nyie...acheni fear mongering!
It's not nonsense, you are just too delusional.Tatizo sio geographical locations,tatizo ni ukabila wa makabila hasa kwenye economic advantages and disadvantages
Wala sio majimbo ambayo ni geographical locations ...
Stop this nonsense
Huo ni ugomvi makundi yenye shida na economic preveledges against each other na sio eti geografia ya majimbo
Shida hapa ni RESOURCES na wala sio jiografia..acha upumbavu!
Na hizi resources ugomvi unatokea pale nyie wageni mnapokuja kwenye migodi ya watu halafu wenyeji mnawanyima nao wasile hilo ndio tatizo
Mnawanyima wenyeji nao wasile..hilo ndio tatizo....