Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Nani kasema tatizo la Mynamar ni majimbo?Burma au Myanmar tatizo ni Military Junta kupindua serikali za kiraia na sio suala la majimbo.
Wewe ndie unajadili kinyume nyume.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani kasema tatizo la Mynamar ni majimbo?Burma au Myanmar tatizo ni Military Junta kupindua serikali za kiraia na sio suala la majimbo.
Wewe ndie unajadili kinyume nyume.
Hatari sana kamarada.....Mabeberu wanataka kurudi na kutawala upya kupitia migogoro yetu kama hiyo ya Ethiopia tayari Marekani wanampango wa kupeleka ASKARI Ethiopia. Next ni Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka kesho tutegemee the same problem. Hapa Tanzania tayari sera ya majimbo CHADEMA ndio wanaotaka
Hilo halimaanishi kuwa utawala wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo yatake kujitenga. Ni uvivu kifikiri hivyo.Nchi 54 za Afrika ni nchi 5 tu zenye mfumo huo.......
Nchi 48 za bara la Asia ni nchi 5 tu zenye huo mfumo wa kimajimbo......
India na ndugu yake Pakistan.....
Nepal na Burma pamoja na Iraq.....
✓India mpaka Leo uchumi wake haujawa sawa kimajimbo na Kuna matabaka sugu ya kutosha tu......
✓Iraq toka enzi ya Saddam kumekuwa na msuguano na WAKURDI wanaotaka kujitenga.....
Kule Amerika ya kusini ,Kati ya 12 ni 4 tu ( Venezuela ,Mexico ,Argentina na Brazil)......
✓Jimbo la ZULIA nchini Venezuela wanapambana kujitenga(vikundi viko active)
✓Argentina kule Patagonia wanataka kujitenga (vikundi vya silaha)
✓Brazil Jimboni Sao Paulo(vikundi vya silaha)
✓Mexico imefurutu ADA ya madawa ya kulevya.....
SIEMPRE JMT
Yaani baada ya kukupa mifano yote hiyo bado unang'ang'ana tu ?!! 🤣🤣Hilo halimaanishi kuwa utawala wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo yatake kujitenga. Ni uvivu kifikiri hivyo.
Nchi ina wajinga wengi sana, mbaya zaidi wanashindana kutangaza ujinga wao mitandaoni.kwa takwimu zipi hasa ukiangalia dunia nzima?
dunia nzima yote ipo kwenye majimbo,then inatokea nchi moja kati ya 400 inapata tatizo unasema 1/400 ni best probability?
Hivi ulisoma Statistics and Probability shule ya chooni?
Na mgogoro wa Tigray sababu yake ni ingine kabisa compared na unachoongea hapa
Mkuu nakukumbusha tu kuwa TPLF kilianzishwa mwaka 1975......na sasa ni CHAMA CHA SIASA pia.....kimeshawahi kuiongoza ETHIOPIA chini ya mwamvuli wa vyama....Mleta mada hujui kwa usahihi unachosema na sitakosea kukuita muongo!! Ingefaa ukaa unachokisema:
a) jambo moja zuri au baya haliwezi kutumika
Kwa ujumla. Umeeleza ubaya wa serikali za majimbo kwa Ethiopia. Ungeenda mbali zaidi na kutuambia ubaya wa jambo hilo kwa nchi kama South Afrika, Marekani, Canada, UK na hata Kenya. Kwa hutujua jambo hili vizuri utabisha kuwa hata Kenya haina mfumo huu, ungependa niseme kaunti badala ja jimbo.
b) si kweli TPLF ni jeshi la jimbo. Ni kikundi cha waasi kikichoanzishwa na watu wa jimbo la Tigray. Sawa na Banyamulenge mashariki mwa DRC. Jeshi la nchi ya Ethiopia lipo na limeshindwa vita eneo la Tigray na kuwafanya waasi washikilie eno.
Ambacho unataka kusema lakini kwa kuficha ni ukandamizaji wa kidemokrasia unaoendelea hapa Tanzania kwa kijisababu cha umoja. Sisi tuna halmashauri zinazoongozwa na chama kilichoshinda viti vingi vya udiwani. Na kiongozi kati halmashauri ni meya. Tungetaka kujilinganisha na wengine, huyu ndio angekuwa juu ya wateule wa Rais kama Mkuu wa wilaya, RAS na mkurugenzi. Wenzetu wamefanya sisi tunachofanya katika ngazi ya halmashauri kuwa na eneo kubwa zaidi kuwa machache!! Na wakawa na mabunge sisi tunaita kikaa cha madiwani!
Unachokisifia kama utaratibu mzuri actually ni kupoka madaraka ya serikali za mitaa. Ushihidi ni mlichokisema sana 2016-2020 - “mnatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM”. Yaani chama kingine kitoe sera zake kwa eneo husika, washinde idadi kubwa, wapate meya au mkuu wa hiyo serikali ndogo lakini mwishoni waletewe mkurugenzi na viongozi wengine na Rais ili kusimamisha ilani walioshindia na kutekeleza ilani ya washindwa!!
Tatizo unaangalia mambo kijuujuu sana. Mfano mmoja, Kurdistan ya Iraq haikutaka kujitenga kwa sababu ni jimbo linalijitegemea bali ilipewa status ya jimbo linalojitegemea kwa sababu inataka kujitenga. Wewe unaliangalia suala lao kinyume.Yaani baada ya kukupa mifano yote hiyo bado unang'ang'ana tu ?!! 🤣🤣
Ok.....
Sababu zinazosababisha baadhi ya majimbo kutaka kujitenga zinashahabiana duniani kote....."mgawanyo wa resources" ukiwa unaongoza.......
✓Majimbo ambayo yana raslimali kubwa huona yanatumika kubeba majimbo mengine na kwa kuwa wanaona hawawahitaji wengine basi hutaka kujitenga(Tigray ,Katanga ).
Kuna la WINGI wa watu (population demographic) mathalani Jimbo la OROMIA na AMHARA nchini Ethiopia.......
Kwa hiyo ndani ya Sera za MAJIMBO inaweza kupita miaka mingi ya UTULIVU ila iko siku tu historia inaweza kubadililishwa kwa sababu hizo nilizoziorodhesha hapo juu......
SIEMPRE JMT
KATIBA ILIYOPO INATOSHA
Nimekuwekea takwimu....Tatizo unaangalia mambo kijuujuu sana. Mfano mmoja, Kurdistan ya Iraq haikutaka kujitenga kwa sababu ni jimbo linalijitegemea bali ilipewa status ya jimbo linalojitegemea kwa sababu inataka kujitenga. Wewe unaliangalia suala lao kinyume.
Na hilo suala ulilolieleza huanza namna hii.
Nchi inakuwa ya kimkoa kama hii yetu lakini kunatokea upendeleo katika kugawana mali. Wanakusanya pesa nchi nzima na kisha viongozi wanaenda kujenga kwao au mikoa inayowapa kura. Wanakopa pesa na kujenga barabara na miundombinu mingine Dar, wakati wa kulipa wanauza kahawa za Mbinga na dhahabu ya Geita. Watu wanaanza kunung'unika na kuanza kutaka kijitenga. Serikali ili kuzuia kujitenga wanaanzisha mfumo wa majimbo. Hii inawapa watu haki kidogo kutokana na mali zao. Lakini wengine wanaweza kuona haitoshi. Wanaamua kuendeleza harakati za kujitenga.
Sasa kwa mtiririko huu utasema mfumo wa majimbo ndiyo umesababisha kujitenga au ulikuwa unazuia kujitenga?
Mfano rahisi ni Kenya hapo. Kulikuwa na harakati za mkoa wa Pwani kujitenga baada ya kuona wanatengwa. Katika kutatua mambo kama hayo serikali ikaja na devolution/ugatuzi ambayo ni kama tu majimbo(tofauti ndogo sana). Kelele za pwani kujitenga hazipo tena.
Mfumo wa majimbo hutumika kuzuia nchi isisambaratike na wala hausababishi nchi kusambaratika. Unaangalia hili suala kivivu na kinyumenyume.
Kwanza elewa kuwa si lazima mfumo wa mikoa ulete machafuko lakini ni mbovu sanaNimekuwekea takwimu....
Kati ya nchi 48 za Asia ni 5 tu zenye Sera za MAJIMBO.....
Kwa maneno yako hizo nchi 43 zisizo na mfumo huo "uupendao" zinasambaratika ama zingeshasambaratika.......
Kati ya nchi huru 54 za Afrika ni nchi 5 tu zenye Sera za majimbo.....
Kwa maneno yako nchi 49 zisizo na mfumo wa majimbo zinasambaratika ama zingeshasambaratika......
Kati ya nchi 12 za Amerika ya kusini ni 4 tu zenye Sera ya majimbo(Brazil ,Venezuela,Mexico na Argentina)....kote huko Kuna vikundi vya silaha vinavyotengeneza kujitenga(Ven-Zulia) (Arg-Patagonia) Brazil- Sao Paulo....Mexico imebaki "ngada"🤣🤣🤣
Hiyo mifano ya ubora wa Sera ya majimbo mnaitoa ULAYA NA MAREKANI?!!!!!
Marekani na Ulaya hatufanani nao kwa mengi tu na sidhani ni rejea yenye mantiki....
Huko juu nimeandika kwa kirefu kumjibu compatriot wako......
✓Ethiopia hali ni tete....ni marudio tu......
✓DRC ndio kabisaaa.....nchi imejikita tu kule Kinshasa na majimbo ya karibu....huko Mashariki serikali ya shirikisho haina udhibiti makini.......Katanga ilitaka kujichomoa mapema kabisa......
✓Nigeria ni sugu.....majimbo ya kaskazini yanajulikana kwa kukosa utulivu.......
Kule BIAFRA toka enzi ni fukuto tu hadi leo hii....nia Yao iko palepale ya kuiondoka NIGERIA
Nimekupa mifano ya nchi 3 tu za barani Afrika zenye "nakama" ya majimbo halafu bado unashupaza shingo tu 🤣🤣
SIEMPRE JMT
nakubaliana na ww kuhusu matatizo ya ethiopia ni zaidi ya issue ya majimbo but sikubaliani kabisa na mtazamo wako kuhusu abby, shida ni wa tigray kwanza si mara ya kwanza kwa wa tigray kuanzisha vita kuja addis ababa walishafnya hivyo miaka ya mwanzon mwa tisini wakafumbiwa macho na wanajiita jumuiya ya kimataifa, na sasa tena wana wanapigana kuelekea addis ababa again jumuiya ya kimataifa inawapressure ethiopia tu wakati watigray wako busy kuelekea tena kuuchukua mji mkuu, kimsingi wa tigray watatulia tu as long wanadhibiti serikali but km serikali ipo chini ya makabila mengine wao kwao ni shida, na walipokua madarakan walitumia rasilimali za taifa kujenga vikosi vyao vya TPLF kufikia kuwa na nguvu kiasi kile, ukishakua na jamii ndani ya nchi inaojiona inastahili zaidi ya jamii zingine hakutakuwa na amani haijalishi ni mfumo gani wa kisiasa mnaoumeandika sahihi, lakini umejikita kwenye sehemu moja ya aina ya mfumo wa uongozi wa nchi. Lakini changamoto za Ethiopia ni zaidi ya hizo. Kinacholeta ukosefu wa amani ni kwa sababu ya serikali ya Abby kuwa wabinafsi na madikteta. Unajua kwa Nini kabla ya Abby migogoro hii haikuwa na Nguvu au haikuwepo? Ni kwa sababu wenzao Watigray walibalance uongozi bila ubaguzii.
Kitu kingine ni aina ya Wananchi. Watanzania wengi wao ni kama mazombie. Hata uwafanye Nini hawezi kuchukua hatua, Ndio maana unaona Kiongozi anafanya anavyotaka na haguswi, Yaani hawajibishwi na raia. Ndio maana kwenye tozo wakasema Watanzania watazoea tu. Na kweli mmezoea.
Sasaivi bei ya mbolea juu, hakuna anayeona, watu wanalia kimyakimya, Tanzania Ina mambo mengi ambayo yangeweza kuwafanya waende msituni au waandame ila kwa sababu ya uzombi Ndio maana kila ripoti ikija Tanzania nchi isiyo na furaha sawa na somalia, Libya, Burundi na Kongo kwenye vita.
In short kila mtanzania anaandamana na kupigana na serikali hii motoni mwake. Ndio maana watu wanazidi kuchakaa. Maandamano ya moyoni ni mabaya kuliko maandamano ya dhahiri. Hope nimeeleweka.
Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi duniani zilizowahi kuwa na civil wars ni zenye mfumo wa majimbo.Tuanze na hizo nchi 5 za Africa unazodai eti ndio zina majimbo pekee yake na nchi 49 zilizosalia hazina majimbo:
1.Burundi : 18provinces
2.DRC: 26 provinces
3.Equatorial Guinea : 8provinces
4.Ethiopia : 12 provinces
5.Gabon: 9 provinces
6.Ghana : 16 provinces
7.Kenya : 47 counties (provinces)
8.Liberia : 15 counties
9.Nigeria : 36 states
10.Sierra Leone : 4 provinces
11.South Africa : 9 provinces
12.South Sudan : 10 States
13.Zambia : 10 provinces
14. etc
15.etc
Sasa wewe hiyo namba ya yako ya 5 countries in Africa umeitolea wapi?
Muongo mkubwa!
Nchi zinazoongozwa kwa mfumo wa majimbo.Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi duniani zilizowahi kuwa na civil wars ni zenye mfumo wa majimbo.
kati ya hizo ulizozitaja, nane zishawahi kuwa na civil wars.
Habari wanajamvi,
Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.
basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.
Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura
Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa
Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya
Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.
Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.
Duuuh [emoji15][emoji15][emoji15]
Hayati Meles Zenawi alitokea Tigray......aliitawala hiyo nchi kwa MKONO WA CHUMA......
Unajua ni kwanini alifanya hayo ?!!!
Kwa sababu Ethiopia ni nchi ya kikabila na matabaka....matabaka makubwa ni OROMO na AMHARA ambao huwa wanadai "share" kubwa kwa sababu ya WINGI wao .....Meles Zenawi aliiongoza nchi hiyo kwa MKONO WA CHUMA Kama afanyavyo ABIY AHMED.....na la kushangaza ABIY AHMED ni mchanganyiko wa kutoka OROMO na AMHARA....ndugu zake hao wanamuona kama mtu msaliti aliyewageuka....wao walitegemea ANGEWABEBA KIKANDA......
Ikumbukwe alipoondoka Meles Zenawi Watigrinya walikuwa ni KABILA hodhi ya kila eneo la kimkakati nchini Ethiopia ijapokuwa ni kabila DOGO.........
Leo wameungana(ajabu kabisa) wanamshambulia ndugu yao Abiy Ahmed wakiwa bega kwa bega na kundi lililofaidika kipindi cha hayati Zenawi(TPLF)....
Hapa ndipo tunapopinga Sera za MAJIMBO kwani hutokea siku isiyo na jina WANASIASA kwa tamaa na ULAFI WAO huiingiza nchi matatizoni....wanaoumia ni wazee ,wanawake na watoto!!!!
SIEMPRE JMT
Hizo habari za Chadema achana nazo. Miaka karibu 60 ya uhuru ccm imefanya nini zaidi ya kuwamasikinisha wananchi. Si ajabu kila siku mnawaita wananchi wanyonge, huo unyonge kawapa nani!? Deal zote za upigaji zinafanywa na wakuu wa chama na mashoga zao wahindi na waarabu.Wako ndugu zetu kutoka CHADEMA
Huiona mbeleko pale wanapotanguliza sera za MAJIMBO na kutoa mifano ya nchi nyingi zilizopiga hatua na kutokuwa na migogoro
Ndugu hao hupendelea kutoa mifano ya nchi za ULAYA NA MAGHARIBI kana kwamba Waafrika/Afrika tunafanana nao hao watu
Wengine hutoa mfano wa Afrika ya Kusini(SA) wanasahau kuwa mpaka leo Afrika ya Kusini bado uchumi wao UKO MIKONONI mwa wachache weupe na ndio maana akina Tate Julius Malema na Floyd Shivambu bado wanaona hawajakomboka KIUCHUMI kufikia kuja na chama chao chenye sera za KIKOMUNISTI (EFF) nilidhani wangeiga na hili kwa CHADEMA kuwa na Sera za kikomunisti 🤣🤣🤣...kinyume chake wao CDM wanavaa tu MAKOMBATI NA BERETI(nyekundu) kinyume kabisa na msimamo wao(siasa za Kati)🤣🤣
Chadema wasichokijua ni kuwa nchi za ULAYA karibuni zote zinaendeshwa chini ya UFALME tena ufalme wenye "nasabu-uhusiano" mmoja, japo chini yake kuna serikali ambazo tunaambiwa zina maamuzi yote kuzidi hizo falme(changa la macho hili) 🤣🤣🤣
Mathalani tawala ya kifalme ya ulaya iitwayo Saxe-Coburg-Gotha ilianzia UJERUMANI...ndio haohao watawala wa UBELGIJI(alipokimbilia ndugu wakili msomi Tundu Lissu) ndio haohao watawala wa Uingereza n.
Hakika kinachoendelea Ethiopia kinaweza kuikuta nchi yoyote ya Afrika yenye tawala za kimajimbo....huko Kongo ilipata kutokea Katanga kutaka kujitenga na isisahaulike kuwa leo KONGO inashindwa kutawalika/kuletwa AMANI kwa sababu hizohizo, baadhi ya majimbo YAMETELEKEZWA kufikia baadhi ya MAADUI WA NJE KUYAFANYA MAKAZI YAO.
Kwa hili la MIKOA tuendelee tu KUMUIMBA KWA SIFA lukuki na kummwagia DUA nyingi hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere ,aaaamin aaaamin 🙏
Hakika bila ya hili pengine tungekuwa tumeshayashuhudia ya ETHIOPIA ama yangekuwa yako njiani karibuni kutujia.........
#SIEMPRE JMT
#NCHI KWANZA
#TANZANIA NCHI YA MFANO AFRIKA💪
#TUILINDE AMANI YETU KWA NGUVU ZOTE
#KAZI IENDELEE
Huko Zanzibar ambako siku zote mnapindua matokeo nako wanataka serikali ya majimbo!?Mabeberu wanataka kurudi na kutawala upya kupitia migogoro yetu kama hiyo ya Ethiopia tayari Marekani wanampango wa kupeleka ASKARI Ethiopia. Next ni Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka kesho tutegemee the same problem. Hapa Tanzania tayari sera ya majimbo CHADEMA ndio wanaotaka
Asante kwa kuwasilisha maoni ambayo yanafanana moja kwa moja na maoni yangu. Hadi nimeangalia id isije ikawa nimeandika mimi, nikajisahau.Habari wanajamvi,
Kama ilivyo kawaida, kufanya tafakuri ya mambo yale mtu anayoyasikia maredioni na magazetini kuhusu yanayoendelea kwenye siasa za nchi mbalimbali.
basi nami nimejikuta nikiyatafakari sana yale yanayoendelea huko Ethiopia na vita vyao vya serikali ya kitaifa na wanamgambo wa jimbo lao la tigrinya, ambapo sasa vita hivyo vimeonekana kuvuta na makundi mengine ya makabila toka majimbo tofauti na tigrinya, tena mbaya zaidi makundi hayo yameanza na kutaka kudai uhuru.
Sasa, nikakumbuka mfumo wao wa uongozi wa Ethiopia wa kutumia majimbo, na kukumbuka jinsi baadhi ya watanzania huwa wanausema mfumo wetu wa mikoa ambao mkuu wa mkoa anateuliwa na rais hivyo kufanya serikali kuu kuwa na mkono wa moja kwa moja kwenye kuongoza mkoa, ambapo ni tofauti na mfumo wa majimbo ambapo kiongozi wa mkoa anapigiwa kura
Ubaya wa majimbo ni kuwa viongozi hao wa majimbo wana kuwa na mamlaka makubwa hata yanawajaa vichwani mara nyingine na kuwa fanya kutaka kuwa juu ya serikali ya kitaifa
Mfano serikali ya jimbo la tigrinya ambalo viongozi wake ndio vinara wa kisapoti waasi wapiganao dhidi ya serikali kuu. Mbaya zaidi mfumo huo wa majimbo unatoa mamlaka ya majimbo kuunda majeshi yao, ndio yanaibuka hayo ya makundi ya kiti gray, ambayo kiukweli ni jeshi la ndani la jimbo la Tigrinya
Kila nikiangalia utulivu wa nchi yetu na jinsi ambavyo serikali ni madhubuti, hivi, hata siuoni mwanya wa mkoa fulani kutuletea vurugu za kujitenga ama kuanzisha mapigano ndivyo ninazidi kuu appreciate mfumo wetu wa mikoa tulio nao
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake.
Viongozi waasisi wa taifa letu walikuwa na ujiniasi wa kipekee kabisa maana taifa hili walilolisuka baada ya kulipokea toka kwa wakoloni wamelisuka vizuri sana, ulimbukeni wa kukaa na kuona mifumo ya siasa ya wezetu ni bora zaidi ya kwetu tukiuendekeza utafanya siku moja tufumuefumue taifa hili lililosukwa vyema.