Mgogoro wa Ethiopia unadhihirisha umadhubuti wa mfumo wetu wa mikoa dhidi ya ule mfumo wa majimbo

Serikali za majimbo ni janja ya Marekani katika kujaribu kutumia kanuni ya divide and rule.
 

Mbona mabeberu yalimpa Abiy tuzo ya Nobel ya amani kwa demokrasia na maridhiano na uongozi uliotukuka? Tukuamini wewe ama mabeberu?
Huna hoja. Kubali serikali za majimbo kwa afrika ni shida. Nigeria ilileta shida na sasa Ethiopia
 
Kwa sisi waafrika aisee hili suala la majimbo ni gumu sana unajua hatuna nationalism, mfano, marekani inaongozwa kwa mfumo wa majimbo Ila wana nationalism (utaifa, uzalendo) yani pamoja mtu anatoka let's say Colorado ,Ila unakutaa hawako tayari kujiondoa kwenye USA.

Kwao kuwa raia wa USA ni jambo kubwa kushinda utambulisho wa majimbo wanakotoka. Mwafrika anawaza ukabila tu, then sijui huo ukabila unamsaidia nini.

Ndio maana Nyerere, Nkrumah na wenzao walishindwa kuanzisha United States of Africa sababu ni hizohizo tu. But imagine leo Afrika nzima ingekuwa taifa moja ingekuwa hakuna Mchina wa mzungu anayetugusa kwa utajiri na nguvu ambayo tungekuwa nayo kushinda hata America sema sasa iafrika ni shida.
 
Nasirimgambo uko sahihi kabisa. Katiba yetu ni bora na madhubuti kuliko barani Afrika. Ushahidi mwingine ni kile kilichotupata mwezi March cha kupotelewa ghafla kwa rais aliyekuwa madarakani. Jambo kama hili lingalitokea kwa majirani zetu ambao CDM huwa inawasifia kuwa na katiba mpya bora, sijui hali ya huko ingalikuwaje. Kwani huko rais wa nchi na makamu wake hawako chungu kimoja na hawatoki chama kimoja cha siasa. Katiba yetu ilituvusha salama salimini.

Katiba yetu kwa miaka yote imekuwa ikituvusha salama salimini kwenye chaguzi kuu zote. Imekuwa ikifanyiwa updates (marekebisho) ili kwenda na wakati kama ambavyo katiba za nchi zilizoendelea zimekuwa zikifanyika hususani ya USA ni ya mwaka 1780 yenye updates lukuki. UK hawana katiba, wao wanaongozwa na sheria tu.
 
Watanzania badala ya kutumia muda mwingi kuponda mifumo yetu ya kisiasa nashauri tuanze kuisifia, maana ni mifumo inayotuletea amani na umadhubuti wa hali ya juu wa taifa na serikali kuu yake
Kwanini mnapenda kutolea mfano nchi zilizoshindwa!! Mbona hauongelei success ya mfumo wa decentralization say Afrika kusini au Kenya?

Huko Ethiopia huwezi ukaacha tu serikali kuu itawale maeneo yote automatically kabila kubwa lingeshinda kila uchaguzi na lingebagua wengine. Kuweka majimbo kunawapa some freedom ya kujitawala hivyo inapunguza tension kuliko ukose kila kitu mpka chaguzi unofuata.
 
😍
 
Mpka huwa najiulza au yale mazindiko ya Lindi hayakutuacha salama
 
Mbona unapotosha;
Ruto na JK ni chama kimoja kinaitwa jubilee, in fact hiko chama kipya cha UDA ni moja ya vyama vilivyopo kwenye muungano wa Jubilee.

Then Rais angefariki wanarudi kwenye uchaguzi simple and clear sio sisi akifariki Rais basi makamu wake licha ya track record wala mandate ya watu anapewa tu Urais!!

Yes katiba mpya ya kenya ni bora kuliko yetu hasa kwenye kulinda uhuru wa bunge na mahakama ndio maana kuna uwajibikaji kuliko hapa kwetu.
 
Vurugu za Kenya mbona zimeanza hata kabla ya majimbo? In fact sahivi zimepungua sababu kila "kabila" lina serikali yake so linajipangia vipaumbele kuliko zamani ambapo wanufaika walikua wakikuyu/kalenjin pekee.

Tatizo waTZ tunapenda kufungamanisha vitu, mfano tatizo la Ethiopia ni kukosekana inclusive economy ila tunakimbilia kulaumu mfumo wa majimbo!!

Mfumo wa majimbo CHADEMA ni sawa tu na halmashauri zilizopo kuongezewa wigo wa mapato na maamuzi tofauti ni kwamba badala ya halmashauri ya Kalambo kusubiri maamuzi ya Dodoma, wao wanaregulate na serikali ya jimbo la Magharibi n.k. ila masuala kama ulinzi yanabaki kwa serikali kuu.

Tusipotoshe
 
Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣
 
Mfumo wa majimbo kwa waafrica bado Sana...changamoto zake bado waafrika hawana uwezo wa kutatua
 
Kenya ilianza na ukabila na ndio unaowatafuna mpaka muda huu....majimbo yamekuja kuongeza balaa zaidi.....

Sera yenu ya Chadema ndiyo hayo majimbo yenyewe kwa kutaka halmashauri ya "Kalambo" ijikusanyie Kodi na kujipangia matumizi yake......

Nchi kama Tanzania inajulikana baadhi ya Kanda zina raslimali nyingi zaidi ya nyingine.....itafikia kipindi hizo Kanda zitauona mzigo kuchangia pato kubwa ndani ya serikali kuu na kutokea waasi na kuwa mwanzo wa kutaka UHURU WAO.........

Si siri baadhi ya maeneo nchini hapa yalitaka KUJITENGA toka enzi za uongozi wa hayati Mwalimu Nyerere......
 
Yaani ikitokea marais 3 wanakufa ndani ya kipindi kimoja cha utawala basi nchi iingie gharama za uchaguzi mara 3 Khaaa 😳🤣🤣
Kwani vifo vitatu ni expected occurence? Unasahau 2016 tulifanya chaguzi ya marudio zenji? Kila kitu ni mipango na chaguzi zinaachana siku 90 tokea makamu ashike nadhani so within that time frame serikali inakua imejipanga.

Tuige mazuri na yale mabaya tuyaache kuliko kupinga mfumo mzima kisa tu "Ethiopia mfumo umefeli"
 
Naunga mkono hoja mfumo wa Majimbo kwa Tanzania hauna umuhimu wowote. Sana sana unaweza kuhatarisha umoja wa kitaifa ambao umejengwa kwa juhudi kubwa hasa kipindi nchi inapata uhuru.

Jambo la kufanya ni kupunguza madaraka ya Rais kikatiba ili kuongeza ufanisi katika utendaji, pamoja na uwajibikaji wa watumishi wa umma. Pia kupunguza utitiri wa viongozi ili kupunguza matumizi ya serikali. Kwa mfano, badala ya kuwa na RC, RAS ambao ni wateule wa Rais kila mkoa ungekuwa na Chief Executive Officer (CEO) ambaye anapatikana kwa kuomba kazi na kufanyiwa usaili (interview) halafu athibitishwe na Bunge. Ukiangalia katika level ya Wilaya pia kuna mengi ya kurekebisha
 
Na kwa kuwa vifo si expected occurrence ndio maana framers wa katiba yetu waliliona hilo kuwaepushia wananchi gharama za chaguzi za mara kwa mara....au bado unataka tuendelee kuchangiwa fedha za uchaguzi na wahisani wetu?!!!
 
Majimbo yamepunguza ukabila in fact ili ushinde Urais ni lazima upate kura kwenye kaunti sio chini ya 27 so imelazimisha vyama kuwa vya kitaifa na sio vya kikanda tena.

Kingine mfano kuwapa kanda ya ziwa haki ya kuweka vipaumbele vyao mbele na kujipangia bajeti ni jambo jema maana shida yetu ni kuwa dodoma inataka iwapangie sera uniform maeneo yote bila kujali tofauti zao.

Kuhusu majimbo ya CHADEMA nmekueleza zinatumika halamshauri zilizopo tofauti ni kwamba zinakua cordinated kwenye ngazi ya jimbo kama tu mahakama kuu ilivyo tu inaendeshwa kwa kanda ama Tanesco.

Kuhusu rasilimali haumiliki zote hta Kenya kwenye mafuta county ya Narok inagawana na serikali kuu ya Nairobi ambayo nayo ina reinvest kwenye maeneo mengine makame kma Marsabit n.k. Na hili limechochea mashindano ya county katika kubuni mapato mapya na inaharakisha maendeleo.

So hta Mtwara na Lindi gesi haitokua yao 100% but itachochea na wao kujisimamia kulingana na absolute advantage walizokuwa nazo na kma kanda ikifeli inapewa support na serikali kuu ama otherwise inarudi chini ya usimamizi wa serikali kuu kwa muda!!

Tusiwe pessimistic tuangalie positives zaidi
 
Na kwa kuwa vifo si expected occurrence ndio maana framers wa katiba yetu waliliona hilo kuwaepushia wananchi gharama za chaguzi za mara kwa mara....au bado unataka tuendelee kuchangiwa fedha za uchaguzi na wahisani wetu?!!!
sio expected occurence lakini ni risk kubwa makamu kupewa Urais bila mandate ya watu, na ndio maana kuna watu serikalini wanampinga Mama wazi wazi sababu wanajua hana mandate yao. Na kaingia kwa sheer luck.

Kwani kurudia uchaguzi ni recurring event?? Si ni once in a lifetime?
 
Sasa hiyo sio amani, huo ni ujuha. Watu wanalalamika mioyoni. Sijajua wewe upo class gani, lakini sisi tunaotoka poor class tunajua namna nchi ilikotoka na inavyozama baharini. Waulize wafanyabiashara na wakulima namna mambo yalivyo magumu. Anyway labda kama tunaishi ilimradi tuneamka salama basi sawa. Lakini tukitaka maendeleo ya kweli, lazima tuwe na watu wanaohoji na sio kukaa. Na maumivu moyoni.
 
Kwako wewe sababu siyo majimbo. Ila, kwa wengine sababu ni majimbo.

Kwanza kabisa, majimbo hutokana na kutokubali kuwa chini ya serikali moja. Yaani nchi ipo na watu ambao hawapo tayari kuwa na nchi moja inayotawaliwa na serikali moja based on interest.

Solution huwa ni kuwa na makundi ya watu wenye interest moja (kabila, resources, religion etc.. ) kutaka kuwa na degree fulani ya autonomy. Sasa sehemu za mipaka ya autonomous regions huwa zina migogoro ya kuingiliana, pia contribution to the federal government huwa inaleta hamu ya ku-recess na movements from one group of people to the other huwa inakuwa limited, au hata wakihamia huwa wanakandamizwa kiaina fulani.

Especially kwenye jamii zetu ambazo bado zipo primitive.

Hizo nchi zote ulizozitaja, majimbo ndiyo sababu ya vita.

jimbo la Bururi (Burundi)
North Kivu (DRC), resources and proximity to the ethno-state (Rwanda).
Cabinda (Angola) resources and proximity to the mainland (Jiografia ya Cabinda ni kama ipo Congo kuliko Angola, easy to rebel).
Ukienda india na Pakistan/Kashmir
China na Taiwan (sasa hivi Hong Kong wana rebel sababu ya western democratic tradition vs. Eastern dictatorial tradition)
Russia/Chechnya
United States civil war ...
 
It's not nonsense, you are just too delusional.
Uta-argue vipi kuhusu majimbo bila kuhusisha geographic location?
Na uta-argue vipi kuhusu wars bila kuhusisha resources?
Resources ndiyo zina-create boundaries between a group of people especially when they don't want to share.
Majimbo yanawapa nguvu makundi ya watu waliogawanyika kutokana na resources (resources are a function of a geographic location).
Wenyeji??? What the f#ck is wenyeji?? At what part of the human timeline utasema hawa ni wenyeji???

Unabisha vitu obvious just because you wana be affiliated with a bogus policy that failed miserably at the ballot box. Stop affilliating your facts with a group of failed politicians.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…