Faida chache ni hizi;
Mgogoro wa kiwanja mtaani kwenu hautasubiri maamuzi ya Lukuvi kutatuliwa. Utawala uliopita hadi jiwe alikuwa ana deal na migogoro ya viwanja huko vijijini. Imagine mtu kutoka ofisi namba moja anashugulikia kesi za mashamba vijijini!
Jimbo likipata bahati mbaya ya kuwa na viongozi kama Bashite anayevamia ofisi binafsi za watu au Sabaya ni rahisi kumuondoa na kumwajibisha.
Hizi sarakasi za wamachinga zinazoendelea kama kungekuwa kuna serikali za majimbo lazima kuna jimbo mojawapo ambalo lingepatia vizuri na lingekuwa mfano kwa majimbo yote kushugulika na wamachinga.
Kama kungekuwa na majimbo suala la Korosho lisingeingiliwa na jeshi wala usingekuwepo uvamizi uliofanyika bureau de changes.
Ukiwa na serikali ya majimbo hutamsubiria waziri kutoka Dodoma akuambie kwa nini barabara za lami hakuna, maji na umeme ni shida. Utambana gavana wako hapo jimboni kwa sababu yeye ndiye atakuwa na bajeti na msimamizi wa hiyo bajeti. Akishindwa kutatua utamuondoa mapema kwa "recall" au uchaguzi unaofuata na hatakuwa na pa kwenda akipoteza ajira jimboni kwake.
Ziko faida lukuki za majimbo, hizi ni chache sana.