Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Na, Robert Heriel Tz
PART 1: SAFARI YA TERA
Huwezi zungumzia Taifa la Israel bila kumzungumzia Tera. Wazo la Israel kwenda Kanaani (Palestine) ya leo liliasisiwa Tera.
Tera ndiye Baba wa Abraham, Nahori na Harani. Tera alikuwa akiishi Uru ya Ukaldayo (Kati ya nchi ya Shinari na bara Aram) hata hivyo eneo hilo kwa wakati huo lilifahamika Kama nchi ya Aram ambapo waliishi Waram alioongea kiaramu.
Tera mbali na kuwa mfugaji pia alikuwa ni mchongaji wa vinyago na sanamu ambapo kazi hiyo ilimpa kipato kutokana na wakazi wa Uru walipenda kuabudu miungu ya sanamu.
Tera Kama binadamu mwingine aliamua kutafuta fursa sehemu zingine kuongeza pato lake kutokana na shughuli yake ya uchongaji na ufugaji (hasa ule ufugaji wa kuhama hama Kama wamasai, wasomi huutambua Kama Nomadic life)
Eneo nyeti Kwa wakati huo lilikuwa ni Kanaani, ambayo ilikuwa na malisho Kwa mifugo, na pia ilikuwa Route muhimu kuingilia Afrika na kwenda nchi za Mashariki ya mbali. Hivyo kibiashara Kanaani Tera aliiona ingemfaa Kwa kazi yake ya uchongaji.
Mambo ya Tera yakazidi kuwa magumu hasa baada ya mtoto wake wa kiume aitwaye Harani Kufariki. Hii ikamfanya azidi kuichukia nchi ya Uru na kuongeza ari ya yeye kuhama nchi hiyo. Kama haitoshi, mkwe wake Sarai ambaye ni mke wa Ibrahimu naye mambo yalikuwa magumu kwani alikuwa Tasa. Hii ikamfanya Tera aone nchi ya Uru haimfai kwani inamletea majanga katika familia yake. Hivyo ahame nchi nyingine (shabaha yake ikiwa Kanaani) kutafuta bahati yake.
Kizamani kufiwa na mtoto lilikuwa ni Jambo baya zaidi lisilosemeka. Ilifahamika kuwa mzazi ndio alipaswa kufa kabla ya mtoto. Hivyo Tukio la kifo cha Harani kiliusononesha moyo wa Tera. Na baadhi ya vitabu vinaeleza kuwa maisha ya Tera yalianza kuharibika kuanzia hapo.
Tera akaondoka Uru ya Ukaldayo akiwa na Ibrahimu mwanaye, Sarai mkwewe, Lutu mtoto wa Harani, na watumishi wengine, hapa Nahori hajatajwa ingawaje Nahori alioa binti wa Harani aitwaye Milka.
Inaendelea...
PART 1: SAFARI YA TERA
Na, Robert Heriel Tz
Kusema Nahori alichukua binti ya Harani (nazungumzia nchi sio Harani ndugu yake). Tera akaondoka Uru wa Ukaldayo na akatembea maili nyingi akielekea Kanaani, safari yake iligota katika nchi ya Harani. Hapo alikaa Kwa muda mrefu mpaka umauti ulipomfika, akafa na ndoto yake ya kufika Canaan.
Pengine sababu ya kukaa muda mrefu yaweza kuwa ni kuona jina la mwanaye Harani likifanana na jina la nchi hiyo, Harrani ingawaje hakukuwa na mahusiano ya kimaana baina ya majina hayo. Kuishi Harani pengine kulimpa faraja pale asikiapo jina hilo likitajwa.
Pia, sababu ya pili yawezakuwa ni uwepo wa baadhi ya ndugu katika nchi ya Harani hasa ndugu zake Labani ambao baadaye kupitia ukoo huo Isacka alimpata Rebeka, na Yakobo akapata wake zake yaani RRaheli na Leah binadamu zake kutoka Kwa mjomba wake Labani.
Safari ya Tera iliishia hapo nchi ya Harani, akiwa Mzee wa miaka Mia mbili na tano -205. Safari ya Tera ukawa turning point Kwa Ibrahim na waisrael mpaka hivi leo.
Tera alipokufa, Ibrahimu hakutaka kuendelea kuishi nchi ya Harani, Maandiko yanasema Mungu aitwaye Yahwe alimtokea na kumwambia aende Mpaka nchi atakayomuagiza, akiirejelea nchi ya Kanaani ambayo Baba yake, Mzee Tera ndio ilikuwa ndoto yake.
Ibrahimu akakusanya virago, mke, na Lutu mtoto wa ndugu yake, pamoja na yote waliyoyapata wakiwa Harani wakachanganya Mbariga kuelekea Kanaani.
TUNAENDELEA PART 3
Isemayo, SAFARI YA ABRAHAM
Uru ya Ukaldayo, Kwa Leo ndio Iraq mji wake Mkuu ilikuwa mesopotamia. Harani hivi leo ni Uturuki ya Kusini, Canaan kwa leo ni Gaza, westbank, ndio Palestine, na Maeneo ya Jordan.
Ulikuwa nami
Robert Heriel
Taikon WA fasihi
06933223000
Hadi kesho tena.
Part 2
Post in thread 'Mgogoro wa Israel na Palestine -- safari ya Tera' Mgogoro wa Israel na Palestine -- safari ya Tera