TRA Tanzania Wanalijua hili na ndio wamefanya kama mtaji wa kula rushwa, bila sheria ngumu kama hizi ambazo hazitekelezeki wanajua hawawezi kuomba rushwa.., sasa hii 100mil. iliwekwa tangu kipindi soda inauzwa 150/=, hadi leo soda inauza 600/= bado kiwango ni hicho hicho.., hii amount imepitwa na wakati sababu ya inflation, pesa imeshuka thamani. Huyo CPA sisi tutamlipa nini kupiga hayo mahesabu kila siku, mbaya zaidi kodi za bandari zinasababisha waagizaji wasitupe risiti kamili, sasa mimi nitoe risiti ya VAT itakuwaje, si nitafilisika?!
Kama haitishi, mtu mwenye duka pembeni yangu hana VAT, mimi nimeunganishwa na VAT , kwahiyo bidhaa yangu itakuwa bei juu, nani atanunua kwangu?!