Mgogoro wa Kariakoo sio rahisi kuumaliza, bado yataendelea

Kama hakuuweka yeye na yeye ni daktari wa filosofia ya uchumi, aziondoe basi. Kuna tatizo gani kuondoa kero, au usomi ni madoido tu sio kunufaisha jamii?
 
Serikali yetu sio Rafiki kwa wafanyabiashara wa ndani (yaani sisi wazawa) lakini mwisho wake unakuja tuta wanyoosha
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Umewahi kufanya biashara?
 
100 m ni sawa na mauzo ya sh 275000 kwa siku ni hela ndogo, ambayo ni faida ya ya elf15 au 16 kwa siku, fikiria unapata faida y 15 kwa siku alaf unatakiwa kumuajiri mwasibu mwenye CPA, ni kitu ambacho hakiwezekan ndo maana wafanyabiashara wanakwepa kutoa risit ili unbalance mauzo usiingie VAT
 
TRA Tanzania Wanalijua hili na ndio wamefanya kama mtaji wa kula rushwa, bila sheria ngumu kama hizi ambazo hazitekelezeki wanajua hawawezi kuomba rushwa.., sasa hii 100mil. iliwekwa tangu kipindi soda inauzwa 150/=, hadi leo soda inauza 600/= bado kiwango ni hicho hicho.., hii amount imepitwa na wakati sababu ya inflation, pesa imeshuka thamani. Huyo CPA sisi tutamlipa nini kupiga hayo mahesabu kila siku, mbaya zaidi kodi za bandari zinasababisha waagizaji wasitupe risiti kamili, sasa mimi nitoe risiti ya VAT itakuwaje, si nitafilisika?!

Kama haitishi, mtu mwenye duka pembeni yangu hana VAT, mimi nimeunganishwa na VAT , kwahiyo bidhaa yangu itakuwa bei juu, nani atanunua kwangu?!
 
Mfano mdogo tu ni Pharmaceutical products, faida ni nusu almost ya mauzo. Kkoo akiuza mzigo wa 5m kwa siku faida si chini ya 2m, hao jamaa ni hawataki kulipa kodi, VAT ni ya mnunuzi ndio analipa, wao inawauma nini ?
Ungekua unajua VAT inavyofanya kazi, usingeandika hiyo post. Unaonekana wewe ni mweupe sana, both kwenye biashara na kwenye mambo ya kodi.
 
Boss acha mihemko ya kung'ang'ania wafanyabiashara kuwa ni wakwepa kodi kwa kiwango kikubwa.

Wafanyakazi mishahara inayoisifia mno inatoka wapi kama sio kodi za wafanyabiashara?

Serikali isikilize hicho kilio, iweke mifumo mizuri ya kukusanya kodi. Mfumo wa VAT utazamwe upya. Hii nchi kodi zinalipwa na bado Rushwa zinatololewa sababu ya mifumo mibovu, Rushwa zote zikiminywa zikawa kodi nchi itapata zaidi.
 
Utaratibu gani mkuu wa ajabu? Pos au efd ziko Kila Nchi hasa hapa Africa
Huwezi ona sababu ww si mfanyabiashara na umeshawabrand kuwa ni wezi na majambazi.

Ukiwa na akili ya kibiashara utajua kuwa watu hawatoi risiti kwa sababu 3.

1. Kukwepa kuingia VAT sababu ya gharama za uendeshaji biadhara ukiwa VAT ikiwemo kufile return ambazo ukichelewa unapigwa fain.

2. Yupo VAT ila anapunguza mzigo ambao aliuziwa bila risiti ya VAT hivyo hana pa ku claim VAT mfano. Anakuja mtu ana kuuzia vitu kibao bei chee na risiti anakupa ila yeye sio VAT.

3. Yupo VAT na waliomzunguka wakiuza bidhaa kama zake hawapo VAT sasa ushindani unampotezea wateja sababu ya hiyo 18% .

Hizi ni changamoto ambazo zinatatulika iwapo serikali itawasikiliza na sio kama unavyotaka ipige na rungu sababu ni wezi.
 
NJAA HAINA BAUNSA serikali ikaze ndani ya wiki watarudi wenyewe. Wanataka waendelee kukwepa Kodi kwa kutegesha maduka kadogo wakati mambo yote yanafanyika stoo na godown? Kwa nini walivyobiwa habari ya kusajili stoo wamekuja juu kama mbogo? Wanajiliza wee ila uwakute site za ujenzi au kwenye burudani lakini serikali ikitaka Kodi anakuonyesha fremu ISIYO na kitu wakati Mali zipo stoo na zinauziwa kwa jumla huko huko duka ni ofisi tuu
 
Mfanya biashara ndo anategemewa atumie rasilimali zake kukusanya mapato apeleke TRA. Anatakiwa afanye biashara, alipe kodi yake, ahakikishe TRA imepata VAT zake, PAYE zake, Witholding zake na taarifa za hizo kodi kwa wakati kwa kutumia muda wake na rasilimali zake.

Halafu anatokea mtu anasema mfanya biashara ni mwizi msijadili naye alazimishwe.

Mfano, nikuulize kodi ya VAT mfanyabiashara anakusanya kwa niaba ya TRA, anatakiwa afile return kabla ya tarehe 20, asipofile anapigwa fain. Anatakiwa awe na computer, internet, mtu wa kufile na hicho kiasi kiende bank. Yeye anapata nini kufanya hiyo kazi ya kwa niaba ya TRA?
 
Binafsi nakubaliana na Mfanyabishara aambae analeta alternative ila sio kupinga tuu Kodi ,kama serikali imefanya uchambuzi na kuona hiyo alternative sio endelevu na Haina Tija hawawezi kuikubali.
% Kubwa ya wafanyabiashara wanatamani kufanya biashara kwa amani ndio maana wanatoa hata Rushwa wasisumbuliwe. Mtu anayeweza kutoa Rushwa anaweza kulipa kodi kama si kandamizi.

Kama kakadiriwa M100 na ana mtaji wa M200 hawezi lipa hiyo kodi ila atatoa Rushwa ya m10-m20 alipe kodi ya m5.

Huyo ukimwambia lipa kodi ya 10m-m20 hutasumbuliwa kwanini asilipe wakati kasave 5m ambayo angeilipa iwapo angelipa kodi ya M5 na kutoa M20 kama Rushwa?

Na ukumbuke, mfanyabiashara yupo hapo miaka yote. Kila mwaka Afisa kazi yake itakuwa ni kumfata kuchukua m20 na kumpa makadirio ya 5m sababu tu mfumo unaruhusu. Na yeye ataficha mauzo.
 
Pale wamesikilizwa wao tu. TRA haijasikilizwa. Serikali utakaa chini na kuisikiliza TRA. Kama yule mama wa vitenge, mama bonge. Ukisikiliza upande wa TRA anaanguka chali. Kuna maeneo TRA unakosea lakini kwenye myororo mzima wa utozaji wa kodi. E-filling na tancis inawaua sana wakwepaji kodi. Hata kama huna VAT ukauza mzigo wa magendo kwa EFD utakosa kuthibitisha manunuzi yako. Maanake watachujua kiasi chote cha risiti kama mapato.
 
Ulipaji Kodi ni muhimu.sana kwa taifa lolote linalotaka maendeleo endelevu watoto wanatumia udhaifu uliopo kufanya
Bunge lilikaa Kama Kama likawa linapitisha bajeti ya wizara ya fedha kifungu kwa kifungu na vikapita hii kwa maslahi ya baadhi ya wabunge na vigogo wenye biashara zao pale kariakoo Kodi zipunguzwe kiboyaboya tu
 
Kufunga biashara sio kosa ila inategemea ni biashara gani.
Kwa taarifa tu Kariakoo kwa mwezi mmoja inaiingizia serikali zaidi ya billioni 10, katika hizo zaidi ya 80% ni kodi ya VAT, kama haujui VAT inapatikana kwa kuuza biashara, na bila biashara hakuna VAT.
Mkuu biashara zote za Kariakoo zikifungwa kwa siku moja serikali inapoteza zaidi ya TZS milioni 300.
Ulishangaa kwanini waziri mkuu aliacha bunge akaja kuwasikiliza wafanya biashara wa Kariakoo??
Kariakoo TRA inaiita ni mkoa wa kiko.
Usiongee kwa jazba, Kariakoo ni uwanja mwngine kabisaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…