Kuna mke na mume wameanza mgogoro mkali ambao unatishia ndoa kuvunjika. Miaka miwili iliyopita walioana na sasa wana mtoto mmoja na wote ni waajiriwa wa serikali na wote wameanza kazi intake moja ila idara tofauti.
Wote wanatokea familia masikini ila familia ya mwanamke ina ahueni kidogo maana wazazi wake wanaishi nyumba ya kudumu ingawa ni ya zamani na imechakaa ila kwa mwanaume wazazi wake wanaishi nyumba za tembe na makuti.
Wote walikopa hela bank kama million 25 kwa kutaka angalau wawajengee wazazi na wakakubaliana kuanza kuwajengea wazazi wa mwanaume. Baada ya hela kuingia mwanamke amegoma kutoa hela anataka awajengee wazazi wake kwanza maana wamesumbuka kumsomesha.
Mwanaume anakataa anasema makubaliano yaheshimiwe lakini mwanamke anakataa. Baadae mwanaume akapendekeza basi hiyo hela wanunue kiwanja wajenge nyumba yao, mwanamke akasema sawa wewe kama mwanaume nunua kiwanja mimi nitajenga msingi wa nyumba panapobaki umalizie hela yangu inayobaki niwajengee wazazi maana wamenitoa mbali.
Mwishowe mwanamke akasema hivi ungenioa bila kazi ungesema hayo unayotaka nifanye, wewe kama mwanaume wajibika kuwajengea wazazi wako, kisha jenga nyumba yetu na mimi niwajengee wazazi wangu.
Jamaaa anawaza sana anatishia kuvunja ndoa, nini kifanyike? NB, Jamaa ana umri wa miaka 36 hivi mke wake miaka 27