mahari ulilipa wewe hhamkulipa wote kuonesha kwamba cha mwanamke ni chake na cha mume(kwa mipaka) ni cha wote.
Mkuu sio DINI WALA sheria za nchi hizi zote zimempa mume wajibu wa kumgharamia mkewe na watoto.
Ndio maana mume ukienda kulalamika serikalini kwamba mkeo halishi familia utaonekana mpuuzi tu.
Mume ndio mwenye majukumu katika ndoa,hiyo ndio asili mzee,msiwatwishe wanawake mizigo isiyowahusu
Samahani kama nitakuwa nimevuka mstari, kwa maoni yako, ni wazi hauko kwenye taasisi hii ya ndoa na huielewi vizuri inapoanzia na inapoishia.
Mahari ikishalipwa, kwa mila nyingi za kibantu, nyumbani kwa mwanamke ni kwa mume wake, na nyumbani kwa mume ni kwake na kwa wazazi wake.
Hii inadhihirishwa pia ule utaratibu uliokuwepo/uliopo wa mwanamke kutumia ubini w mume na watoto kutumia ubini wa baba. Wimbo maarufu ukisema , "ayaya kuolewa, kurudi nyumbani kutembea..."
Ukisema dini, hizi mbili, zinataja majukumu ya mwanamke kwenye ndoa na mwanaume kwenye ndoa, sijui unazungumziaje hapa?
Ukirudi kwenye sheria za nchi, zinasisitiza majikumu ya mwanaume yaliyoainisha kwenye dini, na sheria inasisitiza kuwa mali zote zilizochumwa kwenye ndoa ni za wanandoa wote wawili, hili likidhaniwa mwenye nafasi ya kutengeneza hizo mali ni mwanaume zaidi kuliko mwanamke.
Ukiachana na dini ambayo kimsingi inapinga mwanamke kutafuta na kumpa jukumu la kwanza na la msingi ambalo siku hizi amekabidhiwa beki tatu, sheria itaamuaje ikiwa mwanaume akawajengea wazazi wake ikiwa tayari kuna ndoa na mwanamke akijenga kwao ikiwa yuko ndoani endapo mmoja kati yao akaaga dunia? Nyumba hizo zitajumuishwa kwenye mirathi endapo aliyebaki akidai?
Mara nyingi, demokrasia ikishindikana kwenye ndoa, mfumo dume unashika hatamu na hakuna wa kupinga, ndio sababu ya BABA kuwa kichwa cha familia, hakuna kichwa kilicho juu ya mwili wa kiume kikawa na mawazo yasiyo na jinsia.
Asante.