safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Mkuu pengine mimi naifahamu ndoa vizuri kuliko hata mzee wako(sio wewe tu)wazi hauko kwenye taasisi hii ya ndoa na huielewi vizuri inapoanzia na inapoishia.
Naaaam anakokaa mume ndipo hapo atakapokaa mke,hiyo ni nyumbani kwake kwa mujibu wa kuishi na sio kwa mujibu wa kumiliki.Mahari ikishalipwa, kwa mila nyingi za kibantu, nyumbani kwa mwanamke ni kwa mume wake, na nyumbani kwa mume ni kwake na kwa wazazi wake.
Mke wangu nyumba yangu mimi ndio nyumbani kwake kwa sababu ndo anatakiwa aishi hapo,na sio ni nyumbani kwake kwa maana ya kuwa anaimiliki ile nyumba naye ni yake hapana.
Hivyo neno "NYMBANI KWAKE" hutakiwi kiingia kichwa kichwa mkuu.
Hayo ni mambo ambayo hayahukumu juu ya kuwa mali ya mke ati mume aichukue bila ridhaa ya mke mwenyewe.Hii inadhihirishwa pia ule utaratibu uliokuwepo/uliopo wa mwanamke kutumia ubini w mume na watoto kutumia ubini wa baba. Wimbo maarufu ukisema , "ayaya kuolewa, kurudi nyumbani kutembea..."
Yaani kuhalalika kwa baadhi ya mambo kwenye ndoa sio kwamba yamehalalika mambo mengine yote.
Mambo ya jina yatabaki kuwa jina,na mambo ya mali yatabaki kuwa mali,hakuna mahusiano hapo ati useme kwa kuwa kwenye jina mke ananasibishwa na mume basi na mali ya mke ni ya mume pia,hii haipo kabisa.
Utaratibu wa wapi wa ajabu namna hii.
Nazungumzia kama mwqnzo kwamba mali ya mwanamke ni ya mwanamke na mali ya mwanaume ni ya mwanaume maadamu bado mupo kwenye ndoa.Ukisema dini, hizi mbili, zinataja majukumu ya mwanamke kwenye ndoa na mwanaume kwenye ndoa, sijui unazungumziaje hapa?
Tofautisha mambo haya.
Mali ya wanandoa wakati wanaachana.
Mali ya wanandoa endapo mmoja wao akifa.
Na mali ya wanandoa wakati wapo pamoja.
Hapa nimekupa mambo matatu mkuu.sheria inasisitiza kuwa mali zote zilizochumwa kwenye ndoa ni za wanandoa wote wawil
1.mali za wanandoa endapo wakiwa pamoja.
2.mali hizo endapo mmoja akifa.
3.mali hizo wanapokuwa wapo katika ndoa.
Hakuna uhalali aw mwanamke kujichukulia mali ya mumewe atumie anavyotaka ilhi bado wapo katika ndoa hawajaachana.
Maadamu mtu hajaachana na mumewe basi mwanamke hana uhuru wa kusema hii mali yetu sote acha niifuje no no.
Na mwanaume pia huwezi kusema huu mshahara ni wa mke wangu acha niufuje tuu nifanyie mambo yangu,hiyo haiwezekani.
Ndio maana kama mfanyakazi hatoi huduma kwa watoto mke akienda kushtaki yule mume atakatwa kiasi fulani cha pesa cha kuwatosha watoto na mke then ingine anaachiwa mwenyewe.
Sio kwamba mume atakatwa pesa yote no no..
Maadamu umeuliza kisheria basi mimi sio mtaalamu wa sheria hizi za NCHI SIJUI zinasemaje.Nyumba hizo zitajumuishwa kwenye mirathi endapo aliyebaki akidai?
Lakini hata katika sheria ya dini iko hivi..
Ikiwa mume au mke alishasema bayana wakati wa uhai wake kwamba hiyo nyumba sio yake kwamba kamjengea mtu fulani manake ameshaitoa mali hiyo katika milki yake wakati yupo hai kabla hajafa,hivyo hata akifa hiyo haiingii katika mirathi kwa sababu sio yake alishakwisha igawa.
Ni sawa na wewe umpe mtu zawadi ya gari leo alafu baada ya miaka 5 Mungu akuchukue eti watu watake kurudisha hii gari uliyogawa nayo waitie kwenye mirathi wakati ishampa mtu.
Katika uislamu nafahamu iko hivyo na Mola ndio mjuzi zaidi.
Mfumo dume ni jina baya lenye kutia chuki ambalo lina malengo ya kuleta usawa baina ya mwanamke na mwanaume usawa ambao haupo kiufupi.mfumo dume unashika hatamu na hakuna wa kupinga,
Lazima kila sehemu awepo mtu ambaye atamzidi mwenziwe kikauli na mamlaka hivyo maisha ndo yanaenda vizuri.
Asante