Mgogoro wa ndoa: Tuanze kuwajengea nyumba wazazi wa nani?

Mgogoro wa ndoa: Tuanze kuwajengea nyumba wazazi wa nani?

Kila mtu na roho yake, Niko maskini lakini mali na pesa hazinipelekagi mputa mputa sijui nina kaujinga, naona km mke kakosea sababu walikubaliana kiroho safi kubadilika mwishoni maana yake Ni utapeli uhuni na wizi kwa mume wake,, narudia Tena mume wake wa ndoa😲 aisee poleni wanaume baadhi mko gerezani
 
Kuna mke na mume wameanza mgogoro mkali ambao unatishia ndoa kuvunjika. Miaka miwili iliyopita walioana na sasa wana mtoto mmoja na wote ni waajiriwa wa serikali na wote wameanza kazi intake moja ila idara tofauti.

Wote wanatokea familia masikini ila familia ya mwanamke ina ahueni kidogo maana wazazi wake wanaishi nyumba ya kudumu ingawa ni ya zamani na imechakaa ila kwa mwanaume wazazi wake wanaishi nyumba za tembe na makuti.

Wote walikopa hela bank kama million 25 kwa kutaka angalau wawajengee wazazi na wakakubaliana kuanza kuwajengea wazazi wa mwanaume. Baada ya hela kuingia mwanamke amegoma kutoa hela anataka awajengee wazazi wake kwanza maana wamesumbuka kumsomesha.

Mwanaume anakataa anasema makubaliano yaheshimiwe lakini mwanamke anakataa. Baadae mwanaume akapendekeza basi hiyo hela wanunue kiwanja wajenge nyumba yao, mwanamke akasema sawa wewe kama mwanaume nunua kiwanja mimi nitajenga msingi wa nyumba panapobaki umalizie hela yangu inayobaki niwajengee wazazi maana wamenitoa mbali.

Mwishowe mwanamke akasema hivi ungenioa bila kazi ungesema hayo unayotaka nifanye, wewe kama mwanaume wajibika kuwajengea wazazi wako, kisha jenga nyumba yetu na mimi niwajengee wazazi wangu.

Jamaaa anawaza sana anatishia kuvunja ndoa, nini kifanyike? NB, Jamaa ana umri wa miaka 36 hivi mke wake miaka 27

Utoto unawasumbua, wakibahatika kukua wataacha!
 
Nyumba iandikwe jina la mwanaume kwa sababu tayari kuna mgogoro. Then kila kitu cha familia akiongoze mwanaume tu.

Hii ndiyo shida ya kuoa mke mnayelingana kipato[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Hivi inakuwaje mwili mmoja unabishana na kupingana kiasi kile! Kazi ya kichwa ibaki ya kichwa na ya kiwiliwili ibaki ya kiwiliwili!
 
Mwanaume mjinga sana. Mwanaume Ana wajibu wa kutunza familia yake. Mke wangu sijawahi kumuuliza mshahara wake.
Natoa pesa ya kila kitu na kukamilisha majukumu yote Kama baba.

Pesa yake Kama akiamua kuileta kwenye familia sawa. Akiamua kuwapa ndugu zake atajijua mwenyewe. Lakini hatakiwi kuniuliza pesa ya kuhonga natoa wapi? Na hatakiwi kujua mapato yangu yote. Hayamuhusu
Wewe ndo mwanaume sasa[emoji848]
 
Kila mtu na roho yake, Niko maskini lakini mali na pesa hazinipelekagi mputa mputa sijui nina kaujinga, naona km mke kakosea sababu walikubaliana kiroho safi kubadilika mwishoni maana yake Ni utapeli uhuni na wizi kwa mume wake,, narudia Tena mume wake wa ndoa[emoji44] aisee poleni wanaume baadhi mko gerezani

Ukiachika tu 'nakuwowa'.[emoji8]
 
Kwa macho ya kawaida siyo kosa, ila ukishaingia kwenye ndoa na bahati mbaya mmoja akawa mbinafsi basi KIPATO KULINGANA inakuwa kosa. Imagine mume angekuwa na kipato Mara tatu zaidi ya mke wake, ni wazi kwamba mwanamke angekubaliana na mpango wa kuwajengea wote kirahisi sana ila kwakuwa anajua wote wako sawa so Kila mtu anaamua anachotaka[emoji847]
Umoja ni tunda la upendo uso ubinafsi! Hapo hakuna ndoa ni kupitisha muda tu! Jeuri, ubabe, ubinafsi na ujuaji mwingi wa nsomile ni anguko la dhahiri la u'1' ktk ndoa!
Hapo ni kama kujengea tope tofari ya 'block'! Au mortar cement kwenye tofari ya tope!
Hapo hakuna ndoa wala upendo...! Waambie waivunje kwanza ndoa wakautafute kwanza upendo wa kweli kishwa waunganishe vipande vya hiyo ndoa ndipo wataishi na kuifurahia ndoa!
 
Kila mtu na roho yake, Niko maskini lakini mali na pesa hazinipelekagi mputa mputa sijui nina kaujinga, naona km mke kakosea sababu walikubaliana kiroho safi kubadilika mwishoni maana yake Ni utapeli uhuni na wizi kwa mume wake,, narudia Tena mume wake wa ndoa😲 aisee poleni wanaume baadhi mko gerezani
Huyo ana washauri wengi! Ki uhalisia, yeye mke na kila alichonacho ni cha mumewe n vise versa is true!
 
Siyo mimi ila nipo upande wa mwanaume, maana mpaka wanakubaliana walikubali kuchangiana ili kutatua matatizo madogo madogo na makubwa, pia kuoana watumishi ni kuondoa utegemezi, inakuwaje hela ya mwanamke ni ya mwanamke ila ya wanaume ni ya woteee?
Wewe ndo mlengwa[emoji848]
 
Na busara yenye busara ni kuvunja ndoa tu, jamaa ajengee wazazi wake kabla hajafikisha 49 yrs then afu he ndoa na mke mwingine!

Sent from my TECNO CC6 using JamiiForums mobile app
Nayeye wakope washindwe kuelewana waachane[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] akiwa na 54yrs old aoe tena. Mbona patamu hapo. Yaan mwanaume atumie busara ajue kujibeba yeye kama yeye, inamaana kama anguoa mwanamke asye na kazi asingejenga? Achukue pesa yake ajenge kijumba hata cha kawaida huku akidunduliza hela ya kuongeza kwemye ujenzi. Aache mteremko kabisa
 
Sema mi narudia mkishakuwa mwili mmoja ubinafsi unatakiwa kukatiliwa mbali

Mke lazima pia kipato chako kijulikane kinaisadia vip familia, sio hela yako inaishia saloon na nguo

Ni lazima kusaidiana
 
Huyo ana washauri wengi! Ki uhalisia, yeye mke na kila alichonacho ni cha mumewe n vise versa is true!
Katika vitu huwa namshukuru Mungu kaninyima roho ya uroho wa vitu,
 
Umasikini na Ujamaa ni tatizo kubwa sana nchini kwetu
 
Tunajua ni wewe na unataka tusaport ujinga wako ila nikwambie tu hicho kitu unachokifanya ni mambo ya wavulana na sio wanaume,na kama ulioa mfanyakazi ili akufaidishe umeula wa chuya
Uvulana? Huu ni ulimbukeni! Yaani ww mke wangu afu unifinyie pua eti huu ni mshahara wangu ni huna mamlaka nao...seriously! Utajikuta upo kwenu bila kuelewa umefikafikaje!? Mke kusanya chochote ukusanyacho weka mezani nitoe 'approval' ya matumizi yake! Ofcourse kwa jinsi navyokupenda, maamuzi yangu hayatakuwa kandamizi wala dharirishi! Vinginevyo ishi peke yako ujiamlie mwenyewe maisha yako!
 
Back
Top Bottom