Mgogoro wa ndoa: Tuanze kuwajengea nyumba wazazi wa nani?

Mgogoro wa ndoa: Tuanze kuwajengea nyumba wazazi wa nani?

Aya Mambo vijana wanaoa mwanamke ili mgawane kipato ni kufeli kifikra.

Sio eti unaoa kwa kuangalia vyeti au ana KAZI gani.

Kwa WAKATI tulionao Sasa,
Tafuta mwanamke aliyejitunza, mwenye maadili mema, mrembo na anayejitambua.

Afu mpe pesa zako ilulizotafuta kwa jasho lako azisimamie, Kisha Ndio umpangie wewe matumizi.

Kamwe kwenye Ndoa hamuwezi kubishana KIPUUZ NAMNA HII maana anajua Kwenye familia, Mila, desturi na maadili yetu waafrika wewe ni Nani kwake.


Suala la Mwanaume kuanza kupangia matumizi pesa za mkeo alizozitafuta kwa mgongo wa jasho la wazazi wake (wakwe zako) .

Ni kukiuka miiko,Mila na desturi zetu waafrica.

Huu uzungu uzungu vijana wanaouendekeza ndio chanzo Cha matatizo yote haya.

Kiukweli,
Inasikitisha Sana[emoji22]
Vijana wa siku hizi nao wamezidi wanapenda slope sana yaani mtu anaoa kwa target kwamba huyu kila mwezi atakuwa analeta kiasi fulani
 
Masuala ya kujenga hayatakiwi watoto ndio wahangaike kama maisha yenu yalikua mnaishi mbavu za mbwa waliooana sio mtaji eti wawajengee nyumba, maisha ya wawili wanatakiwa kujenga nyumba yao na watoto wao wazazi kama mlikua hamna kwenu imekula kwenu . Maisha ni ya wawili na sio jumla
 
Ubinafsi kwenye ndoa ni janga linaloangamiza. Hapo hawawezi kuongea lugha moja tena, ni heri busara ikatumika.
Na busara yenye busara ni kuvunja ndoa tu, jamaa ajengee wazazi wake kabla hajafikisha 49 yrs then afu he ndoa na mke mwingine!

Sent from my TECNO CC6 using JamiiForums mobile app
 
Kwani hao wazazi wenyewe wamekwambia wanahitaji nyumba?

Wameishi kwa amani miaka yote humo, na wewe umezaliwa na kulelewa kwenye hizo unazoziita tembe leo…. ukiwajengea tu wanaanza kurogana.
 
Huyo mwanaume ni kilaza. Jukumu la kujenga nyumba kwa wazazi wa kiumeni ni la mwanaume. Nafikiri hajui ndoa vizuri
 
Roho za kimasikini kwa wote, yaani ukiwa masikini wa roho hata uwe na mabilioni utabaki masikini tu...

Mume unang'ang'ania hela ya mke ikajenge kwenu? Hapana bwana...ni heri wazazi waishi waishivyo!
 
Wazazi wangu walikuwa masikini sana na kunisomesha kwa jasho na damu. Nikajisemea moyoni hawa ni muhimu kuliko watoto wangu na mke watakaokuja baadae.

Nikaweka vipaumbele vyangu. Kazi, kuwajengea wao kwanza, ndoa na mwisho kujenga mimi na familia yangu.

Hasara yake nilichelewa kuoa, lakin sote tunaishi kwa furaha sasa. Atakaeingilia maisha yangu na mke wangu basi ana shida binafsi.

Hiyo ndoa haitafika mbali mana mwanaume anahamisha majukumu yake ya asili. Mwanamke anakusaidiaje kujenga kwenu? Anahitaji wazazi wake wasemwe vibaya kila wanapokosana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wanandoa kuna sehemu wanafeli tena mwanaume ndio anafeli zaidi. Katika maisha kuna majukumu ya mwanaume ambayo ni kuitunza familia kwa kuwajengea nyumba, kuwalisha na kusomesha watoto na matibabu. Hayo ni majukumu ya mwanaume kama mumu. Mke anaongezea tu pale anapojisikia

Kuhusu kuwajengea wazazi mwanaume pambana na wazazi wako na mwanamke apambane na wa kwake. Halafu jukumu la kuwajengea wazazi ni la familia ya upande husika kama mume ni yeye na watoto wengine wa hao wazazi kadhalika na kwa mke ni yeye na ndugu zake waliozaliwa na hao wazazi

Mwanaume simama kama mwanaume na chukua majukumu ya mume ambayo ni makubwa na pia upambane uwe na kipato kumzidi mkeo. Kamwe kwenye maisha mwanaume hawezi kukaa chini na mwanamke wakapeana majukumu 50/50 hilo sio sawa. Mwanaume ndio anabeba majukumu makubwa ya familia mke anaongezea tu kwa hiyari.

Hapo kachemka mwanaume kwa kutegemea mikopo na mishahara ya mke kuendesha familia haitakiwa kuwa hivyo. Kusaidiana kupo ila sio mke eti akope mkajenge kwa wazazi hapo mmezingua
 
Mkuu kubali mwanamke akajenge kwao kwa pesa zake, au mjenge wote nyumba yenu! Wote kwa pamoja mmekopa 25 kila mmoja jumla 50 mil , ajira bado mpya - mmepanga! Natamani hiyo 25mil mnegeanzisha hata mradi ambao mnaufahamu vizuri na mna ujuzi nao ! 25 nyingine kwenye kiwanja chenu...

Njia moja wapo ya kupunguza ubinafsi kuwa muwazi kwa mkeo, hakikisha unamjengea mazingira ya kuamini kila mnachokifanya ni kwa manufuaa ya ndoa yenu na familia yenu wote.. kwa maisha yenu.
 
Kuna baadhi ya Wanawake wamekuwa wabinafsi sana, linapofikia suala la maendeleo wengi hawataki kushare gharama.

Kwa mtazamo wangu, ni heri wangeshare gharama na kufanya ujenzi kwa awamu. Sote tunajua iwapo Mtumishi akikopa Take Home yake hupungua. Hivyo kuna possibilities ya maisha yao ya kila siku ya yaka shake kutokana na take home kupungua.

Na kwa ubinafsi walionesha, ni wazi Mwanaume ndiyo atakayepata tabu kwani Sioni dalili ya Mshahara wa Mwanamke kusaidia matumizi ya nyumbani.

Kwa mkopo waliochukua, ni wazi utaisha baada ya miezi 72 au 84 hivyo natabiri migogoro zaidi itaibuka kwa Familia hii. Hivyo ningeshauri Mume awe mpole kwanza Wakati Mke anajenga kwa Wazazi wake na yeye angesubiri kidogo na awapangie Wazee wake hata nyumba nzima huko Kijijini ambapo Kodi ya Mwaka Mzima haiwezi kuzidi shilingi 600,000 kwa nyumba Nzima.
 
Nadhani kuna pahala sijaelewa.

Jina lililokopa pesa ni la nani au pesa iliingia kwenye jina la akaunti ya nani?
Wote wamekopa na pesa imo kwenye account ya kila mmoja ila ukijumlisha fedha ya mke na Mme ndo wanakuwa jumla ya million 25
 
Wazazi wanaoishi kwenye nyumba za makuti wafikiriwe kwanza, mengine baadae. Ewe mwanamke! Imeandikwa mwanaume ni kichwa cha familia, msikilize bwana wako.
 
Kuna mke na mume wameanza mgogoro mkali ambao unatishia ndoa kuvunjika. Miaka miwili iliyopita walioana na sasa wana mtoto mmoja na wote ni waajiriwa wa serikali na wote wameanza kazi intake moja ila idara tofauti.

Wote wanatokea familia masikini ila familia ya mwanamke ina ahueni kidogo maana wazazi wake wanaishi nyumba ya kudumu ingawa ni ya zamani na imechakaa ila kwa mwanaume wazazi wake wanaishi nyumba za tembe na makuti.

Wote walikopa hela bank kama million 25 kwa kutaka angalau wawajengee wazazi na wakakubaliana kuanza kuwajengea wazazi wa mwanaume. Baada ya hela kuingia mwanamke amegoma kutoa hela anataka awajengee wazazi wake kwanza maana wamesumbuka kumsomesha.

Mwanaume anakataa anasema makubaliano yaheshimiwe lakini mwanamke anakataa. Baadae mwanaume akapendekeza basi hiyo hela wanunue kiwanja wajenge nyumba yao, mwanamke akasema sawa wewe kama mwanaume nunua kiwanja mimi nitajenga msingi wa nyumba panapobaki umalizie hela yangu inayobaki niwajengee wazazi maana wamenitoa mbali.

Mwishowe mwanamke akasema hivi ungenioa bila kazi ungesema hayo unayotaka nifanye, wewe kama mwanaume wajibika kuwajengea wazazi wako, kisha jenga nyumba yetu na mimi niwajengee wazazi wangu.

Jamaaa anawaza sana anatishia kuvunja ndoa, nini kifanyike? NB, Jamaa ana umri wa miaka 36 hivi mke wake miaka 27

Wazaz wao wanaish kwenye miti? Vijana tujenge maisha yetu tusije kuwapa shida watoto wetu mbelen.
 
Back
Top Bottom