Elections 2015 Mgogoro wa UKAWA kuhamia bungeni, Antropia Theoneste akwaa Viti Maalum

Elections 2015 Mgogoro wa UKAWA kuhamia bungeni, Antropia Theoneste akwaa Viti Maalum

Acheni chuki. Mtu wako akikosa mnabaki kianza chuki za kijinga.
 
hii ndio sababu ya kumpa ubunge??

au huyo mtoto ni wa mbowe?

mtoto alihitaji comfortability ya ziwa la mama

Tatizo mkiona wana harakati ni shida, mahaba tupa kule
maombi yenu Mabaya kwa Kafulila yameshindwa,ametangulia mkewe na Kafulila anaenda kushinda,mtaficha wapi nyuso zenu na huyo mmiliki wa ACT
 
Chadema walijua kuna viti maalum na walikua na nafasi ya kumteua huyo Antropia kwa nini asingemuachia Mtatiro asimame kama mgombea pekee wa ukawa?
Huyo dada ametukosesha jimbo la segerea kwa tamaa zake. Kwanza watanzania wengi hawamjui angeanza na viti maalum kabla ya kugombea jimbo wananchi waone uwezo wake ndipo baadaye agombee jimbo.
Wenzake wengi tu walianzia viti maalum wakaonesha uwezo waliporudi majimboni wamechaguliwa. Mfano Ester Matiko, Susan Kiwanga,gekul, Ester Bulaya nk. Mifano ni mingi. Huyo hafai amemnyima Mtatiro nafasi ya uwakilishi.
 
Halaf naamini mtatiro ataingia bungeni tu, wabunge wengi wa CCM waliochaguliwa majimboni ni wagonjwa kuna watakaokufa mapema tu

Alafu tunaomba utwambie mwisho wa dunia itakuwa lini prophet!
 
Kwa hili ukawa wamefanya ujinga kwahyo wanapenda tabia hizi za antropia. Uteuzi umenibore huu

Hakika yote haya yamechangiwa zaidi na udhaifu wa viongozi wa ukawa makao makuu. Wakati ushindani huu ukiendelea Segerea kati ya huyu dada wa chadema ambae ukifuata orodha ya mgao wa majimbo yeye ndie aliekuwa na haki na J.Mtatiro wa cuf nilichangia sana kuwaambia ukawa makao makuu wamtume kiongozi mwenye mamlaka kwenda kutatua mgogoro huu mapema kabla hatujapoteza jimbo kwa ccm kwa kugawa kura. Uelewe wagombea wote hawa wawili walikuwa na ushawishi na nguvu sana. Hili halikufanyika na matokeo wote tumeyaona. Wote wawili kila mmoja alipata kura nyingi tena zinazokaribiana kiasi ukizijumlisha kwa pamoja mgombea wa ccm angeachwa kwa umbali mkubwa.Sasa hili ni funzo lenye majuto sana na ujue hayakutokea Segerea tu ni majimbo mengi.Chadema kama chama kina haki ya kumpa kiti cha upendeleo kwani pamoja na mtifuano huo bado alikuwa na michango kwenye chama huko nyuma.
 
Magamba yameanza fitina. Kwa nini usiseme kwa mama yako kumechafuka ??

Uteuzi huu umetuumiza sana hebu angalia yule Dada wa Dodoma Kunti, kweli anauwezo wa kusema chochote bungeni?,wakati majembe kama Pamela Massay na Rachel mashishanga yanaachwa?
 
Vigezo vya kuwa mbunge maalum ni vipi?

Huyo Antropia hana hivyo vigezo?
 
Katika kuthibitisha ule usemi wa wananchi wengi kuwa UKAWA ni genge la wapiga deal inaonekana mnyukano wa kugawana vyeo umeanza rasmi kabla hata ya kikao cha bunge.

CUF wanalalamikia Anatropia yule dada aliyewakosesha Jimbo la Segerea baada ya kukomaa mwanzo mwisho kutetea haki yake kuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum.

Kimsingi jimbo hilo lilitakiwa kumsimamisha mtu wa CHADEMA ingawa Mtatiro akataka kutia fitna lakini huyu mwanadada akakomaa na baadae kuiacha njia nyeupe kwa mgombea wa CCM.


UPDATES.

Nimetonywa kuwa mgawanyo wa viti maalum ndani ya CHADEMA ndio umeleta mtifuano mkali zaidi.

Watu wanalalamika kukatwa bila sababu.

Watu wanalalamikia nguvu walizotumia kuipambania CHADEMA lakini wamekatwa na baadhi ya waliopata hawakuwahi kuwa kwenye harakati mbalimbali za CHADEMA.
 
Back
Top Bottom