Mgogoro waibuka Moshi Club ,wanachama watoa siku 14 kwa menejimenti

Mgogoro waibuka Moshi Club ,wanachama watoa siku 14 kwa menejimenti

Joined
Jul 30, 2018
Posts
16
Reaction score
19
MOSHI

Moshi Sports Club imeingia kwenye mvutano wa kiutawala baada ya wanachama 16 wa klabu hiyo kuwasilisha malalamiko kwa Trustees, wakidai kuwa uchaguzi wa viongozi haujafanyika kwa mujibu wa masharti ya katiba ya klabu.

Wanachama hao, kupitia barua yao, wanasema kutofanyika kwa uchaguzi kwa muda wanaoutaja kuwa umeainishwa kwenye katiba kumeibua maswali kuhusu uhalali wa uongozi uliopo na namna klabu hiyo inavyoendeshwa.

Kwa mujibu wa wanachama hao, Management Committee imeshindwa kutekeleza baadhi ya majukumu muhimu wanayodai yameainishwa kwenye katiba, ikiwemo kuitisha uchaguzi wa viongozi na mikutano ya wanachama.

Wanasema hali hiyo imewafanya wanachama kukosa fursa ya kushiriki katika majadiliano na maamuzi kuhusu masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa klabu.

Wanachama hao pia wanataka Management Committee kutoa maelezo ya wazi kuhusu sababu za kutofanyika kwa uchaguzi, huku wakitaka kuitishwa kwa kikao cha wanachama ili kujadili hali ya klabu na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Aidha, wanadai kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao uhalali wao unahitaji kufafanuliwa kwa mujibu wa katiba, wakitaka Trustees kuthibitisha uhalali wa viongozi waliopo madarakani.

Katika barua hiyo, wanachama hao wameomba hatua za haraka zichukuliwe ili klabu irejee katika mfumo wa uendeshaji wanaodai umeainishwa kwenye katiba, ikiwemo kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi.

Wameitaka pia Management Committee kutoa majibu kuhusu hoja walizoibua ndani ya siku 14 tangu tarehe ya barua hiyo.

Mgogoro huo sasa umeelekezwa kwa Trustees wa Moshi Sports Club, huku wanachama hao wakisubiri majibu na hatua zitakazochukuliwa kuhusu uchaguzi na uendeshaji wa klabu.
1.jpeg
2.jpeg
images.jpg
 
Back
Top Bottom