DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud Said, amesema moja ya ajenda zake kuu endapo atapewa ridhaa ya kuongoza ni kuruhusu ulimaji wa bangi kwa matumizi ya kiuchumi, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kuwa mkombozi wa maisha ya wananchi na chanzo kipya cha mapato kwa taifa.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya uteuzi katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maisara – Mjini Unguja, Said amesema sera hiyo inalenga kuwainua wakulima, kuongeza ajira na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Aidha, amependekeza watu wanaotumia kilevi kupewa leseni rasmi, kwa lengo la kudhibiti matumizi na kuweka mfumo wa kisheria utakaorahisisha ukusanyaji wa kodi.