Hakika Mungu asaidie Watanzania tufanikishe mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya uende kwa amani na hatimae tupate katiba mpya kwa niaba ya Watanzania.
Moja ya kiu kubwa ni kuona katiba inatamka haki ya kikatiba ya Mtanzania kama haki ya kuchagua na kuchaguliwa inafanya kazi hasa kwenye kipengelee cha Kuchaguliwa.Manake kwenye kipengele hicho ndiko tutapata mgombea binafsi au mgombea huru asiye na chama chochote cha kisiasa.
Kwa sasa vyama vya kisiasa vimeibuka na aina ya udikteta wa aina yake ambao umekuwa ni mfumo kuwa pasipo aina fulani ya Itikadi ambayo siyo itikadi lasmi ya chama basi mfuasi wa chama hicho hana haki dhidi ya chama chake.Wenye sale za kichama wanajua jinsi kwa baadhi ya watu katika vyama vya kisiasa wamegubikwa na tamaa ya fedha,mitandao, utiifu kwa viongozi hata kwa mambo ya kipuuzi, usengenyaji, wivu, ulaghai, ukosefu wa nidhamu, maadili, kutokuwa na miiko ya chama, uchonganishi na mengineyo mengi ya kuchefua. Mambo hayo chini ya usimamizi wa baadhi ya watu yameguka kuwa ndio itikadi ya chama na malengo makuu ya chama na sio sera na itikadi lasmi kama ndio misingi ya kuendesha chama.
Hakika ombi langu ni ujio wa mchakato wa katiba mpya kwa kuwa huo ndio utakuwa mwalobaini wa vyama vya siasa,kwa kuwa tuendako dunia ya watu ambao Integrity [If you have integrity, you are honest and firm in your moral principles.] watakuwa na nafasi kubwa sana na heshima kubwa sana kwenye jamii kwa kuwa wako genuine na wanakubalika kwenye jamii.
Hivyo vyama vya kisiasa itavibidi vifuate itikadi zao lasmi ili viwe na mlengo halisi na kuibua changamoto,kuwa mwanachama wake au mfuasi wake au mkeleketwa wake ni lazima awe na itikadi ya chama chake kama ndio mwongozo wake.Hivyo kupitia ujio wa mgombea binafsi ni nafasi ya kutengeneza CONFLICT OF INTEREST kati ya vyama vya kisiasa na nafasi za watu ambao watakubalika kwenye jamii ambao au kwa namna fulani wameshindwa kufanana na haiba [Persoality] au falsafa ya vyama vyao kwa wakati huo husika, hivyo wanaamua kujitoa na kusimama kama wagombea binafsi.
Ndio kwa vyama vya siasa legelege na sio makini mfumo huo ni mwiba lakini kwa demokrasia na ujenzi wa vyama makini vyenye mlengo sahihi bado hilo la mgombea binafsi ni changamoto ndogo sana,kwani usemi ule wa kiswahili palipo na wengi hakialibiki kitu,au kidole kimoja hakivunji chawa,hivyo hofu na mashaka ya vifo vya vyama ni hadithi na utastawi na kutoa matunda mazuri kwa vyama ni ubarikio unaojisimamia kwa wazi kabisa.Tunaweza kuona kwenye Taifa kama Marekani kuna mgombea binafsi lakini daima mbio za kisiasa ndani ya Taifa hilo kubwa ni la vyama viwili vikuu navyo ni Democratic na Republican kama vile hakuna nafasi ya mgombea huru.
Tukitazama sasa gumzo la wabunge wa NCCR na CUF,wabunge hao tungekuwa na mgombea huru au binafsi hakika vyama vyao vingepata shida sana kwenye chaguzi ndogo.Lakini kwa kuwa mchakato huo wa mgombe huru hatuna basi vyama vinakuwa na vulumai na michezo kauzu kibao na ukosefu wa maadili kwa kuwa baadala ya chama kuwa ni jumuiko la watu wenye nia moja kupitia Itikadi lasmi na sera zao lasmi za chama husika inakuwa ni kusanyiko la kundi au vikundi vya watu wenye malengo binafsi na si malengo ya jumuiya kama chama.
Hakika palipo na heri na majaliwa wanajf tuliangalie hili la mgombea binafsi kama kitu cha msingi kitakacholeta mabolesho kwenye vyama vya kisiasa.Tunaweza kujifunza kupitia malumbano yanayoendelea sasa kati ya NCCR,CUF, Mahakama,Msajiliwa vyama Tendwa,Wananchi ambao ndio waajili wa Mbunge, Vyombo vya habari, Bunge na Serikali kwa upande wao.Ni changamoto nzuri na mpambano mzuri wa kukuza maitaji ya mfum huo wa mgombe binafsi.
Nawasilisha