Mchakato wa kuandika katiba ya JMT umekamilika na aliyekuwa mwenyekiti wa BMK aliikabidhi katiba hiyo iliyopendekezwa kwa marais wetu jana katika sherehe iliyofanyika uwanja wa Jamhuri pale Dodoma.
Binafsi sijapata fursa ya kuipitia katiba hiyo iliyopendekezwa ila nimesikia kuwa mgombea binafsi ameruhusiwa katika katiba hiyo. Pamoja na kuruhusiwa kwa mgombea binafsi inadaiwa pia kuwa masharti yaliyotolewa ni sawa na kuzuia uwepo wa huyo mgombea binafsi.
Sasa kwa yeyote aliyepata kuipitia katiba hiyo,tafadhali ninaomba ainishe hivyo vigezo/mashrti yaliyotolewa ili mtu aweze kukidhi kusimama kama mgombea binafsi katika chaguzi zijazo.