Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Watu wote CCM inataka iwafungie kwenye CAGE kama makinda ya ndege. Wakiruhusu mgombea binafsi makinda yatapata UHURU.

Sehemu pekee iliyokuwa inawapa UNAFUU ni KUHAMIA vyama vya UPINZANI. Na kwenyewe CCM wanataka kuziba, kwamba ukihamia chama kingine ukae miaka 2 ndio UGOMBEE
 
Kamundu,
Wakati huo hicho kipengele kilikuwa kinataka ku control watu kama Mzee Mengi. Sijajua kwa sasa zuio linamlenga nani.
 
Kamundu,
Ni wazo zuri but kumbuka vyama vya Siasa especially the ruling party hawana maslahi na Hilo, wanapenda kuendelea kuwa na absolute power na ndio maana ni Ngumu kwao kubadilisha katiba kuruhusu mgombea binafsi, Serikali nyingi duniani zinapenda kuwa na control dhidi ya Bunge for safety.

Can you imagine Una Serikali ambayo haina control ya kinachoendelea Bungeni?! Impeachment zinaweza kufanyika kirahisi Sana. So wagombea wengi wanakuwa controlled na vyama vyao ili wasilete chokochoko .
 
Enzi ya Nyerere miaka ya 1960's ilikua inaruhusiwa baadae ikaja ikafutwa

Chief Sarwat aliwahi kugombea ubunge wa jimbo la Mbulu kama mgombea binafsi na akashinda akawa mbung asie na chama for 5 years
 
Kamundu,
Yaani unaruhusiwa kumpigia mtu kura hata kama huna chama ila kupigiwa kura lazima uwe na chama. Siyo sawa kabisa.
 
Kamundu,
Mkuu Kamundu, hii ni hoja ya msingi sana, Mchungaji Mtikila aliipigania sana hadi anaingia kaburini. Imezungumziwa sana humu, na mimi pia niliwahi izungumzia.


P
 
Kama vyama vya siasa vinapigwa vita kila uchwao tena vipo kwa mujibu wa katiba hao wagombea binafsi wataishia magerezani maana peoples power hawana na rahisi pengine kutishika na vitisho vya watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za saizi

Nilipenda kuuliza kwanin Tanzania wasiweke ruhusa ya mgombea huru bila ya kuwa chini ya chama flani maana MTU anachaguliwa na watu na pale chama kikimfukuza anakua ana cheo husika uko alichaguliwa na watu na sio chama ??
 
Kama vyama vinafutwa kwa makusudi sembuse wagombea binafsi hill lilifutwa nyerere alikuwa hai
 
Hiyo sheria itakaribisha vijakazi wa mabeberu
Itaondoa utamaduni wa Nchi
 
Mgombea binafsi ni hatari sana kwa usalama wa Nchi

Hata huko walikoendelea wagombea binafsi hawaaminiki
Kama vyama vinafutwa kwa makusudi sembuse wagombea binafsi hill lilifutwa nyerere alikuwa hai
 
on point but waweke sheria kama mbunge au yoyote atakaye fukuzwa chama basis atabaki kweny kitu chake adi mda utakapo isha
Hiyo sheria itakaribisha vijakazi wa mabeberu
Itaondoa utamaduni wa Nchi
 
Back
Top Bottom