rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Mgombea binafsi alisharuhusiwa na mahakama ya afrika ambayo Mch. Mtikila alifungua kesi na akashinda kwa sababu hiyo serikali ilitakiwa ianze mchakato wa kurekebisha vifungu vya katiba ila serikali ilifanya ujanja kwa kisingizio cha kuwepo rasimu ya katiba ambayo ilikuwa imeingiza na kipengele cha wagombea binafsi baada ya mchakato wa katiba kuvurugwa serikali imekaa kimya.
Tatizo sio CCM wala vyama vya upinzani wanaotaka wagombea binafsi ndio maana tumeona hakuna kelele yoyote toka kwa vyama vyote kwani mgombea binafsi akiruhusiwa ndio mwanzo wa vyama vingi kufa kwani karibia vyote vinaendeshwa kwa njia zinazofanana na mtu akitaka kugombea hata kama hakubaliani na vyama hivyo inabidi ajiunge navyo