Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya Muungano.

Kama kichwa kinavyosema. Naomba kuelimishwa kuhusu faida ya mgombea binafsi, hasara zake na status ya jambo hilo hapa Tanzania.

Mchungaji Mtikila alilipigania sana hili suala, napenda kujua vita yake iliishia wapi hadi mauti yanamkuta.
Pia napenda kujua athari za jambo hilo kwa vyama vya siasa.

Cc MALCOM LUMUMBA
 
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Paskali
 
mkuu unaweza kunisaidi ilani ya mama samia tofauti na ilani ya magufuli, navyofahamu wote wanatumia ilani ya ccm na mama alipoingia ccm haikuleta ilani nyingine tofauti na ile waliyotumia 2020.
Mang'ula aliwahi kuwajibu wale waliotaka bandari ya bagamoyo kuwa ilani yao ilisema wajenge gati na sio bandari.
Kwa kifupi ilani inayotumika ni ya awamu ya tano.
 
Kwa wale msiojua, kile kilichonikuta kwenye lile jambo langu, kinatikana na ubatili huu niliuzungumza hapa!. Kuna uwezekana mtu una jambo lako unalitaka, unalipania sana la Mungu anakunyima, unalikosa, unakubali matokeo kwasababu waliochaguliwa wamekupita sifa, ila kuumia kulikosa jambo lako unakuwa umeumia!. Kumbe kuna uwezekano, majanga mengine sio majanga, ni mapito!. Unapitishwa kwenye mapito ya majanga huku unachapwa mijeledi, kumbe ni kwa kupigwa kwako, unapigwa ili wengine waponywe, hivyo majanga hayo yakawa ni a blessing in disguise!.

Mungu Nisaidie Niyaweze yote katika YEYE anitiaye nguvu!.
P.
 
Katika kuadhimisha Nyerere Day, tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kulitekeleza hili!.
Rais Samia akiamua, anapaswa kuwapuuza wahafidhina wa CCM, na kulitekeleza hili!.
Happy Nyerere Day!

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…