Waziri2025
Senior Member
- Sep 2, 2019
- 148
- 379
Baadhi ya wagombea Ubunge wa Kura za Maoni CCM katika jimbo la Arusha mjini wamefichua mazito siri ya Ushindi wa mgombea mwenzao Mrisho Gambo aliyepata kura 333 na kufuatiwa na Philemon Mollel aliyepata kura 68 kuwa alilipia ukumbi wa uchaguzi na kulala katika hotel ya Mt.Meru karibu na ukumbi wa uchaguzi siku moja kabla ya uchaguzi ili kujijengea mazingira mazuri ya kukutana na wajumbe.
Makada hao wa CCM ambao waligombea nafasi hiyo, RAYSON NGOWI NA VICTOR NJAU wameamua kujilipua kwa kudai kwamba hawezi kuvumilia kuona demokrasia ikibakwa na wenye fedha kwa uroho wa madaraka jambo hilo ninapoteza heshima ya CCM na kuwapa nguvu wapinzani.
Siku chache baada ya kura za maoni kupitia hapa nchini za kupata waakilishi wa ubunge katika majimbo makada wa chama chamapinduzi CCM Mkoa wa Arusha wamelalamikia kitendo cha wajumbe kumpa kura za ndio aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kufanikiwa kuzoa kura za kishindo .
Makada hao wamesema wajumbe wa mkutano Mkuu maalum wamepingana na kauli ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa John pombe Magufuli aliyemtoa kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa Mrisho Gambo baada ya kupingana na watendaji wenzake akiwemo Mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Arusha Maulid Madeni
"CCM ilipewa ukumbi bure na AICC kufanya mkutano wa kura za Maoni lakini ulibadilishwa ghafla na kupelekwa Mount Meru iweje CCM ikachukue ukumbi wa gharama kubwa za mamilioni ya fedha hii nia ajabu"
"Kilichonisukuma hapa ni uzalendo wa nchi yangu na chama changu ninapogundua haki imekiukwa siwezi kuvumilia nikiwa kama mtumishi wa mungu...
"Mgombea Mwenzetu alipata namba siku moja kabla ya uchaguzi, mgombea Mwenzetu kutoa usafiri kwa wajumbe, kulipia watu chai, kulipia ukumbi, kulala hoteli tuliofanyia ukumbi na kulala chumba namba 403 ushahidi tunao, mgombea Mwenzetu kupanga safu ya madiwani, Rais alisema uchaguzi lazima uwe huru matokeo yake hili jimbo litaenda upinzani" Alisema Ngowi.