Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika hali ya kushangaza, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameanza kufanya siasa za ajabu sana kwenye uchaguzi mkuu huu. Wameanza kutumia watoto wadogo kisiasa.
Watoto ambao walihitaji kulindwa na serikali dhidi ya kushiriki matendo wasiyokuwa na ufahamu nayo kama vile siasa za kampeni na manipuations za kisiasa, inashangaza kuona kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa kikitumia watoto kwenye mikutano yake.
Tumeona, Mikutano ya Mgombea uraisi wa CCM ndugu Magufuli ikisheheni watoto wadogo.
Na wananchi wanalalamika badala ya watoto wao kwenda shule kusoma, wanaambiwa wao na walimu wao waahudhurie mikutano ya CCM.
Inashangaza zaidi, Majuzi hapa tumefiwa na rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa hakuna agizo lolote kutoka serikalini la kutangazia watoto wasiende shule hata wale wa Dar ili wakamuage, lakini shule kwenye mikutano ya mgombea wa CCM huko Mwanza tunaelezwa kuwa zimesitisha masomo na kuwataka wanafunzi na walimu waende kwenye kampeni za Magufuli. Hii ni ajabu sana.
Hapa Chini ni video na picha za watoto kwenye mikutano ya CCM