Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini, Tulia Ackson afanya kampeni na watoto wadogo

Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini, Tulia Ackson afanya kampeni na watoto wadogo

Ukisikia Simba hula majani akizidwa kwa njaa, basi ndio hiki kinachofanywa na CCM hii ya leo!!
 
Wanawajenga kuipenda CCM tangy utotoni. Hata wakiwa wakubwa huwaambii kitu juu ya CCM. Magwanda endeleeni kushangaa tu
Lakini ukiwa ni binadamu mtu mzima mwenye akili timamu na kwa kuzingatia makubaliano ya UN ya haki za mtoto, utawaacha watoto wawe watoto, wa-enjoy utoto wao, michezo yao, shule zao na sio kuwalisha pumba za kisiasa kabla ya wakati wao. Ma-CCM m wakatili hata kwa watoto wa wenzenu.
 
Yaani CCM pamoja na policcm, tumeccm, mahakamaccm, bungeccm, tissccm bado mmeongeza na watoto wa shule ccm kweli mko maji ya shingo Mpaka mkataka kuchukua na kifimbo cha baba wa taifa kwa lazima nyinyi mnatafuta laana , Kama mlivyopanga mlazimisha Bibi wa watu aje kwenye mkutano wenu wa kijani kibichi.
 
watoto wadogo kama hao wanapaswa kua shule, hao wanafanya nini kwenye mikutano ya siasa maji taka
 
Tulia angeenda Kugombea kwao huko Rungwe angepata jshindi mkubwa sana wa kishindo.

Nani amemdanganya huyu dada?

Kwa nini CCM hawapendi Amani?

Sugu ni Rais wa Mbeya.
 
Katika hali ya kushangaza, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi wameanza kufanya siasa za ajabu sana kwenye uchaguzi mkuu huu. Wameanza kutumia watoto wadogo kisiasa.

Watoto ambao walihitaji kulindwa na serikali dhidi ya kushiriki matendo wasiyokuwa na ufahamu nayo kama vile siasa za kampeni na manipuations za kisiasa, inashangaza kuona kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa kikitumia watoto kwenye mikutano yake.

Tumeona, Mikutano ya Mgombea uraisi wa CCM ndugu Magufuli ikisheheni watoto wadogo.

Na wananchi wanalalamika badala ya watoto wao kwenda shule kusoma, wanaambiwa wao na walimu wao waahudhurie mikutano ya CCM.

Inashangaza zaidi, Majuzi hapa tumefiwa na rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa hakuna agizo lolote kutoka serikalini la kutangazia watoto wasiende shule hata wale wa Dar ili wakamuage, lakini shule kwenye mikutano ya mgombea wa CCM huko Mwanza tunaelezwa kuwa zimesitisha masomo na kuwataka wanafunzi na walimu waende kwenye kampeni za Magufuli. Hii ni ajabu sana.

Hapa Chini ni video na picha za watoto kwenye mikutano ya CCM


View attachment 1562251

View attachment 1562258
Inaonyesha dhahiri sasa kuwa kifo chao CCM kimekaribia mno............

Hakika kitakuwa tarehe 28/10/2020
 
Back
Top Bottom