Uchaguzi 2020 Mgombea Udiwani CHADEMA Kata ya Sandari Temeke akatwakatwa mapanga na kupokonywa fomu

Uchaguzi 2020 Mgombea Udiwani CHADEMA Kata ya Sandari Temeke akatwakatwa mapanga na kupokonywa fomu

Imefika wakati tuache kuuchekea huu uhuni na wananchi wawalinde wagombea, hivi kweli unaweza kubali mwili wako udhuriwe kwa kiasi icho ubaki na kilema sababu ya udiwani?? Tuache kuongea matapishi, Muda mwingine tutumie vichwa kufikiri kabla ya kutamka chochote badala ya kufikiri kwa kutumia tumbo..
 
Ndio kata ninayoishi kwasasa.
Uhuni huu bila shaka umefanywa na wale vijana wasio na kazi wa CCM.
 
Huijui siasa ndo maana unaongea upupu mkuu..

Marekani imeua Marais wake wawil livelive na watu wanadaiwa wasiojulikana.

Mtu Kama JF. Kennedy na Abraham linkolin.
Siasa Ni Mchezo mchafu kote usitake kuichukulia marekan Kama MUNGU wako nakwenyewe kuna mapuuza Sana tu.

Uko sahihi kwamba siasa ni mchezo mchafu, kama ni hivyo yale maombi ya kuombea amani ni ya nini wakati inafahamika kuwa siasa ni mchezo mchafu?
 
Kule Moshi msimamizi wa uchaguzi alitoa fomu na risiti tofauti kwa wagombea wa upinzani na zile za wagombea wa ccm. Nini matokeo yake. Ubungo mgombea feki wa cdm alipewa fomu kabla hata chama hakijamteua mgombea. Ni nini hii kitu!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani kuna haja ya kupunguza maslahi serikali inayotoa kwa wanasiasa.
 
Acha kuunga mkono uhuni na ushenzi, siasa siyo chafu ila wanasiasa wahuni ndiyo wachafu.
Hivi umetumia kichwa kunielewa nilichokiandika au umetumia makalio kuelewa. Ni Wapi umeona nimeunga mkono?
 
Narudia Tena siasa Ni Mchezo mchafu. Ukiamua kuingia huko Basi jua muda wote uhai wako unahitajika kwa mtu au watu Fulani.

Siasa siyo taasisi ya dini Bali Ni uwanja wa mapambano Ila zisitufanye tuumizane na kuuana Sisi kwa Sisi.
Kuna maisha nje ya siasa wakuu.
Weka bunduki chini tujibishane kwa hoja.
 
Katika hali ya kushangaza mgombea udiwani kupitia chama cha CHADEMA amevamiwa na watu wasiojulikana na kumkatakata na mapanga na hivi sasa yupo hospitali kupata huduma ya kwanza.

Jamani kama watanzania tunaelekea wapi? Je ccm imeshindwa kuongoza nchi hii kiasi kwamba sasa inabidi itumike nguvu kuzuia watanzania?

Haya tuendelee, mwisho utafika.View attachment 1547226


Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Katika hali ya kushangaza mgombea udiwani kupitia chama cha CHADEMA amevamiwa na watu wasiojulikana na kumkatakata na mapanga na hivi sasa yupo hospitali kupata huduma ya kwanza.

Jamani kama watanzania tunaelekea wapi? Je ccm imeshindwa kuongoza nchi hii kiasi kwamba sasa inabidi itumike nguvu kuzuia watanzania?

Haya tuendelee, mwisho utafika.View attachment 1547226
Ndo hapo nashidwa kuwaelewa viongozi wa dini, hili la kuua na kujerui awalikemei ila mtu akija kulalamika kuwa hatuta kubari kuvumiria matukio haya ya kinyama utaona wanalalanika shida eti wajengewe makanisa na misikiti. Yesu alisema NYUMBA YA BABA YANGO SIYO PANGO LA WANYANG'ANYI

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
NEC ingesema hata Kama umevamiwa umeporwa fomu wanaruhusu aliyeporwa kujaza upya Tena nadhani huu uhuni ungeisha
 
ccm ni chama cha kishetani
Huwa nasema kila siku ccm ni mashetani sana.

Hawana tena hoja za kupeleka kwa wananchi wanachokifanya sasa hivi ni kuhakikisha wananchi hawana chaguo jingine zaidi ya mwanaccm tu
 
NEC ingesema hata Kama umevamiwa umeporwa fomu wanaruhusu aliyeporwa kujaza upya Tena nadhani huu uhuni ungeisha
Tume ndiyo inaratibu huu uhuni na huyo judge wa tume naye ni mhuni tu kama wahuni wengine wanaomzunguka
 
Ujinga tu,,unajua kabisa saa za kurudisha fomu au kuchukua matatizo ndo huwa yanakuwepo na unatakiwa usimange mange na ujigiche kwenye handaki ambalo hata bomu la nyuklia haliwezi kupenya,,ni uzembe wake
 
Back
Top Bottom