Uchaguzi 2020 Mgombea Udiwani CHADEMA Kata ya Sandari Temeke akatwakatwa mapanga na kupokonywa fomu

Siasa za hovyo na za kihuni sana hizi.
 
Imefika wakati tuache kuuchekea huu uhuni na wananchi wawalinde wagombea, hivi kweli unaweza kubali mwili wako udhuriwe kwa kiasi icho ubaki na kilema sababu ya udiwani?? Tuache kuongea matapishi, Muda mwingine tutumie vichwa kufikiri kabla ya kutamka chochote badala ya kufikiri kwa kutumia tumbo..
 
Ndio kata ninayoishi kwasasa.
Uhuni huu bila shaka umefanywa na wale vijana wasio na kazi wa CCM.
 

Uko sahihi kwamba siasa ni mchezo mchafu, kama ni hivyo yale maombi ya kuombea amani ni ya nini wakati inafahamika kuwa siasa ni mchezo mchafu?
 
“Taarifa mbaya tulizopokea muda huu ni kwamba mgombea Udiwani Kata ya Sandari kwenye Jimbo letu la Temeke amevamiwa muda huu, akapigwa mapanga na kunyang'anywa form ya Ugombea. Viongozi wa jimbo wanafuatilia.”

Ccm ina wenywe, wenyewe ndio hao wazee wa mapanga shaaaaa
 
Kule Moshi msimamizi wa uchaguzi alitoa fomu na risiti tofauti kwa wagombea wa upinzani na zile za wagombea wa ccm. Nini matokeo yake. Ubungo mgombea feki wa cdm alipewa fomu kabla hata chama hakijamteua mgombea. Ni nini hii kitu!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani kuna haja ya kupunguza maslahi serikali inayotoa kwa wanasiasa.
 
Acha kuunga mkono uhuni na ushenzi, siasa siyo chafu ila wanasiasa wahuni ndiyo wachafu.
Hivi umetumia kichwa kunielewa nilichokiandika au umetumia makalio kuelewa. Ni Wapi umeona nimeunga mkono?
 
Weka bunduki chini tujibishane kwa hoja.
 


Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Ndo hapo nashidwa kuwaelewa viongozi wa dini, hili la kuua na kujerui awalikemei ila mtu akija kulalamika kuwa hatuta kubari kuvumiria matukio haya ya kinyama utaona wanalalanika shida eti wajengewe makanisa na misikiti. Yesu alisema NYUMBA YA BABA YANGO SIYO PANGO LA WANYANG'ANYI

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
NEC ingesema hata Kama umevamiwa umeporwa fomu wanaruhusu aliyeporwa kujaza upya Tena nadhani huu uhuni ungeisha
 
ccm ni chama cha kishetani
Huwa nasema kila siku ccm ni mashetani sana.

Hawana tena hoja za kupeleka kwa wananchi wanachokifanya sasa hivi ni kuhakikisha wananchi hawana chaguo jingine zaidi ya mwanaccm tu
 
NEC ingesema hata Kama umevamiwa umeporwa fomu wanaruhusu aliyeporwa kujaza upya Tena nadhani huu uhuni ungeisha
Tume ndiyo inaratibu huu uhuni na huyo judge wa tume naye ni mhuni tu kama wahuni wengine wanaomzunguka
 
Ujinga tu,,unajua kabisa saa za kurudisha fomu au kuchukua matatizo ndo huwa yanakuwepo na unatakiwa usimange mange na ujigiche kwenye handaki ambalo hata bomu la nyuklia haliwezi kupenya,,ni uzembe wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…