Uchaguzi 2020 Mgombea urais anatoa vitisho kwa wananchi, NEC shughulikieni hilo

Uchaguzi 2020 Mgombea urais anatoa vitisho kwa wananchi, NEC shughulikieni hilo

Bora wapinzani ni mbuzi lakini wanafanya mambo kama binadamu kuliko nyinyi binadamu lakini mnaishi na kuwaza kama mbuzi.
Andamana sasa mbuzi wakushikishe adabu
 
Tatizo sio kumpumzisha, tatizo ni tukimpumzisha tunampa nani?
KWA KWELI MUDA WA KUMPUMZISHA MAGUFULI UNAKARIBIA KWA KASI SANA.

Kauli gani hizi za kibaguzi? Kwani maendeleo anayaleta kutoka hela za mfukoni mwake?
Kwani wananchi wanaochagua upinzani hawalipi kodi kwa ajili ya kupata maendeleo yao bila kujali wamemchagua nani?

Inasikitisha sana kuona mtu wa kauli kama hii eti ndiye Rais wa nchi. Hajitambui kabisa
 
Think like a real Man;Hiyo haki ya kuwapangia wengine cha kufanya umeitoa wap?
Sipingani na chama chochote wala sina chama chochote

Umeshawahi kujiuliza tukishaipora nchi Ccm tunampa nani?
 
Sipingani na chama chochote wala sina chama chochote

Umeshawahi kujiuliza tukishaipora nchi Ccm tunampa nani?
Swali gani sasa hili ndugu yangu? au ndo kujaza server za Jf kwenyewe?
 
1599466582949.png
 
Q
Haya nayo yatapita. Mungu mkubwa miaka mitano sio mingi kiviile....
Yaani mitano tena?Tutakuwa tumefariki sote kwa mateso,alisema ataongeza zaidi maana hii mitano ya kwanza zilikuwa ni rasharasha.Tutalimia meno hakika.
 
Ukweli ndio huo.. hakuna wa upinzani atafanya hata 2% ambayo Magufuli amefanya hadi sekunde hii..

Na sijaona ni kitisho yeye kwani kushika panga n.k au maiki??? bali ukweli.kausema.. yeye ni Jembe.. kwamba yeye ndiye atawapa watakayo.. Munaweweseka kuita kitisho... eeeeh hao wenu maneno yao sio vitisho pia!!!!

#Magufulitanotena
Magufuli 2020 💯
Hii ni kauli ya hatari sana, anapaswa atambue kuwa yeye ni rais wa waislamu, wakristo, Hindu, wapagani, wenye vyama na wasio na vyama, waliomchagua na waliompinga nk . Na ukishachaguliwa una angalia nchi kwa ujumla wake, na yeye anatunzwa yeye na familia yake na kodi za watanzania wote , hata wale waliompinga/wanaompinga. Haiwezekani ukasema nyama ya nguruwe haramuhalafu mchuzi wake unakunywa,
Kama Bunda hawapaswi kuletewa maendeleo, basi hata kodi zinazotoka Bunda zimeharamika
 
Ukweli ndio huo.. hakuna wa upinzani atafanya hata 2% ambayo Magufuli amefanya hadi sekunde hii..

Na sijaona ni kitisho yeye kwani kushika panga n.k au maiki??? bali ukweli.kausema.. yeye ni Jembe.. kwamba yeye ndiye atawapa watakayo.. Munaweweseka kuita kitisho... eeeeh hao wenu maneno yao sio vitisho pia!!!!

#Magufulitanotena
Magufuli 2020 💯
Mbona unaandika huku ukitokwa na jasho na vishuzi vya jumlajumla kwa mbali? Si mlisema mna mbinu 7000 na mshatumia 1? Kwani shida nini hadi ayaongee kwenye kadamnasi yale ambayo huyafanya sirini?
 
Ha!aaaaaaaaaaaa Haaaaaaaaaaah Duuuuuuuu. Siasa Buana
 
Sasa kuwaambia watu ukweli ni kuwatisha?
Wewe uliyeandika hicho kichwa cha habari huna upeo wa kutosha wa kuchanganua mambo. Na hujui maana ya uhuru na haki. "Uchaguzi huu utakuwa HURU na HAKI" na Chama Cha Mapinduzi kitapita kwa kishindo.

Raisi Dr. John Pombe Magufuli ni mkweli kabisa. Kawaambia ukweli, ukweli huo utawaweka Huru. Wafanye maamuzi mazuri Wasijepata shida wakasema hawakuambiwa.
 
Dada wangu Mzee wetu alivyojichafua toilet paper tu haitoshi hata kama ni bunda zima la karatasi lakini. Hapa ni kumrudisha Dar au Dodoma na kumuosha kwa maji pipa nzima.
Apewe mtu wa kumkontrol hata kwa kumnyang'anya mic.
Tukimuacha nchi ina kwenda upinzani chadema. Mpaka sasa chadema wanamvuto kuwasikiliza.
Turufu ya miradi imesikika sana kama wimbo wa taifa maana ilikuwa ndio sala ya bwana kwa miaka mitano.
Waje watu watakaoshawishi kuwapo kwa Uhuru wa kidemokrasia, amani na ustawi wa watu
Hahahaaaaaahaaaa eti "Mkiamua"

Amueni sasa tuone.

Bado hamjafanya maamuzi.
Afadhali mzee Sipunda anaongea point kuliko huyo mpiga jitaa, hana cha kusema na ndio maana kawafukuza waandishi wa habari. Nadhani hakuamka na cha kuongea au alikuwa hajapiga mtungi apate idea.
 
Ikiwa mwenyewe amesema hawatishi sasa ni kama hadhari tu sasa unataka nini zaidi
 
Back
Top Bottom