The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Wenye ndoto za kuoa na Mahali ni kipengele baasi tumsikilize huyu mgombea wa CCK
==
CHAMA cha Kijamii (CCK) kimewataka Watanzania, hususan vijana, kukiamini na kukipa ridhaa ya kuongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Chama hicho kimeahidi kwamba kikipewa dhamana ya kuunda serikali, kitahakikisha kinawalipia vijana mahari, kuondoa kabisa mikopo yenye masharti magumu na isiyowafaidi wananchi (“mikopo ya kausha damu”), na kupambana na tatizo la wananchi kulala njaa.
Akizungumza katika viwanja vya Kabwe, Jijini Mbeya, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCK, David Mwaijojele, pamoja na mgombea mwenza wake Masudi Abdalah, wamewaomba wananchi kuwachagua ili kuleta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa upande wake, mgombea mwenza Masudi Abdalah alisema chama hicho kikipewa nafasi ya kuunda serikali, kitaondoa mikopo isiyokuwa na tija kwa wananchi na kuhakikisha vijana wanaotaka kuoa wanapatiwa msaada wa mahari.
Naye mgombea udiwani wa kata ya Mbalizi Road, Jijini Mbeya, kupitia CCK, Endrick Joseph, alisema mabadiliko ya kweli yanapatikana ndani ya chama hicho, huku baadhi ya wananchi wakionesha mtazamo chanya kuhusu sera na ahadi zinazotolewa na wagombea wa chama hicho.