GE2025 Mgombea Urais CCK: Serikali yangu itagharamia mishahara wahudumu wa Bar

GE2025 Mgombea Urais CCK: Serikali yangu itagharamia mishahara wahudumu wa Bar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,966
Reaction score
26,220
Sasa kweli eti hii nayo ni sera ya chama kinachotaka kuchukua dola.
Hivi wapo serious kweli hawa watu,walijiandaa kweli na huu uchaguzi au walikurupushwa tu?

----
Chama Cha Kijamii (CCK), kimezindua kampeni zake katika Jiji la Dodoma, ambapo Mgombea Urais, kupitia chama hicho Ndg. David Mwaijojele, amesema endapo atachaguliwa, katika kiti hicho serikali yake itagharamia gharama zote za matibabu kwa kila raia, italipa mishahara wahudumu wa baa, na wafanyakazi wa majumbani pamoja na kutoa huduma mbalimbali zitakazowezesha wananchi wa hali ya chini kujikwamua kiuchumi.

 
Kama wanavyowabeba watu kwenye maroli na treni kwenda kujaza mikutano yao ya Kampeni

Basi wajiandae kufanya hivyo wakati wa kupiga kura

Otherwise, wenye akili watabaki nyumbani siku hiyo wakicheza hata na Watoto wao kuliko kwenda kupoteza muda wao
 
Ni huzuni mtu mzima kuongea point kama huu kwenye maswala ya muhimu ya kitaifa.Ni kweli Tanzania uelewa wa wanasiasa umeshuka kiasi hiki?
 
Kwa mujibu wa Chama Cha Kijamii (CCK), kupitia kampeni za Mgombea Urais, Ndg. David Mwaijojele, kimesema serikali yao itagharamia gharama zote za matibabu kwa kila raia,huku akisepa watalipa mishahara wahudumu wa baa, na wafanyakazi wa majumbani

Amesema hiyo ni pamoja na kuwa serikali yao ni ya kijamii na hivyo watahakikisha keki ya nchi italiwa na wote na wananchi wale wanenepe


 
Hivi vyama vingine ni upigaji wa ruzuku
 
Back
Top Bottom