Mgombea Urais CCM 2015: Vita kali yatabiriwa kati ya Wasira, Lowassa na Nchimbi

Mgombea Urais CCM 2015: Vita kali yatabiriwa kati ya Wasira, Lowassa na Nchimbi

Nchimbi ama Wassira akiwa raisi wa nchi hii nitatorokea Malawi..... Akili ndogo kuongoza kubwa, tutakuwa na hali mbaya zaidi ya ilivyo sasa,kile kiti si cha kufanya majaribio,tulikosea 2010 tukikosea tena 2015 tumekwishaaa!!
 
Point yake ni sahihi, kaka Sisiemu bado yeyote kati ya Wassira, Nchimbi, Lowassa, Sitta au Membe anaweza kuwa kiongozi wa Nchi hii..Bado Mgombea wa Urais akitoka CCM atashinda sababu wapiga kura wengi nje ya miji hawawezi kumpa Mbowe, Dr. Slaa wala Tundu Lissu kwa mfumo Uliyopo...ndio maana mbio ni ndani ya CCM...akipatikana huyo, pesa zote zitakuwa nyuma ya huyo alafu atashinda...Life Goes on!

Kwa hilo inaweza ikawezekana. Ila kaka kama na wewe ni mpenda mageuzi usipende kufa moyo mapema. Amini kila kitu kinawezekana usiamini kuwa kila kitu ni kigumu. Mageuzi yanawezekana pamoja tukiwa mimi na wewe. Come on boy...!!
 
hakuna ubishi kuwa membe ameamua kunyoosha mikono mimi kwa uzoefu wangu ndani ya siasa za ccm mtu mwenye nguvu kubwa ndani ya ccm kwa miezi 16 iliyobaki hadi kikwete kuondoka madarakani ni edward ngoyai lowassa pia kumbukeni nchimbi ni mfuasi mwaminifu kwa lowassa na ni wazri mkuu mtarajiwa wa lowassa akiingia mjengoni na ikumbukwe lowassa alimsaidia sana nchimbi kuushika uongozi wa umoja wa vijana uvccm...

no permanent friends in politics, only permanent interest...kikwete atampiga chini lowassa sababu lowassa ni mtu wa kisasi hawezi kuwa sure na leadership yake..kama sitta aliyopigwa mweleka uspika same for lowassa...no permanent friends in politics, urafiki wa mwaka 47 wa nchimbi na lowassa...jk will give tz a suprise candidate or compromising candidate...stay tune theory ya urafiki haipo na lowassa might not be
 
Duh...kumbe hata Wassira na Nchimbi nao presidential materials?
 
Analysis ya kampaign! Mbona hao waliotajwa woote majanga tuu! We want new idea! Nchimbi ni new generation na old idea!
 
Mungu wangu, hata Nchimbi naye anaota kuwa Rais wa nchi hii? Pole sana Tanzania. Wassira by default hana uwezo wa kuongoza nchi hii ije mvua lije jua.
 
Membe ametangaza lini kwamba angegombea na ametangaza lini kwamba hata gombea? Au hii ni mbinu ya mahasimu wake kumwondoa katika kutajwatajwa? Mbona kazi wanayo hao wanaopingana naye? Mbona kuna taarifa kwamba ameshaoteshwa na sasa anapiga jalamba? Kaazi kweli kweli kuamini yupi anasema ukweli na yupi anapiga ushabiki JF
 
Mungu wangu, hata Nchimbi naye anaota kuwa Rais wa nchi hii? Pole sana Tanzania. Wassira by default hana uwezo wa kuongoza nchi hii ije mvua lije jua.

by default hana uwezo? au by default ndio de facto nominee? sijakuelewa! default huwa ni sure thing...Lolote linawezekana TZ
 
Hatma ya Urais wa nchi hii ipo mikononi mwa Mungu na kwenye kura za Watanzania na wala si mieleka na hivi vikumbo wanavyopigana sasa
 
Alhamisi, Aprili 18, 2013 07:41


MPAMBANO WA MGOMBEA URAIS CCM 2015
*Vita kali yatabiriwa kati ya Wasira, Lowassa na Nchimbi
*Mpango wa kukatwa jina la Lowassa waunganisha makundi


KATIKA hali inayooshesha kupamba moto kwa harakati za kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), makundi ndani ya chama hicho yameanza kuungana.

Mbali ya kuungana kwa makundi, pia wale wote wanaotajwa kuwania kuteuliwa, macho na nyoyo zao vimeelekezwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ambaye nguvu aliyonayo ndani ya vikao vya uteuzi inatarajiwa kutumika kumpata mgombea urais.

Ingawaje viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakipinga mjadala kuhusu mgombea urais au Rais ajaye ndani ya chama hicho kikongwe nchini, lakini mjadala huo unatajwa kufunika hata ile mijadala muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Uchunguzi wa Rai umebaini kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ameanza ‘kurudisha majeshi’, na anatajwa kumuunga mkono Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye anatajwa kuwa ‘safi’, mtu asiye na kikwazo mbele ya Rais Kikwete.

“Hali inavyoonekana sasa, Membe anaelekea kuungana na kambi ya Dk. Nchimbi, na si yeye pekee, wale wote ambao wanampinga Lowassa lakini wanajua hawana kura ndani ya CCM, wanaanza kumuunga mkono Nchimbi.

“Lengo kubwa hapa ni kutengeneza mgombea mmoja mwenye nguvu kubwa ili kumkabili Lowassa ambaye anatajwa kuwa na nguvu kubwa zaidi ndani ya chama katika ngazi zote.

“Katika hao, yumo Waziri Samuel Sitta, Dk. Harrison Mwakyembe na watu wao, lakini vile vile wanasahau uhusiano mzuri na kuheshimiana kati ya Lowassa na Dk. Nchimbi.

“Pia tetesi za kuwapo mpango wa kulikata jina la Lowassa katika ngazi ya Kamati Kuu lisirudishwe kwenye Mkutano Mkuu ambako anadaiwa kukubalika kuliko wagombea wengine, kunatajwa kuwa moja ya sababu za makundi kuungana,” alisema mchambuzi mmoja wa mambo ya siasa nchini.

Mgombea mwingine anayetajwa kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM 2015, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira,
ambaye tofauti na wagombea wengine, yeye hana kundi wala makundi.

Kutokana na kutokuwa na makundi, wachunguzi wa mambo wanasema haitakuwa rahisi jina lake kukwama katika ngazi ya Kamati Kuu, hivyo uwezekano wa jina lake kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu kuchuana na wagombea wengine ni mkubwa.

“Huyu Mzee ana advantage moja kubwa, Kanda ya Ziwa inatajwa kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura tofauti na maeneo mengi, na ni katika kanda hiyo hiyo Lowassa anaungwa mkono sana.

“Kama CCM wataamua kulikata jina la Lowassa, kuna uwezekano mkubwa sana kwa wana-CCM waliokuwa wakimuunga mkono kuhamishia kura zao kwa Wasira, na kumchagua,” alisema mchambuzi huyo.

Wakati hali ikiwa hivyo, pia imethibitika vigogo wa chama hicho wakiwamo wale wa kundi la wanamtandao lililomwingiza Rais Kikwete madarakani mwaka 2005 hawaaminiani katika harakati za kugombea urais kupitia CCM.

Uchunguzi unaonyesha vigogo wa CCM kutoka kambi zote wamekuwa wakiendesha kampeni za chini kwa chini kwa ajili ya kujiimarisha na kisha kuweza kuteuliwa kugombea kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu 2015.

Taarifa zinaonyesha kwamba hata baadhi ya vigogo wanaosadikiwa kuwa kundi moja sasa hawaaminiani jambo ambalo linaashiria kuwa vita ya urais CCM inapamba moto siku hadi siku.

Wakati wa vikao vyake vya juu vilivyomalizika Novemba 24 mwaka jana mjini Dodoma, CCM kilipokea na kupitisha taarifa ya hali ya siasa ambayo kimsingi ilibainisha kuwa hali ya siasa ndani ya chama si shwari, kutokana baadhi ya viongozi kupigana vikumbo kuwania madaraka.

Katika taarifa hiyo, CCM kilisema chanzo kikubwa cha migawanyiko ndani ya chama hicho ni harakati za kugombea urais mwaka 2015.

Hata hivyo, wimbi hilo la urais limeendelea kutikisa kambi ya wanamtandao ambayo taarifa za ndani zinasema huenda suala la urais likaibua mtafaruku mkubwa siku zijazo, hivyo kutoa mwanya kwa kundi jingine kuibuka kidedea.

“Kuna hali ya kutoaminiana ndani ya CCM, kila kundi sasa liko mstari wa mbele kujijega ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutoa mgombea urais.

“Hata ndani ya kundi la mtandao ambalo ndilo lenye nguvu kwa sasa wakubwa hawaaminiani,” alisema mtoa habari mmoja kutoka kundi la mmoja wa kiongozi anayetajwa kutaka kuwania urais ndani ya CCM.



sura%20ya%20rai.jpg



Hata huyu babu anataka kuongoza kizazi cha dot.com? sasa haya ni mahoka
 
hata huyu babu anataka kuongoza kizazi cha dot.com? Sasa haya ni mahoka

Wasira ana miaka 67, Dr. Slaa 67, JKikwete 63, Benard Membe 61, Edward Lowassa 61, Samwel6 73, Reginald mengi 74....hapo nani sio babu...babu sambeke kafa kwa ndege hata hamsini hajafika.r.i.p to the high flyer...kizazi cha Social Media kina mababu watupu kaka
 
Wasira ana miaka 67, Dr. Slaa 67, JKikwete 63, Benard Membe 61, Edward Lowassa 61, Samwel6 73, Reginald mengi 74....hapo nani sio babu...babu sambeke kafa kwa ndege hata hamsini hajafika.r.i.p to the high flyer...kizazi cha Social Media kina mababu watupu kaka

Wasiraana zaidi ya miaka 70,sina uhakika na Mengi ila niltaka kujua tu hata Sambeke naye alikuwa ana nia ya kugombea urais?au ni kunogesha taarifa tu.
 
Tutasikia mengi sana kutoka kwa ccm mpaka 2015 ikifika tutakuwa tumesikia ya kutosha. mimi ninauhakika watafalakana hao yetu macho.
 
Atakuwa raisi nyumbani kwake. CCM wakileta ushenzi wanaipa CHADEMA nafais we subiri!
 
Back
Top Bottom