Mgombea Urais CCM 2015: Vita kali yatabiriwa kati ya Wasira, Lowassa na Nchimbi

Duh ila CCM wakimsimamisha MWIGULU NCHEMBA vichaa dema vitalia machozi kama mtoto mdogo. Rais anakwenda kuapa MIMI, MWIGULU NCHEMBA, NAAPA KUWA ...... NA MAJUKUMU YA RAIS WA JAMHURI YA MUNGANO....... MUNGU NISAIDIE. HAAAAAAAAAA. CHADEMA HAPO WANATAFUTA UCHOCHORO KAMA PANYA
 
Naona harakati za kusafisha njia ili kukabidhi nchi kwa upinzani zinaendelea.
 
kataneni tu ili msambaratike vizuri kisha tuchukue nchi kiulani kuliko tulivyotarajia
 
Nadhani umeamua kufurahisha forum!
Hakuna kitu hapo...bora awe Mulugo kuliko hayo 'mabomu'
 
Ana mke mzuri kuliko wewe!
Ana roho nzuri ajabu, uzuri wa tabia yake ni tofauti na sura yake.

Hivi mtu anayetamka hadharani anapenda chama cha upinzani kife,unadhani anazo za kutosha.Namshauri akapumzke kwao huyo mzee wa Gombe hana uwezo wa kuiongoza Tanzania tunayoitaka kwa jazba,chuki,ubinafsi na udikteta wake.
 
Hivi mtu anayetamka hadharani anapenda chama cha upinzani kife,unadhani anazo za kutosha.Namshauri akapumzke kwao huyo mzee wa Gombe hana uwezo wa kuiongoza Tanzania tunayoitaka kwa jazba,chuki,ubinafsi na udikteta wake.

Red inahusika hapo juu.
Wewe na Wasira nani anatakiwa kumpuzishwa.
 
Ninapojaribu kuyaangalia matukio na misuko suko ya Kisiasa inayoendelea ndani ya CCM pamoja na Misuguano ya Kiimani inayolisiga Taifa letu la Tanzania inanipa PICHA moja iliyo dhahiri kabisa ya Lowassa kuibuka kama a clear Presidential Candidate kutoka CCM tofauti na watu wanavyofikiria sasa.Sote tunakumbuka namna Lowassa alivyoandamwa na kadhia ya UFISADI akisukwa sukwa na baadhi ya MAADUI zake ndani ya CCM waliotumia fursa hiyo kummaliza Kisiasa lakini aliweza kupambana na majaribu yote hayo kwa UTULIVU na BUSARA ya hali ya juu na ameshinda kwa kiasi kikubwa.Sasa hoja ya UFISADI imeishiwa nguvu.Kuna hili la UDINI sasa limeibuka & unfortunately kwa MAHASIMU wa Lowassa kwamba hili linawahusu wao safari hii na muda ni mfupi sana kwao kuweza kujisafisha kutoka katika doa hili la UDINI.Amini nakwambia nguvu ya JK imedhoofishwa na doa hili.Kete kubwa ya Lowassa ni kutokuwa na UDINI na anakubalika na makundi yote ya KIIMANI na yatatoa shinikizo kubwa kwa CCM kumpitisha yeye kama Mgombea wao.2015 hapatatosha CCM.
 

Nashindwa kuelewa sana watu mnapomfikiria Nchimbi kuwa rais wa nchi hii.Hivi kama ameshindwa kuliongoza jimbo lake hapa Songea urais wa nchi atuwezaje?jamani tuwe wakweli.Huu urais tuendako sasa hata mimi nitagombea.Wasira ana uwezo gani wa kuongoza nchi?Vipi wanaccm mmebadili sera ya ujana na kwenda uzee?Au mnabadilika kulingana na mazingira?
 
Mungu wangu, hata Nchimbi naye anaota kuwa Rais wa nchi hii? Pole sana Tanzania. Wassira by default hana uwezo wa kuongoza nchi hii ije mvua lije jua.

kama c lowasa bac n nchimbi kubali kataa
 

je wajua shule 15 za sekondar jimboni mwake zimejengwa kwa juhudi zake kabla hata hajawa mbunge??
 

ukwel ni kwamba cdm bado sana lbd 2050. Kama huamini njo mpwapwa utaona!
 
JK atapata wakati mgumu sana kuwakana na kuwatosa waliotoa pesa zao na kuhangaika kwa miaka 10 kumuweka pale,leo hii anakaa sebuleni na watu wachache ambao wanamtii na kumdanganya kuwa watapambana na hao EL/RA si kweli!atashangaa wakimgeuka dakika za mwisho!ajue kuwa mbinu zile zile na zaidi zitatumika,ajue kuwa makubaliano yao bado yapo na anatakiwa kuyatimiza!alisema urais wake hauna ubia sio kweli!wamekaa pembeni afanye kazi yake ila asisahau viapo vyao!EL asipopitishwa na CC ataiharibu CCM yake na nchi pia!
 
Vioja haviishi...Wassira anakuwa Rais kisha Picha ZakeTunaziweka kwenye sarafu zetu! Uchumi ukidorora Tutanza laumiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuruhuru mijitu ya Gombe kuongoza nchi.... Wala CCM Wasijidanganye maana kati ya hao wanaowapigia chapuo hakuna hata mmoja mwenye uwezo achilia mbali track records zenye kuonesha ufanisi wa Jambo lolote lile...Ngoyai anawafunika wote tena kwa mbali sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…