Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma?

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule?

Sheria ya Maadili ya Uchaguzi, kifungu 2.1k kinasema vyama vya siasa na wagombea wana wajibu wa "kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee itakayotumika katika kampeni za uchaguzi"

9107C2E0-5A2D-4EBF-9326-DC197DB523A5.jpeg
 
Mgombea urais kupitia CCM akiwa Magu ametumia muda mrefu Sana kutoa hotuba kwa kisukuma akiomba kura.

Huku ni kuendekeza ukabila, kitu ambacho baba wa taifa letu akitumia muda mrefu Sana kupambana nacho.

Hata mgombea ubunge ndugu Kiswaga akiwa Nyanguge ametema kisukuma tupu.

Sasa tunasubiri kuona NEC ikimchukulia hatua kali mgombea huyu na ikibidi kumfuta kabisa. Kwasabb anapandikiza ukabila nchini wakati wa kampeni zake.

Hiki kitendo hakikubaliki kabisa.
 
Back
Top Bottom