Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.
Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?
Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.
Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma???
Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule??