Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Hata membe kusini aliongea kilugha hii ni kawaida ya wa Tz

Anamuiga Membe! Halafu tume iko kimya kabisa mgombea mmoja akivunja maadili ya uchaguzi wazi wazi.
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma???

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule??
Sasa kama yuko kwa wasukuma kuchombeza kwa lugha yao wewe inakuuma nini?
 
Wasukuma pekee ni Milioni ngapi Chief? Kama umeenda shule njoo na jibu halafu nikulipue
Zaidi ya milioni 7,halafu huwezi kumpangia raisi kuwa asiongee lugha yake ambayo hata ndoto huwa anaota kwa kisukuma.
 
Kila Watu wanaelezwa masuala ya Eneo lao na ndio maana kampeni ni kila eneo mgombea anaenda kuwaeleza Watu wa eneo husika na wanaelezwa ilani inawagusa vipi.

Kama ishu ni kurushwa na TV basi wangeongea tu mara moja kila mgombea wakarushwa na TV basi tukasubiri kupiga kura lakini si hivyo kila eneo wanaelezwa masuala yao ya eneo lao na ya nchi.

Unajua kuwa kuna watu usukumani hasa wazee Hawajui kiswahili mpaka Leo? Mgombea akiwaambia kwa Lugha wanayoielewa wataelewa tu na sidhani Kama anaongea Kisukuma bali anakazia baadhi ya masuala kwa kisukuma Ili wananchi hata wasiojua kiswahili wamwelewe.
Ukienda baadhi ya maeneo ya wamasai na wasukuma hawajui kiswahili hili ninauhakika nalo .

Utetezi wa kipuuzi kabisa, mbona huduma za serikali kwenye hayo maeneo hayatolewi kwa lugha ya eneo hilo? Tukisema Magufuli kaleta ukabila nchi hii mnatokwa na mishipa. Kanuni za uchaguzi haziruhusu ukabila. Ingekuwa ni mpinzani angewekewa pingamizi, maana hata wapinzani walioonguliwa wameenguliwa kwa kanuni ndogondogo.
 
Ameogopa Tundu atajua alichokisema akaripuliwa Kama ya Juzikati singida. Meseji ilimfikia na jana aliigusia kwa machungu.


Tatizo ndege Tunduni, amepita amemnyea mazima. Khahahahahaha. Mwambieni anajisumbua bulletpluf imetoboka
 
Zaidi ya milioni 7,halafu huwezi kumpangia raisi kuwa asiongee lugha yake ambayo hata ndoto huwa anaota kwa kisukuma.

Ni msukuma? Kwanini kanuni za tume kuwa huruhusiwi kutumia kilugha kwenye kampeni zimewekwa? Huyu mtu huwa tunasema ana ulevi wa madaraka, na ndiye anayeagiza chaguzi za nchi hii kunajisiwa.
 
Kila siku mnatukana wasukuma washamba mara magu msukuma anapendelea kanda ya ziwa haya kaja kuwaonyesha usukuma mnalalamika aiseee

Ukitaka kujua hujui unachoongea, angalia hujaweka koma wala nukta kwenye huu upuuzi wako.
 
JPM mpaka sasa anakura kama milioni 10 hivi.na wapinzani wanajua, ndo maana kila jambo wao wanalamika kwasababu wanajua washashindwa.
 
Kisukuma kinaongelewa Mwanza na wasukuma, na Watanzania wengine wa mikoa ya kanda ya ziwa wanaelewa ujumbe unaotolewa tafuta wakalimani tu. Au ulitaka aongee Kiingereza? Akili za kushikiliwa hizo na mabebebru.
 
Ukabila ktk kampeni haukubaliki... Ni nje ya democrasia na unachchea ubaguzi...
Nyerere alisema msiyafanye makabila makubwa ya Wasukuma, Wahaya, Wanyakyusa nk kuwa watawala wakuu wa nchi, tumeishakosea, tusirudie.
 
Lisu najua atakuja na vifungu vya sheria na kulisemea hili.
Kwani hawa watu wanafuata hata hivyo vifungu vya sheria basi? Kama ingekuwa wanafuata vifungu vya sheria huyu mzee tayari si mgombea halali, tumelazimishiwa na tume yake ya uchaguzi. Na kwakuliendeleza hilo hata yeye anatulazimisha tumchague yeye na watu anao wataka, bila hivyo tusiulizane huko mbeleni.
 
Lissu alipoongea kinyaturu kwao mlisemaje,? Juzi kati Membe kaongea kikwao huko kusini mlisemaje?
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?...
NEC ya CCM yeye ndiye mwenyekiti wake, ukweli anazungumza kwa kiswahili ila vipazasauti vinagoogle kwa kisukuma, hivyo hana kosa.
 
Kuna mambo mengi sana ya ajabu kwenye chama changu. Rais na timu yake wanaongea Kisukuma, anatishia wapiga kura kumpigia anayemtaka. Bashiru naye anamponda Kigwangalla, Makamu wa Rais anajidai na risasi zao.

Kila mtu anaongea lugha yake. Je ndio mwisho wa CCM? Maana hakueleweki kabisa. Mnara unaanguka, siyo kitu cha kawaida mgombea kumpigia kampeni mpinzani. Nimeuona TLP na CCM au Dozi ya Lissu inaingia?
 
Mapokezi ya Mwanza ni Shida kesho Kirumba na Furahisha zitajaa.
 
Rais na timu yake wanaongea Kisukuma, anatishia wapiga kura kumpigia anayemtaka
IMG-20200906-WA0023.jpg


Makamu wa Rais anajidai na risasi zao.

20200906_153110.jpg

Bashiru naye anamponda Kigwangalla,
2509992_85964FB6-F44E-4AB7-9794-81654EC0BA7D.jpeg
 
Back
Top Bottom