Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Endelea kupamba kaburi lkn ndani mwake ni uvundo mtupu. Swali: Kutumia kilugha kwenye kampeni ni kuendeleza ubaguzi na ukabila. Kweli si Kweli??
Sio kuendeleza ukabila. Vitendo ndivyo vinaendekeza ukabila kuliko lugha peke yake.

Enzi za Mkapa TRA ilikuwa na wakurugenzi nane kutoka Mkoa mmoja wa kaskazini na hakuna aliyehoji chochote.

Nenda Nigeria ndio utaujua ukabila upo vipi.
 
Asilimia kubwa ya wanaokuwepo katika hiyo mikutano wanaelewa kisukuma na sio kwamba kwa kuongea kisukuma kuna kifungu cha katiba kinavunjwa.

Hili ni jambo dogo sana kulinganisha na yaliyoandikwa kwenye ilani ya kurasa 303 yenye kutakiwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano.

Nyerere alikuwa anaongea kizanaki mpaka katika mikutano ya CCM miaka ile na hakuna aliyewahi kumkosoa.

Tuachane na hizi nongwa za kitoto.
Nyerere alipoongea kizanaki alitafsiri pia. Unapotaka kuusema uongo yakupasa kuujengea mazingira ili ufanane na ukweli na usionekane kuwa ni upuuzi fulani unaopaswa kupuuzwa. Nikufahamishe kitu kimoja rahisi "ukiacha shonde au mashi kalioni nzi watakufuata!!" Na ukiuza utumbo usiogope inzi Mkuu.
Hakuna pori ambalo huteketea pasipo kuanza na cheche ndogo ya moto.
Mtakata sana viunu na vigelegele mtapiga sana kweli itabaki kweli UKABILA NA UDINI VINAZIDI KUSHAMIRI
 
Anaongea na wasukuma wenzake wewe unachowashwa ni nn?
Sawa, lakini nini maana yake kwa mgombea mwingine ambaye sio Msukuma, akifika pale si ataonekana ni wakuja tu? Alichofanya kinaondoa dhana kubwa ya kushindana katika masafa yanayolingana, anawafanya wapiga kura wamtambue yeye kama mmoja wao zaidi ya chochote na kumnyima fursa mgombea asiye msukuma ya kufikiriwa. Ni vizuri akazingatia sheria lakini pia kwa nafasi kubwa aliyo nayo ya kulea demokrasia, anapaswa aadhibiwe kwa kweli!
 
Nyerere alipoongea kizanaki alitafsiri pia. Unapotaka kuusema uongo yakupasa kuujengea mazingira ili ufanane na ukweli na usionekane kuwa ni upuuzi fulani unaopaswa kupuuzwa. Nikufahamishe kitu kimoja rahisi "ukiacha shonde au mashi kalioni nzi watakufuata!!" Na ukiuza utumbo usiogope inzi Mkuu.
Hakuna pori ambalo huteketea pasipo kuanza na cheche ndogo ya moto.
Mtakata sana viunu na vigelegele mtapiga sana kweli itabaki kweli UKABILA NA UDINI VINAZIDI KUSHAMIRI
Acha kuwa na mawazo yaliyokufa tayari.

Ukitaka kuujua ukabila na madhara yake waulize Sudan waliopata uhuru wakiwa taifa moja na leo wana Sudan kusini na kaskazini.

Waulize Ethiopia wanaoishi na matabaka. TZ usitegemee tukafika huko unakotaka wewe tufike.

Kama unaelewa maana ya viongozi wa dini kuanza kwa sala mikutano yote ya kampeni ya JPM huwezi kuwa na mawazo kwamba kuongea kisukuma kwa Rais kunaweza kuwa na madhara yoyote.

Achana na hizo njozi za mchana.
 
Kila siku mnatukana wasukuma washamba mara magu msukuma anapendelea kanda ya ziwa haya kaja kuwaonyesha usukuma mnalalamika aiseee
Mgombea wa CCM John Pombe Joseph Magufuli amesema kwa kipindi cha miaka 5 ametengeneza ajira milioni 6.

Nyie waimba sifa wake mwambieni labda waliojiriwa walitangaziwa ajira Ikulu, wakafanyiwa interview Ikulu,wakaajiriwa Ikulu. Lakin Huku mtaani kwetu vijana hawana ajira,walimu hawana ajira.Hali ni ngumu Mzee.
 
Eti viongoz wa din!!!hawa wajasiriamali wanaoendesha maisha yao kupitia din
Acha kuwa na mawazo yaliyokufa tayari.

Ukitaka kuujua ukabila na madhara yake waulize Sudan waliopata uhuru wakiwa taifa moja na leo wana Sudan kusini na kaskazini.

Waulize Ethiopia wanaoishi na matabaka. TZ usitegemee tukafika huko unakotaka wewe tufike.

Kama unaelewa maana ya viongozi wa dini kuanza kwa sala mikutano yote ya kampeni ya JPM huwezi kuwa na mawazo kwamba kuongea kisukuma kwa Rais kunaweza kuwa na madhara yoyote.

Achana na hizo njozi za mchana.
 
Acha kuwa na mawazo yaliyokufa tayari.

Ukitaka kuujua ukabila na madhara yake waulize Sudan waliopata uhuru wakiwa taifa moja na leo wana Sudan kusini na kaskazini.

Waulize Ethiopia wanaoishi na matabaka. TZ usitegemee tukafika huko unakotaka wewe tufike.

Kama unaelewa maana ya viongozi wa dini kuanza kwa sala mikutano yote ya kampeni ya JPM huwezi kuwa na mawazo kwamba kuongea kisukuma kwa Rais kunaweza kuwa na madhara yoyote.

Achana na hizo njozi za mchana.
Mtakatika kila aina ya mkatiko mkuu ukabila tayari upo mlangoni. Hoja ni nguvu za kuukemea fullstop.

Inasikitisha na kuhuzunisha kura za Magufuli zinaombwa kwa ukabila na eneo analotoka.

Leo yuko Geita cha ajabu kikabila kinatumika kuomba kura tena kwa vijembe kwa kusema inakuwaje mnataka kumchagua asiye wa nyumbani kwenu usukumani na kasema kwa kuwa tunafahamiana kwenye mikutano yao wakija ole msukuma ahudhurie baada ya Uchaguzi wataonana.

Huu ukabila Tume ya Uchaguzi haioni kuwa ni kuligawa taifa?
 
Jiunge nao kama ni rahisi sana kuwa kama wao.
Matunda ya Miaka 43 ya Utawala wa CCM Maradhi, Ujinga na Umaskini wa kutupwa. Walau wakati wa TANU hawajamaa walikuwa wanakondeana... tangu CCM ifanye Azimio la Zanzibar 1992, kasi ya unono na ukibonge inaongezea maradufu!
 
Mbona Lussi kule Singida wakati wa kutafuta wadhamini aliongea Kinyaturu?

..Tundu Lissu alikosea kuzungumza kilugha.

..anatakiwa aonywe ili asirudie tena.

..muongozo wa tume ya uchaguzi uzingatiwe kwamba wagombea wazungumze Kiswahili.

..kama kuna wananchi hawaelewi Kiswahili, Tume inaelekeza kwamba watafutiwe mkalimani.
 
Ila humu JF kuna watu wanajiamini kijinga mpaka unajiuliza Kuna limbwata la kumfanya mtu awe mjinga. Sasa wewe Lisu amemshika Pabaya kwa Lipi. Unazungumzia Tanzania au ubelgiji.
Usinifokee
Huoni mzee wa watu anapiga push up
 
..Tundu Lissu alikosea kuzungumza kilugha.

..anatakiwa aonywe ili asirudie tena.

..muongozo wa tume ya uchaguzi uzingatiwe kwamba wagombea wazungumze Kiswahili.

..kama kuna wananchi hawaelewi Kiswahili, Tume inaelekeza kwamba watafutiwe mkalimani.
Acha kasumba mkuu. Kabla mkoloni hajaja babu zetu waliongea lugha za asili muda wote.

Leo baada ya kutawaliwa haina maana lugha zetu zimepoteza umuhimu wake.

Tujivunie utu wetu na asili yetu kwani ndio utambulisho wetu.

Wamasai wanatembea na mashuka yao na ukiwakuta wapo wao tu sehemu huwa wanaongea kimasai, haimaanishi kwamba wao ni watanzania nusu kwa kutunza Mika na desturi zao.
 
Wewe unaeujua juhudi zako zinaonekana mkuu ndugu yangu.

Tuwe wapole mheshimiwa akikimwaga kisukuma mbele ya wasukuma. Hakuna kinachopungua.

Mwambie Mbowe amwage kimachame mbele ya wamachame wa hai.

Mwambie Lissu amwage kinyaturu mbele ya wanyaturu wenzake.
 
Back
Top Bottom