Uchaguzi 2020 Mgombea Urais CCM kuhutubia kwa kisukuma huko Mwanza. Huu ni ukabila. NEC tunasubiri kuona hatua kali dhidi yake

Acha kasumba mkuu. Kabla mkoloni hajaja babu zetu waliongea lugha za asili muda wote.

Leo baada ya kutawaliwa haina maana lugha zetu zimepoteza umuhimu wake.

Tujivunie utu wetu na asili yetu kwani ndio utambulisho wetu.

Wamasai wanatembea na mashuka yao na ukiwakuta wapo wao tu sehemu huwa wanaongea kimasai, haimaanishi kwamba wao ni watanzania nusu kwa kutunza Mika na desturi zao.

..lugha ya taifa ina nafasi yake, na lugha za makabila zina nafasi yake.

..kwenye masuala ya ya kitaifa, hususan kampeni za uchaguzi, lugha inayopaswa kutumika ni lugha yetu ya taifa, KISWAHILI.

..kama kuna wananchi ambao hawaelewi, Tume ya Uchaguzi imeelekeza kwamba wapewe huduma ya MKALIMANI.

..maana yake ni kwamba hakuna mgombea ambaye anaruhusiwa kuongea kilugha, kama wanataka waeleweke zaidi wanatakiwa waweke wakalimani watakaotafsiri Kiswahili kwenda kwenye lugha inayolengwa.

..mwisho, TL alikosea kuzungumza kilugha akiwa Singida, na Magufuli alikosea kuzungumza kilugha akiwa Mwanza.

NB:

..binafsi naamini Mtanzania msomi anapaswa kuzungumza lugha yake ya asili, lugha ya taifa Kiswahili, na lugha ya fursa Kiingereza.

..jambo la msingi ni kuzingatia mahala sahihi, na mazingira muafaka, ya kuzitumia lugha hizo.
 
Mkuu wewe kama ni mwanasiasa na unaweza kuongea lugha yako ya asili zungumza tu kwani sio wote wenye kujua kiswahili.

Huko umasaini mpaka leo kuna wazee ni mpaka watafsiriwe wanachokisikia kikiongelewa kwa kiswahili.

Ni jambo dogo linalokuzwa.
 
..Tume imeelekeza nini cha kufanya pale ambapo kuna wananchi wasioelewa lugha ya Kiswahili.

..na imeelekeza kwamba wananchi wapewe huduma ya ukalimani ili waweze kuwaelewa wagombea.
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma?

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule?

Sheria ya Maadili ya Uchaguzi, kifungu 2.1k kinasema vyama vya siasa na wagombea wana wajibu wa "kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee itakayotumika katika kampeni za uchaguzi"

View attachment 1560689
Ni kweli; jamaa anatumia kisukuma sana anapokuwa kanda ya ziwa na hayo ni makosa. Ingawa bado hajavunja sheria kwa vile huwa anahutubia kwa kiswahli ila anakuwa anatumia kisukuma kama kikolezo tu, lakini ni image mbaya sana. Ni kama ambavyo angeweza kuwa anahutubia kwa kiswahili lakini akiwa anaweka maneno ya kiingereza. Huwa sifurahishwi na watu wanaojidai kutumia kiswahili huku wakichanganya lugha
 
..Tume imeelekeza nini cha kufanya pale ambapo kuna wananchi wasioelewa lugha ya Kiswahili.

..na imeelekeza kwamba wananchi wapewe huduma ya ukalimani ili waweze kuwaelewa wagombea.
Miongoni mwa wasikilizaji wa hotuba kuna wanaofanya kazi ya ukalimani kwa wasiojua kiswahili.
 
..Kanuni za Uchaguzi zilizowekwa na Tume ya Taifa zinaelekeza kwamba ni MWIKO kwa wagombea kutumia lugha za makabila.

..hili tatizo liko kwa wagombea wa vyama vyote na kwa ngazi zote, tunapaswa kuungana pamoja kuwataka wajirekebishe.

..tatizo hili siyo la Magufuli peke yake,ingawa yeye ndiyo anaonekana zaidi. Wapo hata wagombea wa upinzani wenye tatizo hilo.

..tuweke ushabiki wa wagombea, na ushabiki wa vyama pembeni. Tujenge nchi pamoja.
 
Hapa mkuchika anapiga kilugha huko mtwara lakini kabudi nae kule kilosa alipiga cha nyumbani
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma?

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule?

Sheria ya Maadili ya Uchaguzi, kifungu 2.1k kinasema vyama vya siasa na wagombea wana wajibu wa "kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee itakayotumika katika kampeni za uchaguzi"

View attachment 1560689
MTU umekwenda geita vijijini huko kiswahili tu ni changamoto kisukuma kipigwe kabisa
 
MTU umekwenda geita vijijini huko kiswahili tu ni changamito kisukuma kipigwe kabisa
Mkuu, hata hili ni la kulitetea!? Mengine ni kukaa kimya tu. Yeye siyo malaika, anakosea kama binadamu mwingine tu. Hapo sheria hairuhusu ndugu. Inasema pale Kiswahili kisipoeleweka kwa watu wa eneo husika, yeye mgombea aongee tu kwa Kiswahili na mtu mwingine atafsiri kwa hiyo lugha ya watu wa eneo hilo. Hii inataka watanzania wengine waendelee kuelewa kwa Kiswahili, na wakati huo huo hao wengine wapate tafsiri kwa hiyo lugha yao. Ila kwa sababu NEC ndo hivyo tena, hawataliongelea hilo. Hapo ndipo utaona umuhimu wa tume huru ya uchaguzi.
 
..Kanuni za Uchaguzi zilizowekwa na Tume ya Taifa zinaelekeza kwamba ni MWIKO kwa wagombea kutumia lugha za makabila.

..hili tatizo liko kwa wagombea wa vyama vyote na kwa ngazi zote, tunapaswa kuungana pamoja kuwataka wajirekebishe.

..tatizo hili siyo la Magufuli peke yake,ingawa yeye ndiyo anaonekana zaidi. Wapo hata wagombea wa upinzani wenye tatizo hilo.

..tuweke ushabiki wa wagombea, na ushabiki wa vyama pembeni. Tujenge nchi pamoja.
Huwezi kukwepa watu wasiojua kiswahili na hao wenye kuiongoza tume wanalijua hilo.

Matumizi ya lugha ni huru katika nchi huru.
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma?

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule?

Sheria ya Maadili ya Uchaguzi, kifungu 2.1k kinasema vyama vya siasa na wagombea wana wajibu wa "kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee itakayotumika katika kampeni za uchaguzi"

View attachment 1560689
Kwani ameshafanya mangapi ambayo ni kinyume na katiba?
1. Kuwatisha wananchi Musoma na Geita
2. Kuongea kisukuma tofauti na kanuni za tume ya uchaguzi ilizojiekea
3.
4.
5.
Na ataendelea na kuendelea.
Yote haya yakidhihirisha kuwa yeye ni dikteta na anafanya kampeni akiwa na matokeo tayari. Hii inadhihirika pale alipowaambia wananchi "siwatishi bali nawaambia ukweli, mkinichagulia wa vyama vingine, maendeleo kwenye maeneo yenu hayatakuja"
Hapo hapo akijinasibu na kauli yake maendeleo hayana vyama.
Labda kama upinzani una strategies za kukabiliana na maamuxi yatakayochukuliwa na tume. Nguvu ya umma ni muhimu
 
Huwezi kukwepa watu wasiojua kiswahili na hao wenye kuiongoza tume wanalijua hilo.

Matumizi ya lugha ni huru katika nchi huru.

..kweli.

..lakini tume imeelekeza wawepo wakalimani na siyo wagombea kutembelea walikozaliwa halafu kuanza kuzungumza kilugha.
 
Tuwe wapole mheshimiwa akikimwaga kisukuma mbele ya wasukuma. Hakuna kinachopungua.

Mwambie Mbowe amwage kimachame mbele ya wamachame wa hai.

Mwambie Lissu amwage kinyaturu mbele ya wanyaturu wenzake.
Tunajenga nchi kinamna hiyo au sio? Kisha kila mtu aombe kura kikwao nyumbani kwao na wengine wasikanyage huko!!!
Kuna methali yasema "aljununu fununu!!"
 
Hii ni aibu aisee, yaani inatia kinyaa sana niko namsikiliza anapiga kampeni Magu kila baada ya maneno matatu ni full kisukuma.

Haileti picha nzuri kabisa, kwa sababu kampeni inarushwa Tanzania nzima, sasa kusema kwamba kama anamwaga sera, mtu wa kule Tanga anamuelewa vip?

Huu ni udhaifu mkubwa, halafu eti ndo anajifananisha na Baba Wa Taifa, shame. Nashangaa hata wanaomtetea, huu ni ukabila wa wazi wazi.

Ingekuwa ni mgombea ubunge sawa ila rais anahutubia kisukuma?

Hivi hawa ndo CCM walikuwa wanasema watu wa kaskazini ni wakabila? Au ni tabia ya Nyani kutokuona Kundule?

Sheria ya Maadili ya Uchaguzi, kifungu 2.1k kinasema vyama vya siasa na wagombea wana wajibu wa "kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee itakayotumika katika kampeni za uchaguzi"

View attachment 1560689
Mgombea Urais wa CHADEMA anamsimanga Magufuli, sasa mnaanza kumshabulia nanyi pia mitandaoni! Mwaga Sera zenu hapa tuzichambue kwa jinsi gani zitaleta maendeleo ya "watu" na siyo "vitu".

Akili ndogo huzungumzia watu, BASI
 
Tunajenga nchi kinamna hiyo au sio? Kisha kila mtu aombe kura kikwao nyumbani kwao na wengine wasikanyage huko!!!
Kuna methali yasema "aljununu fununu!!"
Tunajenga nchi kwa kufanya kazi na kuwa na nidhamu ya kimaisha.

Suala la lugha ni dogo sana kwa mtu mwenye upeo mkubwa wa kuitazama dunia inakwenda vipi na Tanzania ifanye nini ili iweze kuwa na maendeleo.
 
Hakuna wakati wa kabila kubwa wala dogo kutawala, ujumbe ni kwamba tuwashukuru kina Nyerere kwani kama wangekuwa hawana maono basi kabila kubwa kama wasukuma wangesumbua tangu miaka ile ya sitini mwanzoni baada tu ya uhuru.

Nigeria na mataifa mengine makubwa yalishindwa kuwadhibiti “wasukuma” wao na mpaka kesho wanasumbuka.
Hata Kenya wakikuyu wameshindikana
 
Tunajenga nchi kwa kufanya kazi na kuwa na nidhamu ya kimaisha.

Suala la lugha ni dogo sana kwa mtu mwenye upeo mkubwa wa kuitazama dunia inakwenda vipi na Tanzania ifanye nini ili iweze kuwa na maendeleo.
Maendeleo hayaletwi na mdomo, chuki na utengano. Maendeleo hayaletwi na kutokubali katika kutokubaliana. Maendeleo hayaletwi kwa kusifiana pasina kukosoana. Maendeleo hayaletwi na ubinafsi, uchama, udini, ukanda, ukabila, unafiki, uzandiki au vinavyofanana na hayo...
Maendeleo hayaji pasina sera maridhawa na endelevu kwa taifa. Maendeleo ni vigumu sana kupatikana kwa katiba yenye viraka na matobo mengi.
Ikiwa hatujifunzi kwa Malaysia, Philippines, Botswana na tuendelee na uzalendo wetu wa nyimbo na mapambio ili tuonwe na wakubwa!!
*nidhamu ya kazi pasina madaraja wala mishahara kuongezwa...!!
*bila wakulima kupata stahili na stahiki zao...!!!
*uzalendo kuwa ni wa kile chama na wafuasi wake walioifilisi nchi..!!!
Sote sio mazwazwa na wasahaulifu tunajua tulikojikwaa...
 
Unaweza kuwa umejikwa kifikra pia kwa kuwa na tafsiri potofu ya kinachofanywa na serikali.

Wale wenye tafsiri sahihi wakawa ni wengi kuliko wa aina yako hivyo machungu uliyonayo yakawa ni kama kuikausha bahari kwa glasi ya maji.
 
WALIOSEMA WAZIMU PIA NI FANI HAWAKUKOSEA. HUWEZI ONA MATOBO WALA HUWEZI KUONA UKATAMBUA USICHOPENDA KUKIONA. UNAJUA WAZI UMASKINI WA NCHI HII UMEKUJAJE!! Kubeza na madharau ni silka ya watu wanaoamini kuwa wanajua kana kwamba wengine kasoro hawazioni. Yawezekana KWELI NINYI NI WENGI KAMA MAJI YA BAHARI LAKINI YASIYOFAA KUNYWEKA KWA WENYE KIU. Hata tende huanza kama kipele. Ila walisema wahenga mdharau mwiba huota tende hawakukosea.
Mwisho wa siku msomi kujipa sifa "...majalalani!!"
Vema tubakize akili kichwani kuliko kuzihamishia matumboni.
 
Back
Top Bottom