Acha kasumba mkuu. Kabla mkoloni hajaja babu zetu waliongea lugha za asili muda wote.
Leo baada ya kutawaliwa haina maana lugha zetu zimepoteza umuhimu wake.
Tujivunie utu wetu na asili yetu kwani ndio utambulisho wetu.
Wamasai wanatembea na mashuka yao na ukiwakuta wapo wao tu sehemu huwa wanaongea kimasai, haimaanishi kwamba wao ni watanzania nusu kwa kutunza Mika na desturi zao.
..lugha ya taifa ina nafasi yake, na lugha za makabila zina nafasi yake.
..kwenye masuala ya ya kitaifa, hususan kampeni za uchaguzi, lugha inayopaswa kutumika ni lugha yetu ya taifa, KISWAHILI.
..kama kuna wananchi ambao hawaelewi, Tume ya Uchaguzi imeelekeza kwamba wapewe huduma ya MKALIMANI.
..maana yake ni kwamba hakuna mgombea ambaye anaruhusiwa kuongea kilugha, kama wanataka waeleweke zaidi wanatakiwa waweke wakalimani watakaotafsiri Kiswahili kwenda kwenye lugha inayolengwa.
..mwisho, TL alikosea kuzungumza kilugha akiwa Singida, na Magufuli alikosea kuzungumza kilugha akiwa Mwanza.
NB:
..binafsi naamini Mtanzania msomi anapaswa kuzungumza lugha yake ya asili, lugha ya taifa Kiswahili, na lugha ya fursa Kiingereza.
..jambo la msingi ni kuzingatia mahala sahihi, na mazingira muafaka, ya kuzitumia lugha hizo.