Aende hata akiwa uchi wa mnyama... Sisi tunasubiri kwa hamu kubwa rais wetu wa 2020-2025, Lissu aende kuchukuwa tumsindikize.
Wanata ku make headline, waandikwe wao, watambulishwe vyama vyao, ionekane vyama vingi vimeshiriki ili wakija kuwafanyia figisu Chadema na ACT wawe na vyama vya upinzani kusema tumekubali kushindwa viwe vingi.
Wanasahau upinzani uko Chadema na ACT hao wengine hawana kitu. Wakiungana Chadema na ACT na uchaguzi ukawa huru na haki ni wana kijani wanashindwa na wanalijua hilo
Amewatupia ujumbe waliotutangazia kuwa tumeingia Uchumi wa Kati! Bila kuwa Great Thinker hauwezi kumuelewa utaona kama kituko.#Uchaguzi2020 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza Satia Musa, walipowasili hii leo Agosti 7, 2020, kwenye ofisi za NEC wakiwa peku bila Viatu kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ.
View attachment 1529723
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha SAU, Mutamwega Bati Mgaiwa (kushoto) katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Chama hicho kimekuwa cha tano kuchukua fomu
View attachment 1529724
Kwamba hapo tume ni ardhi takatifu!!
Hii inamaanisha nini kuenda peku peku?