Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia SAU, Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza wamewasili Ofisi za NEC peku kuchukua fomu

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
#Uchaguzi2020 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza Satia Musa, walipowasili hii leo Agosti 7, 2020, kwenye ofisi za NEC wakiwa peku bila Viatu kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ.

1.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha SAU, Mutamwega Bati Mgaiwa (kushoto) katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Chama hicho kimekuwa cha tano kuchukua fomu

2.jpg

1.jpg
2.jpg
 
Wanata ku make headline, waandikwe wao, watambulishwe vyama vyao, ionekane vyama vingi vimeshiriki ili wakija kuwafanyia figisu Chadema na ACT wawe na vyama vya upinzani kusema tumekubali kushindwa viwe vingi.

Wanasahau upinzani uko Chadema na ACT hao wengine hawana kitu. Wakiungana Chadema na ACT na uchaguzi ukawa huru na haki ni wana kijani wanashindwa na wanalijua hilo
 
Watakuwa wanatafuta nafasi za kuteuliwa hao sio kwa mwembwe hizo aisee
 
Hata wangeazima makalio ya DAB yule aliyefyekwa na wajumbe ukivuka ferry na kuja nayo matupu tungeeapuuza tuu
 
Chadema na ACT navyo vilipitia maneno yako mkuu its multiparty system. Wapo huru kuwa na tolerance
Wanata ku make headline, waandikwe wao, watambulishwe vyama vyao, ionekane vyama vingi vimeshiriki ili wakija kuwafanyia figisu Chadema na ACT wawe na vyama vya upinzani kusema tumekubali kushindwa viwe vingi.

Wanasahau upinzani uko Chadema na ACT hao wengine hawana kitu. Wakiungana Chadema na ACT na uchaguzi ukawa huru na haki ni wana kijani wanashindwa na wanalijua hilo
 
Mgombea wa Chama cha SAU, Mutamwega Bati Mgaiwa amefika katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020 kuchukua fomu ya kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania.

Chama hicho kinakuwa cha tano kuchukua fomu na Mgaiwa amekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage.

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi Agosti 25,2020.

photo_2020-08-07_13-01-40.jpg
 
#Uchaguzi2020 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza Satia Musa, walipowasili hii leo Agosti 7, 2020, kwenye ofisi za NEC wakiwa peku bila Viatu kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ.

View attachment 1529723
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha SAU, Mutamwega Bati Mgaiwa (kushoto) katika Ofisi za NEC, Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 6,2020. Chama hicho kimekuwa cha tano kuchukua fomu

View attachment 1529724
Amewatupia ujumbe waliotutangazia kuwa tumeingia Uchumi wa Kati! Bila kuwa Great Thinker hauwezi kumuelewa utaona kama kituko.
 
Kwahiyo wakishika madaraka wananchi tujiandae kutembea bila viatu hawatufai hawa.
 
Back
Top Bottom