Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa ACT Wazalendo ni Zitto au Membe? Tuko hoi Jamani

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa ACT Wazalendo ni Zitto au Membe? Tuko hoi Jamani

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
MGOMBEA URAIS WA ACT NI ZITTO AU MEMBE? TUKO HOI JAMANI

WARAKA WA KWANZA WA VIJANA

Sisi Vijana wa ACT kutoka mikoa mbalimbali tunaendelea kusikitishwa na mwenendo wa uendeshaji wa Chama chetu ambapo mpaka sasa hatuelewi kampeni inaendeshwa vipi zaidi ya kuona kila kitu kiko kwa mtu mmoja.

Pale Mlimani City tena kwa mbwembwe, Chama chetu kilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa mgombea Urais na akaahidi kampeni ya kishindo. Kiongozi wa Chama naye akaahidi hivyo hivyo.

Cha ajabu na ambacho sasa tunahitaji majibu kwa Chama ni badala ya mgombea huyo rasmi wa Urais kufanya kampeni sasa hivi tunamuona kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe akifanya mikutano mingi ya kampeni kuliko hata mgombea Urais.

Juzi tu Zitto Kabwe alikuwa Dar, akaenda Kigoma na tukamionankwenye ndege za ATC, akarudi Dar, akaenda Mafia, akaenda Mtwara sasa kaenda Kigoma, swali huyu ndiye mgombea Urais wetu mpya? Ameteuliwa kimya kimya? Mzee wetu Membe kapatwa na nini?

Hivi kwa stratejia hizi zilizoshindwa mapema tukipata kura kiduchu tutaanza vurugu za kudai tumeibiwa kura? Na nani kama mgombea wiki nne sasa hayuko majukwaani badala yake anafanya mtu ambae sio mgombea na kujibrand yeye.

Tena bahati mbaya Ndugu Zitto wala hamwombei kura mgombea, yeye ni kuhangaika na Magufuli na CCam na kumsifu na kujipendekeza kwa Lissu wa Chadema. Hakika hivi ni vituko!

Zaidi sasa kiongozi wetu wa vijana naye akitoka Kigoma kama Zitto, Abdul Nondo, anamzidi Membe eti kwa naye kusafiri kwenda kuzindua mikutano ya Wabunge nchi nzima!!

Hiki Chama hakina uongozi, hakina stratejia na kimechoka katika umri mdogo sana. Tunasikitika.

Yani tunaumia sasa sisi vijana tunaohangaika huku mitaani kukitangaza Chama, huku kiongozi wa Chama na mgombea Urais wakituahidi kampeni ya kishindo ndio hii ya Zitto kuzunguka kula per diem na Nondo aliyetoka chuoni mwaka jana kuwa ndio mwanasiasa wa kwenda kuzindua kampeni za majimbo na wakongwe wa siasa ndani ya Chama kuachwa??

Kweli!!!!!Ndio tumefikia this low?

Tunahitaji majibu. Yani ACT kimekuwa chama cha kikabila, utasikia Maalim Seif yuko Pemba, Zitto yuko Kigoma, mikoa mingine chama ziiiii. Inatuuma sana.

*Waraka wa Vijana wa ACT, Tanzania Bara*
 
Yani mi mwenyewe sielewi kwa kweli bora mmeuliza, membe namuona tu tweeter huko akijinasibu
 
Zitto amehojiwa kuhusu hilo akajibu kuwa Bw. Membe yupo bize kupanga baraza la mawaziri maana ameshashinda!

Mimi nadhani NEC inachezewa mchezo flani! Nadhani kuna makubaliano flani yasiyo rasmi kati ya ACT na CHADEMA. Muda utasema
 
Zitto amehojiwa kuhusu hilo akajibu kuwa Bw. Membe yupo bize kupanga baraza la mawaziri maana ameshashinda!

Mimi nadhani NEC inachezewa mchezo flani! Nadhani kuna makubaliano flani yasiyo rasmi kati ya ACT na CHADEMA. Muda utasema

Ni kweli hata mimi nimezisikia hizo tetesi
 
Kimbunga kumba kumba kimefika pwani ya Kenya kikitokea Dubai,kueni Na suburbs kitafika tu
 
Hesabu inakwama, Zitto yeye anatafuta wabunge wa kutosha ndio sababu anazunguka sehemu nyingi.

Membe simuelewi, sijui ana bifu na Zitto au pesa za kampeni ni shida.
 
Hata mimi pia, Membe anapanga Baraza la Mawaziri la Tundu Lissu. Ushindi tayari na nchi za Afrika Rais hapatikani jukwani kama alivyosema. Wanadai eti hatuna Tume Huru za Uchaguzi. Wanatuchagulia wao Rais wanayemtaka bila hivyo nchi za Afrika hazina uwezo wa kuwatoa madarakani watawala. Omba uhai Oct 28 uwepo.
 
Back
Top Bottom