kinje ketile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 5,089
- 9,664
Mama Ana Mghwira Uko wapi ? Kile chama ulichokisimamia na kusimama kama mgombea Uraisi leo wanakinajisi wale uliowaacha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo alishakua mchumia tumbo anataga mayai ya kija i sasaMama Ana Mghwira Uko wapi ? Kile chama ulichokisimamia na kusimama kama mgombea Uraisi leo wanakinajisi wale uliowaacha.
Dakika ya 89 ipo karibu...Tulieni nyie, kula mtori nyama utazikuta chini.
We UVCCM hayo ya ACT waachie wenyewe... hangaikia ya kwako.MGOMBEA URAIS WA ACT NI ZITTO AU MEMBE? TUKO HOI JAMANI
WARAKA WA KWANZA WA VIJANA
Sisi Vijana wa ACT kutoka mikoa mbalimbali tunaendelea kusikitishwa na mwenendo wa uendeshaji wa Chama chetu ambapo mpaka sasa hatuelewi kampeni inaendeshwa vipi zaidi ya kuona kila kitu kiko kwa mtu mmoja.
Pale Mlimani City tena kwa mbwembwe, Chama chetu kilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa mgombea Urais na akaahidi kampeni ya kishindo. Kiongozi wa Chama naye akaahidi hivyo hivyo.
Cha ajabu na ambacho sasa tunahitaji majibu kwa Chama ni badala ya mgombea huyo rasmi wa Urais kufanya kampeni sasa hivi tunamuona kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe akifanya mikutano mingi ya kampeni kuliko hata mgombea Urais.
Juzi tu Zitto Kabwe alikuwa Dar, akaenda Kigoma na tukamionankwenye ndege za ATC, akarudi Dar, akaenda Mafia, akaenda Mtwara sasa kaenda Kigoma, swali huyu ndiye mgombea Urais wetu mpya? Ameteuliwa kimya kimya? Mzee wetu Membe kapatwa na nini?
Hivi kwa stratejia hizi zilizoshindwa mapema tukipata kura kiduchu tutaanza vurugu za kudai tumeibiwa kura? Na nani kama mgombea wiki nne sasa hayuko majukwaani badala yake anafanya mtu ambae sio mgombea na kujibrand yeye.
Tena bahati mbaya Ndugu Zitto wala hamwombei kura mgombea, yeye ni kuhangaika na Magufuli na CCam na kumsifu na kujipendekeza kwa Lissu wa Chadema. Hakika hivi ni vituko!
Zaidi sasa kiongozi wetu wa vijana naye akitoka Kigoma kama Zitto, Abdul Nondo, anamzidi Membe eti kwa naye kusafiri kwenda kuzindua mikutano ya Wabunge nchi nzima!!
Hiki Chama hakina uongozi, hakina stratejia na kimechoka katika umri mdogo sana. Tunasikitika.
Yani tunaumia sasa sisi vijana tunaohangaika huku mitaani kukitangaza Chama, huku kiongozi wa Chama na mgombea Urais wakituahidi kampeni ya kishindo ndio hii ya Zitto kuzunguka kula per diem na Nondo aliyetoka chuoni mwaka jana kuwa ndio mwanasiasa wa kwenda kuzindua kampeni za majimbo na wakongwe wa siasa ndani ya Chama kuachwa??
Kweli!!!!!Ndio tumefikia this low?
Tunahitaji majibu. Yani ACT kimekuwa chama cha kikabila, utasikia Maalim Seif yuko Pemba, Zitto yuko Kigoma, mikoa mingine chama ziiiii. Inatuuma sana.
*Waraka wa Vijana wa ACT, Tanzania Bara*