Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CCM aelezea faida za Kitambulisho cha Mjasiriamali

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CCM aelezea faida za Kitambulisho cha Mjasiriamali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
"Vitambulisho vya Ujasiriamali vina faida, unaweza hata kukopa kwenye Mabenki kwa kutumia vitambulisho hivi, maeneo kama Kigamboni wameweza kupangiwa kukopeshwa, vinatumika hadi kwenye Bima za Afya, mkituchagua vitaendelea ili kulinda maslahi ya wanyonge"-JPM
1601472200770.png

Kama wewe kweli ni Rais wa wanyonge, ungevitoa Vitambulisho hivi bure kwa wanyonge ili uwasaidie waweze kupata mikopo ya biashara kirahisi. Hakika wanyonge wasingekusahau.
 
Acheni kutuletea matatizo bure. Kitambulisho hakina jina, hakina picha, hakina alama yeyote ya kumtafuta mtu, lifespan ni mwaka mmoja, unapewa tu bora uwe na 20,000, hakuna sehemu yeyote ya kujaza fomu kama kumbukumbu ili upewe. Theni ukachukulie mkopo benki. Hivi benki siku hizi zinaendeshwa na wenda wazimu wa Lumumba? Mbona mnatuona Watanzania kama wajinga fulani aisee?
 
... duh! Vitambulisho vyenyewe si biashara? Vinauzwa vile na vimetungiwa sheria sijui kanuni in short havistahili kuitwa vitambulisho badala yake ni LESENI waache kuhadaa watanzania.
Acha kushushia hadhi leseni broo. Leseni ina jina la mmiliki na inatambulika kisheria na TRA wana kumbukumbu zake. Hizo photocopy za vitambulisho ndo ukachukulie mkopo benki? Benki gani? Hata VICOBA tunakutimua kudadeki. Yaani kitu ambacho unaweza kumuhasima mtu na ikawa halai yake ukachukulie mkopo?
 
MATAGA umemuelewa mgombea wenu au anawachanganya mnashindwa hata kumtetea Leo hii nilitarajia mkurugenzi watume aulizwe kuwa ni bank gani wanakopesha kwakupitia hivi vitambulisho visivyo na jina wala picha?je mgombea yupo sahihi au la?
 
MATAGA umemuelewa mgombea wenu au anawachanganya mnashindwa hata kumtetea Leo hii nilitarajia mkurugenzi watume aulizwe kuwa ni bank gani wanakopesha kwakupitia hivi vitambulisho visivyo na jina wala picha?je mgombea yupo sahihi au la?
Vinatumika kuunda vikundi vya wajasiriamali na wanachukua mikopo kama vikundi. Hivi vinakuwa kama uthibitisho kuwa wana kikundi ni wajasiriamali. Tatizo Chadema ni kupinga pinga tu. Hii haitusaidii
 
Dah ! ,hizi ni dharau za wazi kabisa.Wananchi kitu hawajui wana dharauliwa sana na wana Siasa.Imekuwa kama mchezo wa Paka na Panya dah.Yani ukakope Bank kwa Vitambulisho vya aina hii !!?.
 
Back
Top Bottom