hivi Kijana mkakamavu na Mzee aliekongoroka na kuchoka mwili na akili na alieshindwa uchaguzi kwa miaka sitini tangu uhuru ukiwa na akili zako timamu unachagua yupi?
hao wawili wakishindana kutimua mbio nani atashinda? wakishindana kick box nani ataua mwenzake? wakishindana kupiga kasia kutoka mchambawima kupitia mji Mkongwe, Nungwi kisha Kojani , Jang’ombe , Bububu, hadi mferejiwima nani atashinda? wakishindana kula pweza, uduvi, ngisi na chaza nani atamaliza bakuli kubwa? wakishindana kula urojo na mapembe nani ataibuka kidedea?
wakipiga push up mchangani nani atapiga nyingi?
hata hakuna haja kupiga kampeni kijana keshashinda kabla ya mechi!!
kijana anawaza kujenga nyumba ya familia, mzee anawaza kujenga nyumba yake peke yake tena huko Oman!!
wazenji tuchague kilicho bora!! Mzee hana maajabu tena kwanza ni kinyonga leo kavaa nyeupe kesho kijani!!