Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote

Norway wana SWF ya mifuko ya hifadhi ya jamii.
Rwanda wanafanya hii pia ya kuhakikisha kila raia anapata bima ya afya.
Wanafanya je wamefanikiwa kwa kiasi gani?
Je hizo nchi zina uchumi wa kiasi gani na zimekuwa kwenye stability ya uchmi kwa muda gani na zinafanya hayo tangu lini baada ya kuwa huru na kuwa na uchumi wa juu?
 
Rwanda ana uchumi wa Juu? Mkuu lolote linawezekana kma mnawekza Trillion 7+ kwa SGR unadhani ingewekwa kwenye SWF izungushwe ili iendeshe Bima bila hasara unadhani ingeshindikana?

Hapo piga hesabu ya opportunity cost... Pesa wanayotumia kugharamikia afya wataitumia kwa vitu vingine ambavyo serikali itakata kodi huko pia!! Masuala ya uchumi ni complex sana hakuna linaloshindikana ukiamua na kuweka nguvu zote huko!
 
Watu wenye upeompana wa ufahamu wa mambo wanataka Lissu afafanue fedha za mambo yote anayoahidi anazitoa wapi kama ni kodi basi aseme.

Kama JPM kashindwa kuongeza ajira yeye Lissu ataongeza ajira atazitoa wapi?.sio kupayuka tu kama anakula ugali na mrenda.
Shule hazina walimu, hospitali hazina madaktari, ofisi nyingi za halmashauri hazina watumishi, mahakama hazina mahakimu na makarani.

Hizo zote ni ajira ambazo Magufuli kashindwa kuajiri kwa kufuja pesa za walipa kodi kujenga uwanja wa ndege kwao.
 
Iko kwa trump
Kampeni za uchaguzi zishaanza.

Wagombea wanakatiza nyika sehemu mbalimbali za nchi kuzinadi sera zao. Wanatoa kila aina ya ahadi. ‘Mimi nitafanya hivi, nitafanya vile, nitafanya haya, nitafanya yale’.

Sasa mimi ni mmoja wa watu ambao huwa sitegemei mwanasiasa au mtu mwingine kuniboreshea maisha yangu. Naamini hilo jukumu linaanzia na kuishia kwangu mimi mwenyewe. Nimemsikia mgombea wa CHADEMA akitoa ahadi tele. Ahadi zinazowapagawisha misukule wake.

Moja ya ahadi anazotoa ni ile ya bima ya afya kwa wote. Yaani kila mtu, kila raia, eti awe na bima ya afya. Mimi si mtaalamu wa mambo ya bima wala mambo ya afya. Na wala sina ‘usomi’ wowote ule. Nimeishia kidato cha nne tu [emoji1787][emoji6]. Hivyo, huenda nikawa na uwezo mdogo wa kuelewa na kuchanganua mambo.

Katika ahadi zake hizo, sijasikia namna ambayo mgombea huyo wa CHADEMA ataweza kumpatia kila raia hiyo bima.

Hizo hela atazitoa wapi? Ataenda kuziomba kwa nchi hisani? Ataongeza viwango vya kodi ili kuongeza mapato yatayotumika kuileta hiyo bima? Au ataomba kwa Mungu atudondoshee hizo hela toka mbinguni?

Ahadi ni tele. Namna ya kuzifanikisha ahadi hizo, mpaka sasa ni sufuri!

Oh, na jingine ambalo sijamsikia kabisa akilizungumzia ni hili suala la Corona.

Kulikoni wewe mbeba maono wa CHADEMA? Ushakubali sasa kuwa Corona haipo? Au ushakubali kuwa ipo, lakini si hatari kama tulivyolishwa matango pori na Wazungu?

Manake we mwenyewe tokea urudi, zaidi ya mwezi sasa, huvai cha barakoa na wala hujitengi na jamii!

Unajichanganya kama ilivyo ada na sijakuona hata mara moja ukipiga chafya wala kukohoa.

Kwenye suala la Corona, hata kama huwezi kukiri kwa sauti, nahisi kimoyomoyo unakubaliana na jinsi Ngosha alivyoamua kukabiliana nalo[emoji6].

Sisi akina Ngosha hatukutishika. Mfano mimi, hakuna hata siku moja niliyojifungia ndani. Sijawahi kuvaa barakoa. Na bado nipo nadunda nikibeba maboksi tena yale mazito kwelikweli ilhali kuna watu eti mpaka leo hii wamejifungia ndani kama mwali.

Mangosha wa ukweli hawawezi kujifungia ndani wakiogopa mafua na kikohozi[emoji1548][emoji1548].
 
Rwanda ana uchumi wa Juu? Mkuu lolote linawezekana kma mnawekza Trillion 7+ kwa SGR unadhani ingewekwa kwenye SWF izungushwe ili iendeshe Bima bila hasara unadhani ingeshindikana?

Hapo piga hesabu ya opportunity cost... Pesa wanayotumia kugharamikia afya wataitumia kwa vitu vingine ambavyo serikali itakata kodi huko pia!! Masuala ya uchumi ni complex sana hakuna linaloshindikana ukiamua na kuweka nguvu zote huko!
Unaelewa maana ya bima wewe,
Hiyo SGR itawasaidia watu kufanya shughuli zao za kibiashara na kuweza kulipa bila wenyewe kwa kiwango wanachoweza kuliko kusubili bila ya bei nafuu ambayo kuna sehemu hutibiwi.
Ukizungumzia hayo mataifa makubwa kwenye miundi mbinu walishamaliza sasa ndo wanaboresha maisha ya watu wao.
 
Wapi nimesema SGR haifai? Nilichosema kma kuwekeza Trl 7 imewezekana je ndio mshindwe bima ambayo watu wanachangia kwa kuangalia income bracket?
Rwands kufikia 2016 zaidi ya 95% walikua na bima ya Afya. Najua utasema ni nchi ndogo.... Ila ambacho hujui tumewazidi GDP mara 7 ila ssi hatuna hta mkoa mmoja ambao coverage ya bima ni walau 50%!!

Hakuna linaloshindikana ukiamua
 
Back
Top Bottom