The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Katika hali isiyo ya kawaida mtoto (15) amekamatwa kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi Seneta wa Colombia anayewania kuwa rais ajaye wa nchi hiyo.
Katika tukio hilo, seneta Miguel Uribe Turbay (39) akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kampeni yake uliofanyika Bogota nchini humo alijeruhiwa vibaya katika shambulio la mtoto huyo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ya nchini humo, Seneta huyo alipigwa jana Jumamosi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika bustani eneo la Fontibon, Mji Mkuu wa Colombia, Bogota.
Ofisi hiyo ilieleza kuwa Turbay alipigwa risasi mbili kutoka nyuma na washambuliaji waliokuwa na silaha kisha kuonekana akitokwa damu kichwani huku akisaidiwa na wasaidizi wake na watu waliokuwa kwenye mkutano huo, kama inavyoonyeshwa kwenye video iliyosambaa mitandaoni.
Kulingana na ripoti ya kitabibu kutoka Hospitali ya Santa Fe Foundation nchini humo, Turbay alilazwa hospitalini humo akiwa katika hali mahututi na bado anafanyiwa upasuaji wa mfumo wa neva na wa mishipa ya damu.
Mkewe, Maria Claudia Tarazone, aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa X kwamba mumewe “anapigania uhai wake” huku akiwahimiza raia wa Colombia kumuombea.