The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
ni ngumuKituo kinacho fata kiwe ni kizimkazi maushungi, amen.
Wanangu Bado wachanga Sana siwezi comment HIVI @Kituo kinacho fata kiwe ni kizimkazi maushungi, amen.
Hatari sanaKatika hali isiyo ya kawaida mtoto (15) amekamatwa kwa tuhuma za kumshambulia kwa risasi Seneta wa Colombia anayewania kuwa rais ajaye wa nchi hiyo.
Katika tukio hilo, seneta Miguel Uribe Turbay (39) akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kampeni yake uliofanyika Bogota nchini humo alijeruhiwa vibaya katika shambulio la mtoto huyo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ya nchini humo, Seneta huyo alipigwa jana Jumamosi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika bustani eneo la Fontibon, Mji Mkuu wa Colombia, Bogota.
Ofisi hiyo ilieleza kuwa Turbay alipigwa risasi mbili kutoka nyuma na washambuliaji waliokuwa na silaha kisha kuonekana akitokwa damu kichwani huku akisaidiwa na wasaidizi wake na watu waliokuwa kwenye mkutano huo, kama inavyoonyeshwa kwenye video iliyosambaa mitandaoni.
Kulingana na ripoti ya kitabibu kutoka Hospitali ya Santa Fe Foundation nchini humo, Turbay alilazwa hospitalini humo akiwa katika hali mahututi na bado anafanyiwa upasuaji wa mfumo wa neva na wa mishipa ya damu.
Mkewe, Maria Claudia Tarazone, aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa X kwamba mumewe “anapigania uhai wake” huku akiwahimiza raia wa Colombia kumuombea.
View attachment 3360631
hio nchi ngumu sana ukiwatetea wananchi jamaa wa madawa wanakufuata, ukiwatetea jamaa wa mdawa ndo wananchi hawakupi kura 🤣 🤣Colombia wa tatizo kuwa la wauza madawa ya kulevya yaaani ukiwa una gombea ukajifanya unawataja taja mara nikiwa raisi nitawamaliza wote .... huwa hawana muda wa kupoteza wanakumaliza kabla hujawa raisi
Pia mexico huko wanasiasa wanauliwa daily kuanzia wabunge ... mameya .... drug cartels za huko ni hatari uwezo wao ni millitary level... wanamiliki kila silaa za kijeshi ...pia wana training za kijeshi so ukiwa mwanasiasa huko ukileta unoko jiandae
Halafu wanakuambia somalia ni failed state....mi naona hata wao ni failed state piahio nchi ngumu sana ukiwatetea wananchi jamaa wa madawa wanakufuata, ukiwatetea jamaa wa mdawa ndo wananchi hawakupi kura 🤣 🤣
Colombia wa tatizo kuwa la wauza madawa ya kulevya yaaani ukiwa una gombea ukajifanya unawataja taja mara nikiwa raisi nitawamaliza wote .... huwa hawana muda wa kupoteza wanakumaliza kabla hujawa raisi
Pia mexico huko wanasiasa wanauliwa daily kuanzia wabunge ... mameya .... drug cartels za huko ni hatari uwezo wao ni millitary level... wanamiliki kila silaa za kijeshi ...pia wana training za kijeshi so ukiwa mwanasiasa huko ukileta unoko jiandae
ingekuwa ni waislamu ungeanza kusikia story za ugaidi