Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kujibu maswali ya wananchi watumiao mitandao

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kujibu maswali ya wananchi watumiao mitandao

Heko kwenu, tunaimani na Platform hii ya JF kujadiliana/kutoa na kupokea habari mubashara hapa Tanzania. Keep it up Guys for Tanzanians, wengine wamelegezwa na kudhibitiwa.
Tunaomba tuendelee kuhabarishana kupitia hii forum ya Wananchi wazalendo; The Great Thinkers.
 
KILIO CHANGU NI KWENYE MADINI JE HUYU MTU ATAWEZA KUYALINDA ILI YALINUFAISHE TAIFA AM NOT HAPPY WITH MBOWE HAWATATUMIA FURSA NI KUJITAJIRISHA KUPINDUKIA? JE WATALINDAJE KURA ZAO? JE WATAWALINDAJE WALINDA KURA WAO ILI WASINUNULIWE NCHI NZIMA KUTOKANA NA HALI MBAYA MNO YA UKWASI WATU WALIYONAYO/ ENDAPO KURA ZITAIBWA NA WAKAJUA ZIMEIBWA NI NINI WATAFANYA ILI KUTWAA NCHI BILA KULETYA VURUGU WALA KUMWAGA DAMU/
 
Moderator sijajua ni njia gani atakayo tumia kujibu hayo maswali.
Nilikuwa naomba au nashauri apewe Airtime kwenye media yoyote iwe live. Kama itashindikana basi hata kwa online Tv kama wanavyo fanya Dar mpya inasaidia sana.
Akijibu kwa maandishituu hainogi sana wengine wavivu wa kusoma lakini pia kusoma mtu huwa anakuwa na tafasiri tofauti na kusikia.
 
Muheshimiwa makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu,wewe kama kiongozi wa Chadema na wenzio mmeshindwa hata kujenga ofisi nzuri ya chama.

mpaka sasa mnapanga,mtaweza kweli kuijenga Tanzania ikiwa taasisi ndogo kama chama mmeshindwa pamoja na kupewa ruzuku kilamwaka na kuchangisha wabunge wenu fedha kilamwaka?
 
Je umeunda kikosi kazi chochote cha kijeshi cha kuokoa demokrasia nchini iwapo NEC haitokutangaza mshindi kama umeshinda kweli???
 
mheshimiwa lisu vp maslah ya watumishi wa umma umepanga kuyaboresha kwa namna gani?
 
Tunamuomba amkumbushe Magufuli ule mdahalo wetu hasa kipindi hiki amepumzika
 
Swali langu ni kwa namna gan mawakala watakuwa salama?
Watahapishwa
Hilo limeshaulizwa jana .wewe endelea kusubiria majibu

na wengine ambao bado mana maswali nadhani mda wa kukusanya maswali umeisha,so tuendelee kusubiri majibu
 
Mods muwe makini na team ya wapopoaji wasije wakaupopoa Uzi na huu usahili kwa Mgombea Lissu ukaingia DOA.

Chondechonde
 
Vipi ikiwa atashinda Urais na ushahidi wa kimazingira utaonesha kuwa kashinda na tume ya uchaguzi haikumtangaza mshindi, atachukua hatua gani kudai haki yake ? Akizingatia kwamba Matokeo yakitabgazwa hayapingwi mahakamani!
 
Back
Top Bottom